Google Earth itasaidia kuishangaza dunia juu ya kazi za Rais Samia

Google Earth itasaidia kuishangaza dunia juu ya kazi za Rais Samia

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Mchakamchaka wa kujenga madarasa nchi nzima utaishangaza dunia kupitia Google Earth waki update image zao by January 2022. Nchi itakuwa imejaa mijengo tu nchi nzima.

Huwezi amini Kuna shule naijua imepewa madarasa kumi kwa mpigo. Hakyanani mama unajua kucheza draft bila mbwembwe. Watu wengi Sana hasa wa kipato Cha chini wanaenda kupata kazi kwenye hii miradi . Mama piga kazi.
 
Mchakamchaka wa kujenga madarasa nchi nzima utaishangaza dunia kupitia Google Earth waki update image zao by January 2022. Nchi itakuwa imejaa mijengo tu nchi nzima. Huwezi amini Kuna shule naijua imepewa madarasa kumi kwa mpigo. Hakyanani mama unajua kucheza draft bila mbwembwe. Watu wengi Sana hasa wa kipato Cha chini wanaenda kupata kazi kwenye hii miradi . Mama piga kazi.
Trip to Trip from one continent to another. One day she will go to Antarctica to wonder some bulk of frozen ice.
I sit in the front row....waiting for that changes.
20211031_082443.png
 
Swala sio madarasa swala ni kuwa je,tutaendelea kuzalisha wanafunzi wanaokuja kukosa ajira mpk lini..?
Ulitaka wakae nyumbani wazaane tutengeneze familia za malumpeni? Yasiyojua kusoma na kuandika?
 
Ikiwa maisha yako yanadundika kwa kufuata midundo ya wanasiasa ujue basi wewe ni taahira au ni kabwela nusu kaputi so huna ujanja wa kujiongeza kujikomboa na familia yako, au ndio umeshajikatia tamaa.

Elimu ya Tanzania kupitia serikali ni elimu ya kijinga sana, hamna la maana zaidi ya kuridhisha takwimu tu kwamba mwaka huuwamemaliza hawa, ufaulu ulikuwa sijui alama hii, tumetoa mikopo kiasi hiki na maujinga kibao.

Hiyo mikopo ya kumpatia mtu miaka mitatu angewekeza kwenye ufugaji au kilimo lazima angekuwa sehemu nyingine nzuri kuliko kugraduate na kirudi kijiweni hana mbele wala nyuma na madeni juu.
 
Mchakamchaka wa kujenga madarasa nchi nzima utaishangaza dunia kupitia Google Earth waki update image zao by January 2022. Nchi itakuwa imejaa mijengo tu nchi nzima. Huwezi amini Kuna shule naijua imepewa madarasa kumi kwa mpigo. Hakyanani mama unajua kucheza draft bila mbwembwe. Watu wengi Sana hasa wa kipato Cha chini wanaenda kupata kazi kwenye hii miradi . Mama piga kazi.
Dunia hawezi shangazwa kwa mambo ambayo yalibidi yawe yamefanyika miaka 30 iliyopita. Dunia inashangazwa na mambo mengine makubwa mkuu siyo haya ya watu tuna mito na mabonde lakini kuna watu hawapati maji ya kunywa na huku kwetu bunju leo siku ya 3 maji hayatoki kwenyye mabomba 🤣
 
Ikiwa maisha yako yanadundika kwa kufuata midundo ya wanasiasa ujue basi wewe ni taahira au ni kabwela nusu kaputi so huna ujanja wa kujiongeza kujikomboa na familia yako, au ndio umeshajikatia tamaa....
Umeongea point kubwa sana. Ili jambo nilishawahi kulifikiria kuhusu bodi ya mikopo ya elimu ya juu, niliwaza kuwe na bodi ya mikopo ya wahitimu wa kidato cha sita kwa ajili ya biashara ndogo ndogo na wawekewe mfumo mzuri wa kurejesha.

Wakishakuwa wakubwa kiumri ndio waamue kwenda kusoma kwa fedha zao. Bodi ya mikopo ya elimu iwepo ila iwe na ya mitaji ya wahitimu

Ajira limekuwa [emoji378] bomu kubwa sana na mwisho wa siku litakuja kutulipukia wenyewe. Wamachinga walioondolewa mjini baada ya miezi sita tutegemee wizi kuongezeka, vitendo vya kiharifu kama madawa ya kulevya, bangi na kujiuza vitazidi sana.

Kama Taifa inabidi iwekwe mikakati imara kuweza kunusuru wahitimu vijana kukosa shughuli za kufanya
 
Mchakamchaka wa kujenga madarasa nchi nzima utaishangaza dunia kupitia Google Earth waki update image zao by January 2022. Nchi itakuwa imejaa mijengo tu nchi nzima...
Bado mnajikomba kwa mliowaita mabeberu ili mtumie teknolojia zao?
 
Ulitaka wakae nyumbani wazaane tutengeneze familia za malumpeni? Yasiyojua kusoma na kuandika?
Jengeni madarasa huku mkiangalia na mitaala inazalisha nini hicho ndo chamuhimu acha kampeni zako tu za kusifu.
 
Mzee vp ndo kitengo na praise team awamu hii nn,naona nyuzi zinaongozana tu za sifa na mapambio
 
Back
Top Bottom