Graduates sikilizeni kutoka kwa malegend wa kitaa...

Graduates sikilizeni kutoka kwa malegend wa kitaa...

Kuna mwanangu alimaliza dip alichapika mpaka akabaki na suruali moja ili watu wasimuone kauka nikuvae akaanza kutembea usiku kama bundi.Alichapika haswa akanikopa cash akaenda kusoma driving.Shukrani Kwa sakata la vyeti feki akapata kazi Tanesco mambo safi.Tatizo lake moja tu kasahau alipotoka.
Usisite kumkumbusha, enzi anatembea usiku kama Bundi na suruali moja
 
Sio utani after college nilipiga kazi ya saidia fundi that time day walikuwa wanalipa 10K lakini kupata hiyo kazi ilikuwa ni connection pia.

First day kupiga hiyo kazi sikulala mwili wote unauma, kubeba zile tofali nzito si kazi ndogo.
Day two nikaenda tena, kesho yake nikaenda tena nilipiga kama wiki mwili ukazoea lakini mwili wote unapauka na simenti.

Manzi yangu hakuniacha, that time alikuwa anasoma chuo anamalizia mwaka mmoja, hakusita kunisapoti alipopata boom

Namshukuru sana, sasa ndiye mke wangu
Mungu ni mwema life linaenda tuna watoto kadhaa[emoji1431][emoji1431]
 
Kuna mwanangu alimaliza dip alichapika mpaka akabaki na suruali moja ili watu wasimuone kauka nikuvae akaanza kutembea usiku kama bundi.Alichapika haswa akanikopa cash akaenda kusoma driving.Shukrani Kwa sakata la vyeti feki akapata kazi Tanesco mambo safi.Tatizo lake moja tu kasahau alipotoka.
Usisahsu ushauri wa wahenga kuwa "tenda wema nenda zako, usingoje shukrani"

JESUS IS LORD
 
Unamaliza chuo ukiwa na connection zako kadhaa, lakin ukishaanza kuwafatilia kuhusu hizo kazi wanaleta mada zao za kula tunda, unaamua kupotezea na kuwaza njia njia nyingne za kupata kipato
 
Aliyeko Chuoni hawezi ona haya.
Kila mtu anaamini akimaliza Chuo atapata tu Mchongo wa kufanya. Baada ya muda ndio uhalisia unajidhihirisha.

Hata wale wadada wajasiriamali vyuoni huwa wanaacha.
Mtaani n changamotooo
 
Mtaani ni kubad asikwambie mtu. Mimi nimeacha chuo baada ya masuala ya ada kunipiga chenga na familia haina pesa. Nikaamua kurudi zangu nyumbani tu, huu ni mwezi wa sita sasa kila unakoomba kibarua hakuna yaani hadi zile zisizohitaji elimu kubwa hata darasa la saba anafanya hakuna kudadeki[emoji21].
Kibaya zaidi nikikutana na washkaji wananiambia mwanetu unanenepa tuu maisha safi ila hali yangu ya mkunga nikijikuna natoka unga. Bado tunasaka chochote cha kufanya ili mradi tusiwe mzigo kwa familia. Nachukia sana utegemezi especially nikijiangalia najiona umri unazidi kwenda.
Ila hopefully mambo yatakaa vyedi tu.
InshAllah ni kipindi cha mpito
 
Aliyeko Chuoni hawezi ona haya.
Kila mtu anaamini akimaliza Chuo atapata tu Mchongo wa kufanya. Baada ya muda ndio uhalisia unajidhihirisha.

Hata wale wadada wajasiriamali vyuoni huwa wanaacha.
Hujakosea mkuu, wakati nipo chuo nilikua nikiongea na mtu akanambia hajapata kazi naona kama atakua alizingua hivi ndio maana aisee, ukweli ni kwamba akili za darasasni hazihusia na kutoboa kwenye maisha.
Ni Mungu tu akiamua kukufungulia riziki
 
Nikisoma posts za wadau nazidi kumshukuru Mungu. Naomba tu anisamehe kama kuna muda nanung'unika. Kiukweli sijapitia 80% ya waliyopitia wadau. Sijapata kazi na sina mpango wa kupata kazi lakini Mwenyezi hanisahau kamwe. Nimejiajiri mtaji wangu ni computer, router na internet bando.
Kujiajiri pia ni kazi
 
Back
Top Bottom