Goodride: Je, ni tairi bora kwa barabara zetu au tunadanganywa na bei yake nafuu?

Goodride: Je, ni tairi bora kwa barabara zetu au tunadanganywa na bei yake nafuu?

danhoport

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2020
Posts
2,116
Reaction score
4,885
Wakuu, habari za majukumu.
Leo nataka tuguse mada ambayo kila mwenye gari itamfika tu—muda wa kubadili tairi. Kuna hii brand ya Goodride imetawala sana soko letu. Kila duka unalopita utaikuta, na bei yake ukiilinganisha na majina makubwa kama Michelin au Dunlop, utaona kuna utofauti mkubwa sana wa bei.

Swali ambalo wengi wanajiuliza (hata mimi nilijiuliza mwanzo): Je, hii tairi ni ya kweli au ni zile za 'mchina' za msimu mmoja?

Baada ya kufuatilia na kuona uzoefu wa wateja wangu wengi, nimegundua mambo kadhaa kuhusu Goodride ambayo pengine huyajui:

Rubber Compound (Uimara wa Raba): Tofauti na tairi nyingi za bei rahisi ambazo huwa ngumu (plastiki), Goodride ina raba inayohimili joto kali la lami zetu bila kuanza kupata nyufa (cracking) mapema.
Kelele na Comfort: Kwa tairi ya bei hii, utulivu wake barabarani ni wa kushangaza. Haina ule mlio wa 'vuvuzela' unaopatikana kwenye tairi nyingi za kichina.

Mtego wa 'Used': Watu wengi wanakimbilia tairi used za Japan kisa ni brand kubwa. Lakini kiukweli, tairi used ni kamari ya maisha yako. Heri ya Goodride mpya ya mwaka huu kuliko tairi used iliyokaa stoo miaka minne Ulaya.
Uzoefu wa Bei (Kwa wastani):
Kwa sasa, ukiwa na bajeti ya kuanzia 115,000/= (kwa size ndogo) mpaka 215,000/= (kwa SUV/R17), unaweza kupata Goodride mpya kabisa na ukasahau habari ya tairi kwa mwaka mmoja au miwili mbele.
Mimi msimamo wangu ni huu; kama huna mamilioni ya kununua brand za Ulaya, Goodride ndio "Best Value for Money" kwa sasa hapa Bongo.
Wadau, ninyi mnaotumia hizi tairi uzoefu wenu ukoje? Inakaa muda gani kabla ya kuisha treads?
Tupeane uzoefu hapa chini ili kusaidia na wengine wasiojua.
 
Goodride ilikuwa zamani sasa hv wamezichakachua sana hazifai tena. Watumiaji wengi tumeshaziacha. Na wengi sana wanazikimbia sasa hivi, labda wazalishaji wabadilike, tofauti na hapo watapotea sokoni
 
Sisi wenye gari za 4wd goodride tunaifunga tairi za mbele , nyuma tunaweka road cruza kwa ajili ya traction.
 

Attachments

  • 20fe1a8c-f818-47af-8b11-86d53dbf044e.jpeg
    20fe1a8c-f818-47af-8b11-86d53dbf044e.jpeg
    223.7 KB · Views: 27
Back
Top Bottom