Graduates sikilizeni kutoka kwa malegend wa kitaa...

Graduates sikilizeni kutoka kwa malegend wa kitaa...

entry

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
286
Reaction score
539
Ile unatoka zako chuo unarudi nyumbani mwezi wa kwanza unapita kuna vitu vinaanza kutokea.
1. Usb yako inakufa
2. Sendo zinakatika
3. Jeans yako pendwa inachanika
4. Cadet zinapauka
5. Unaachwa na mpenzi wako.
Tuongeze vingine vingine
 
Unakosa hata jero ya vocha, unapoteza mpaka confidence halafu mademu ndio wanazidi kuwa wakali mamaaaee.

Zile illusion ulikuwa nazo kuwa ukimaliza chuo unapata kazi unamiliki ghetto kali na chuma chakutembelea zinayeyuka kama barafu mbele ya jua.

Ukimpigia mtu simu anakata hapo hapo hata kama unataka kumpa salamu anadhani unataka kupiga ukware.
 
Ukitoka chuo,ndani ya mwezi mmoja,mawasiliano na mates wako huwa yanaanza kupotea,maana kila mtu anaanza kuiona reality ya kitaa vzr.

Kuna watakao pata ajira mapema(hii huwa ni bahati tu).

Nakumbuka baada ya chuo,nipo kitaa wiki moja bila deal,kumbe Kuna kampuni moja mpya imetangaza kazi kwenye gazeti,sina cm,taarifa nilizipata kwa email kupitia kwa class mate.
Hiyo ilikuwa 10yrs ago!
Hii leo si balaa
 
Unamaliza na mtaji wako kiasi fulani , wazo la biashara unalo ili ukianza kutekeleza mambo yanaenda ndivyo sivyo !!

Mtaji unakatika [emoji3][emoji3][emoji3] michongo inagoma kabisa !! Kampuni za usafi hawachukui watu , saidia fundi mpaka connection daaah[emoji43]
 
Acha Mkuu hii hali niliipitia kabisa

Na nilibakia kichwa Tu

Ashukuriwe Mungu hata Kwa hii stage niliyobarikiwa but I dream higher!
Ile unatoka zako chuo unarudi nyumbani mwezi wa kwanza unapita kuna vitu vinaanza kutokea.
1. Usb yako inakufa
2. Sendo zinakatika
3. Jeans yako pendwa inachanika
4. Cadet zinapauka
5. Unaachwa na mpenzi wako.
Tuongeze vingine vingine
 
Mi nilianza kujikomba kwa bro,

Nikawa nambrashia viatu vyake,

Nikawa naosha gari yake, nikikuta silesile na fegi nachukua, sometimes vikonyagi vimesalia siviachi salama,

Nikisikia honi anavorudi, nawahi getini kumfungulia, na lazima nimpige ngeo,

Mungu ni mwema nikaja kuotea mchongo, nikasahau zile shida hata bando la jero utata, ikawa ni kuwabandua tu...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom