Ndipo hapo kinapotakiwa kiwepo kipimo cha nani zaidi kati yao,maana wewe utasema huyu na mwingine atasema yule, yupi ni zaidi ya mwenzie hamtajua,ndio maana wenye fani zao wakaja na suluhisho la huo utata nao ni, YUPI ANATENGENEZA PESA NYINGI KUTOKANA NA KAZI ZAKE ZA MUZIKI. YAANI IKO HIVI (KANUNI HII JINSI INAVYOFANYAKAZI ) KAMA MUZIKI WAKO UNAPENDWA NA WENGI KULIKO MWENZAKO BASI WEWE UTAUZA SANA KULIKO HUYO MWENZAKO KWASABABU ANAYEKIPENDA KITU ATAKIGARIMIA KUKIMILIKI,NDIO HATA UKIFANYA SHOO ZAKO HATA KAMA BEI ZAKO ZIKO JUU ZAIDI YA MWENZAKO BADO WEWE UTAJAZA NA UTAZIFANYA SHOO NYINGI KULIKO MWENZAKO. Hii ndio kanuni nyepesi sana kuishika,na ndio hata kwenye maisha ya kawaida mwenye bidhaa nzuri ndio atakayeuza sana,kinyume na hapo ni HISIA,AMBAZO HAZINA NAFASI KWENYE DUNIA ILIYOSONGA MBELE KIMAENDELEO. Huwezi kusema eti fulani ni zaidiya fulani,japo yeye hauzi sana kuliko mwenzake,hiki kitakuwa ni kichekesho.