Graduate wenye Start Up Business Tukimbilie Wapi?

Graduate wenye Start Up Business Tukimbilie Wapi?

kijana13

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
1,981
Reaction score
3,631
Habari wakuu.

Nimepita baadhi ya taasisi za kutoa mikopo kama mabenki na Microfinance nikiwa na vielelezo vya usajili wa biashara(Tin ,lesseni na business registration name) pia niña mchanganuo wa biashara. Lakini hakuna aliye tayari kunikopesha maana biashara yangu ni start up. Nafahamu sí vizuri sana kukopa ukiwa unaanza biashara lakini ukipata mkopo wenye marejesho nafuu unaweza mudu vizuri.

Katika uanazishaji nimefikia hatua nzuri na nimebakiza kiwango kama 1.5 mill nianze biashara yangu. Wandugu nipeni msaada wa mawazo au sehemu nayoweza saidiwa kupata hicho kiasi, kama kuna mkopeshaji naweza lipa kwa miezi 3 na dhamana ni assets za nyumbani.

Natanguliza shukrani.
 
Kwanza nikupongeze kwa kuamua kujiajili.

Nataka kufahamu ni aina gani ya biashara unayotaka kuanzisha?
 
bro ningekupa ushaur na badala ya kukopa, ni kwa nin usitafte partners ili mjiunge na muwe kama wanahisa yan unatafta watu mpaka ikifika 1.5Mil then unafunga mkataba na mnaanza biashara.Mtazamo wangu tu
 
kupata mikopo yakuanzisha biashara kwenye mabenki ni ngumu sana labda kama ungekuwa unaikuza biashara, silazima uwanze na biashara yenye mtaji mkubwa sana unaweza kuanza na biashara ya mtaji mdogo kidogo kidogo kisha ikakupa faida kubwa yakuanziasha biashara hiyo yako ya mtaji mkubwa.
 
bro ningekupa ushaur na badala ya kukopa, ni kwa nin usitafte partners ili mjiunge na muwe kama wanahisa yan unatafta watu mpaka ikifika 1.5Mil then unafunga mkataba na mnaanza biashara.Mtazamo wangu tu
yani mkuu upo sawa kabsa,kua na partner wakuchanga nae ina sound poa,tumejarbu na tumeweza!biashara yetu ya vpodoz iko mbion kuanza,ushaur mzur!
 
mkuu mikopo inalemaze sana na kukufanya uwe mtumwa wa mabank nakusihi usipende sana kukopa hasa wewe ambeye huna mtaji kuna wakati utaichukie hiyo biashara,bora mara mia utafute mbia au mtu binafisi akukopeshe maana hawezi kukusumbua kama mabank...kila la heri
 
kama unataka kukopa walau mfano wewe uwe na mtaji wa m 3 ukope m 1!
sio wewe huna kitu alafu unakopa au una m1 unakopa 3 utafurahia huo mkopo miezi mitatu ya mwanzo na baada ya hapo utaanza kukimbia biashara mara simu unazima!
 
anza kuwa wakala wakuuza mikate na kek za wenzako uku ukijichanga kuanzisha icho kiwanda chako,utakuwa napakutengenezea napakuzia mkuu
 
Naona vema ukaanza kwa kutafuta marafiki au ndugu wenye hiyo amount muwe partners,maana hata mambo yasipoenda vizuri watakuelewa na kukuvumilia
 
anza kuwa wakala wakuuza mikate na kek za wenzako uku ukijichanga kuanzisha icho kiwanda chako,utakuwa napakutengenezea napakuzia mkuu

mm nadhani huu ndo ushauri mzuri na huitaji mtaji mkubwa kama una milioni moja inatosha, for example unaweza utumie laki mbili kwa kutengenezea sherufu, na kodi ya kibanda, tumia laki nne kuchukulia mikate na keki then laki nne iliyobaki utacheck ramani zingine any way nimetoa mchanganuo kidogo tu, then ukishajulikana unaweza kutengeneza ya kwako na ukaunganisha na mikate hiyo na viwanda vingine , patiner wa biashara uwe makini ndugu yangu wekeni mikataba harari maan huko mbele biashara ikishakua inaleta shida kidogo ni experience katika hilo
 
Back
Top Bottom