Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi



Bro mi nakuelewa from the beginning umeongea point sana. Thanks in advance
 
Technology ndio inasaidia vijana sana zaidi kuliko hata hiyo serikali yako.

Imagine magroup ya kibiashara ya whatsapp, facebook inatoa matangazo kila uchao ya biashara kama platform. Uber je, hivi haujui uber, bolt na wengineo imeajiri vijana wengi sana, mpesa, tigo pesa, halopesa, NMB wakala, CRDB wakala na wengineo wameajiri vijana kujitafutia kipato.

Hapo nimekutajia tu sehemu chache namna technology imeweza kuajiri raia kuliko serikali yako hiyo ya kimbweha.
 
Ndugu Mimi na kuelewa sana tena sana cha msingi wewe muombe Mungu na endelea kuweka bidii katika jambo lako hali uliyo kuwa nayo Mimi nili kuwa nayo mwaka 2013 hadi 2015 Mimi na elimu yangu ya master's nilisha wahi weka cheti ndani na kufanya shughuli za umachinga za kuuza nguo viatu na mikoba ya vitu vya kitamaduni nime zunguka sana maeneo ya mitaa ya Dodona..

Nikaja nikaanza Fanya shughuri za ushauri wa uandishi wa research paper pamoja na data analysis yani Nina stori ngumu sana kwangu ila hayo yote kwa sasa namshukuru Mungu mambo sio mabaya sana Mungu ni mwema sana kwangu napambana na mwanga ameni onyesha sija ajiriwa nime jiajiri mwenyewe mtaani maisha yana kwenda kuna walio kuwa wana nitolea dhihaka

Leo tuna salimiana kwa heshima never never never never never never never never naweka tena msisitizo never never give up piga goti chini kila siku omba Mungu huku ukipambana najuwa hali unayo ipitia sababu mm pia nili kuwa Muhanga wa hiyo hali aiseee acha tu kuna siku nami nitakuja kuweka stori yangu humu na ikiwezekana Nita wapa watu chansi waje waone kile ninacho kifanya.. Na kiasi cha maendeleo ambayo Mungu amenibariki kupitia hiyo kazi mpaka sasa
 
Hapa mboa sasa unakuwa una engage katika debate ya "Money is the source of all evil"
 
Mzee baba shida hazikwepeki lazima zikutoe jasho ili upate akili ya kuandaa kesho mbon ata ss tuko kazin lkn wakuu wa idara wanatutukan kibao had unataman kukimbia
 
Ukweli mtupu,hapo uliposema mafundi wa mtaani,wana uhakika wa kula kuriko Graduate,ni kweli kabisa,
Unakuta mtaani kuna kijana anapiga tiles,anapata tenda kibao,anaendesha maisha yake vzr,kuriko graduate wa civil engineering,anaeshinda nyumbani,akingojea ajira,

Siku moja,nilijaribu kutafuta hizi tenda za kufunga umeme wa majumbani,(Mimi ni muhandisi wa umeme),nikakosa,hebu fikiria,ujenzi unaoendelea Dodoma,wewe na degree yako,unakosa hata kazi moja ya wiring,lakini wale vijana,waliotoka VETA,wananetwork kubwa,na wanazipata hizo kazi,

Ikabidi nikae chini nijaribu kutafiti kwanini na Mimi nisijenge huo mtandao,elimu yetu ya juu,inafundisha kiburi cha kudharau kazi hizi ndogo,Graduate anataka afanye kazi,Tanapa,Tigo,uamihaji,nk.

Pale mtaani ninapoishi,kuna kijana,ni Fundi Bomba,anaweka mifumo ya maji na mifumo ya maji taka,vile vile anaboda boda take,anapiga kazi,anafamilia,na amejenga,ufundi alifundishwa na kaka yake,.

Sasa tujiulize sie graduates,kama vijana was dalasa LA saba,wanaanza na mtaji kidogo,wanajenga maisha,kwanini Sir,ambao tayari tuna mtaji mkubwa wa exposure na elimu.

Kitu kingine,wadogo zangu,kama wewe ni graduate,mfano wa kada ya engineering ya umeme,unayajua makampuni yanayofsnya shughuri za power,na electrical engineering?

Tafuta hizi taarifa,usiishie kuandika tu barua,yajue makampuni,yapo wapi,wajue seniors wa hayo makampuni,msisubiri mpigiwe honi,na kuulizwa unaenda mjini,ili upewe lift,uliza uliza uliza,acheni kuona noma.

Hata hapo unapoishi,unaweza kukuta jirani yqko yupo kwenye kwenye kampuni,na anaweza kukusaidia,uliza.

Juzi nilikuta kijana,wife kampa amuoshee gari,nikauliza,akasema ni mtoto wa jirani,kamaliza form 4,kapata zero,anatafuta ajira,mzee wake ni mstaafu,nikamuuliza wife,kwanini,hukuniambia nije niongee nae,maana,hapo mtaani,tunaishi na watu waliokwenye taasisi ambao wanaweza kutoa msaada,
Vijana msikae kimya,fungukeni,sio kushinda mna chart tu,
 
Daa kweli mkuu. Ushauri mzuri sana, naamini wengi watakaosoma hapa watakuelewa .
 
Mzee baba shida hazikwepeki lazima zikutoe jasho ili upate akili ya kuandaa kesho mbon ata ss tuko kazin lkn wakuu wa idara wanatutukan kibao had unataman kukimbia
Kweli mkuu
 
Mkuu kwanza niseme hongera sana kwa uthubutu wako. Pili ikiwezekana uje uandike kidogo kuhusiana na hiyo story naamini utatupa mwanga kwa namna moja ama nyingine. Mwisho tu nikutakie mapambano mema na mungu akujaalie kwa kile unachokifanya
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…