Usisite kumkumbusha, enzi anatembea usiku kama Bundi na suruali mojaKuna mwanangu alimaliza dip alichapika mpaka akabaki na suruali moja ili watu wasimuone kauka nikuvae akaanza kutembea usiku kama bundi.Alichapika haswa akanikopa cash akaenda kusoma driving.Shukrani Kwa sakata la vyeti feki akapata kazi Tanesco mambo safi.Tatizo lake moja tu kasahau alipotoka.
Anavimba sana kijana hashauriki.Usisite kumkumbusha, enzi anatembea usiku kama Bundi na suruali moja
Usisahsu ushauri wa wahenga kuwa "tenda wema nenda zako, usingoje shukrani"Kuna mwanangu alimaliza dip alichapika mpaka akabaki na suruali moja ili watu wasimuone kauka nikuvae akaanza kutembea usiku kama bundi.Alichapika haswa akanikopa cash akaenda kusoma driving.Shukrani Kwa sakata la vyeti feki akapata kazi Tanesco mambo safi.Tatizo lake moja tu kasahau alipotoka.
Kuna chawa halafu kuna masikini jeuriHahahahah kujikomba ni kipaji kama ufupi na urefu [emoji2956]! Wengine ni maskini jeuri tu tunakufa na tai shingoni kama ipo ipo!!!
Mtaani n changamotoooAliyeko Chuoni hawezi ona haya.
Kila mtu anaamini akimaliza Chuo atapata tu Mchongo wa kufanya. Baada ya muda ndio uhalisia unajidhihirisha.
Hata wale wadada wajasiriamali vyuoni huwa wanaacha.
InshAllah ni kipindi cha mpitoMtaani ni kubad asikwambie mtu. Mimi nimeacha chuo baada ya masuala ya ada kunipiga chenga na familia haina pesa. Nikaamua kurudi zangu nyumbani tu, huu ni mwezi wa sita sasa kila unakoomba kibarua hakuna yaani hadi zile zisizohitaji elimu kubwa hata darasa la saba anafanya hakuna kudadeki[emoji21].
Kibaya zaidi nikikutana na washkaji wananiambia mwanetu unanenepa tuu maisha safi ila hali yangu ya mkunga nikijikuna natoka unga. Bado tunasaka chochote cha kufanya ili mradi tusiwe mzigo kwa familia. Nachukia sana utegemezi especially nikijiangalia najiona umri unazidi kwenda.
Ila hopefully mambo yatakaa vyedi tu.
Hujakosea mkuu, wakati nipo chuo nilikua nikiongea na mtu akanambia hajapata kazi naona kama atakua alizingua hivi ndio maana aisee, ukweli ni kwamba akili za darasasni hazihusia na kutoboa kwenye maisha.Aliyeko Chuoni hawezi ona haya.
Kila mtu anaamini akimaliza Chuo atapata tu Mchongo wa kufanya. Baada ya muda ndio uhalisia unajidhihirisha.
Hata wale wadada wajasiriamali vyuoni huwa wanaacha.
Dah....na tuliosaini mikataba ya ajira kabla hatujagraduet tunacomment wapi? 🤣🤣🤣🤣Tunaruhusiwa na sisi darasa la tatu C kutoa uzoefu wetu baada ya kuacha shule kitaa kilikuaje
Kujiajiri pia ni kaziNikisoma posts za wadau nazidi kumshukuru Mungu. Naomba tu anisamehe kama kuna muda nanung'unika. Kiukweli sijapitia 80% ya waliyopitia wadau. Sijapata kazi na sina mpango wa kupata kazi lakini Mwenyezi hanisahau kamwe. Nimejiajiri mtaji wangu ni computer, router na internet bando.