Nilikutana na kimbunga cha uchumi kuyumba 2016 mishe zote zikafa. Nikafungua mgahawa mwananyamala biashara ikagoma ,ikabidi nitengeneze toroli ili iwe mobile kitchen.
Nikawa napika chapati ,nilianzia posta pale kituo kinapakana na usalama wa taifa,tra na mamlaka ya bandari. Baishara ilikua nzuri kweli ila usalama wa taifa wakanitimua. Nikahamia na toroli langu kigamboni nako biashara inawa ngumu Sana,kimara,mbezi kote hola.
Nikaamua kubeba toroli langu mkoani mbeya,nimepambana soweto kama miezi 6 hola. Huku nasikia maneno tu huyu amechanganyikia make amesoma ulaya saizi ilitakiwa awe na kazi nzuri tu.
Baada ya mapambano ya muda mrefu gizani sasa jua limewaka. Waliokua wanasema mbovu wanajificha huku wengine wakijisogeza karibu ili waonje keki ya mafanikio. Maisha ya kutafuta hela inatakiwa kujikana nafsi tu ,usione aibu kwani njaa ni yako na familia yako. Unaemuonea aibu ndiye awe mteja wako wa kwanza.