Gray Mgonja, mwenye kuonja vinavyoonjwa!

Gray Mgonja, mwenye kuonja vinavyoonjwa!

Hivi inakuwaje hakuna anayetaka kumshitaki mwenziwe??;
1. List of Shame vs Dr. Slaa
2. Dr. Slaa vs Mtikila n.k.

Huko mahakamani haki haitendeki au wahusika wanaogopa kitu gani?

Ni hivi mkuu, hawa watu wanaujua kwa uzuri msemo huu "we are standing on slippery ground, don't push me!"
 
makala ya leo tanzania daima

Kwa hili, sitakuacha Mgonja
Kulwa Karedia

“NIACHENI na ufisadi wangu jamani, kwani sina zaidi ya kueleza katika suala hili.”

Hayo ni maneno ya utangulizi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja, aliyoyatoa mwishoni mwa wiki alipotakiwa na gazeti hili kuzungumzia uamuzi wake wa kufungua kesi baada ya kutajwa katika orodha ya aibu iliyohusisha watu 11 katika tuhuma za ufisadi.

Nasema kauli ya Mgonja kwamba aachwe na ufisaidi wake, haiwezi kuingia akilini hata kidogo, kwa kuwa tuhuma hizi ni nzito kwa mtendaji huyo muhimu kwenye wizara nyeti.

Nasema mtendaji muhimu kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye anashughulikia masuala ya wizara nyeti, hivyo anaelewa vizuri mianya ya kuingiza na kutoa kila kitu.

Kabla sijaanza kumzungumzia, naomba niwakumbushe kwamba huyu Mgonja kwa mara ya kwanza alitajwa kwenye kikosi cha watu 11 waliohusishwa na ufisadi (first eleven) na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam.

Baada ya kutajwa kwenye kikosi hicho, kinachoonekana kutokuwa na wachezaji wa akiba (reserve), Mgonja aliamua kuzungumza na waandishi wa habari kwa nia ya kueleza azima yake ya kufungua kesi dhidi ya tuhuma hizo.

Lakini, kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, tulishuhudia vigogo kadhaa wakiumbuka, ghafla Mgonja na timu yake ya ushauri walikaa kimya hadi sasa anapotaka aachwe na ufisadi wake.

Kwanza, kitendo cha kushindwa kufungua kesi kama alivyotangaza awali, kinaashiria wazi kwamba, Mgonja analo neno zito moyoni kama si ufisadi, basi atakuwa analijua mwenyewe, lakini ni bora akawa wazi hivi sasa.

Sasa, mwaka mmoja umepita tangu alipotoa uamuzi wa kufungua kesi dhidi ya Dk. Slaa, lakini ameendelea kuwa ‘bubu’ katika hili.

Katika mkutano huo, Mgonja alisema tuhuma zote zilikuwa na nia ya kumpaka matope, uzushi na upotoshaji mkubwa mbele ya jamii, sasa hapa nikubaliane na Mgonja au Dk. Slaa? Nadhani Dk. Slaa alikuwa katika nafasi ya juu.

Naamini Mgonja ameshikwa kihoro kutokana na ukweli kwamba wahusika wengi wa ‘first eleven’ wamepata pigo, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.

Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, tumeshuhudia viongozi kadhaa akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, wakijiuzulu nyadhifa zao.

Licha ya Lowassa kujiuzulu kutokana na kashifa ya Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, wengine waliosalia wametoka kwenye kikosi hicho ambacho sasa tunaamini kinazidi kupwaya siku hadi siku.

Kama vigogo hawa walifikia uamuzi wa kuondoka madarakani, nini kilichomzuia Mgonja asing’oke licha ya kuandamwa kiasi hiki jamani!

Mgonja amekuwa mfanyakazi wa serikali kwa miaka 33, anatumia maneno haya kutaka abaki na ufisaidi wake. “Tafadhali niache nibaki na ufisadi wangu, maana sitaki kabisa kuzungumzia suala hili, wewe nenda lakini uadilifu wangu ndio ulionifanya niwe kazini kwa muda wote huu.”

Kama Mgonja unaelewa wazi uadilifu wako ndio umekuweka madarakani kipindi chote hicho, umeshindwa nini kutumia uadilifu huo huo kujiuzulu ili uwe mfano kwa viongozi wengine?

Binafsi nasema umefika wakati sasa Watanzania tuseme tumechoshwa kuongozwa na wanaotuhumiwa.

Ninaufahamu urafiki wako na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, bila kumsahau ‘swahiba’ Basil Mramba.

Naelewa majina hayo niliyoyataja hapo juu yalivyolalamikiwa na Watanzania wakati wakiwa madarakani.

Wananchi walishuhudia ununuzi wa rada na ununuzi wa ndege ya rais haya yote ni mzigo mzito ambao tunaendelea kubebeshwa na kuulipa kupitia kodi zetu.

Napenda kumwambia Mgonja kwamba tuhuma zinatokana na machungu ya maisha yanayowakabili wananchi, kama unavyosema mwenyewe kuwa ni mwadilifu, umefika wakati sasa kukaa kando na kuwapa imani watu wengine kuhusu uadilifu wako.

Kwa nini viongozi wetu wanataka kuondolewa madarakani kwa ‘viboko’ hawana utamaduni wa kuondoka wenyewe bila kushinikizwa na kupigiwa kelele kila kukicha?

Mfano mzuri tumeuona kwa Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, aliyeshinikizwa kujiuzulu, naye bila kipingamizi amekubali kwa kauli moja. Huo ndio utawala bora unaozingatia masilahi ya taifa.

Mgonja akumbuke kilio hiki kinatokana na matumizi mabaya ya fedha za wananchi maskini wanaovuja jasho kila siku iendayo kwa Mungu huku wakipigwa jua barabarani.

Lakini Mgonja na wenzake wamekuwa watumiaji wa magari aina ya VX Land Cruiser, maarufu kama ‘mashangingi’, hawajui kabisa kama wapo wazalendo wanataabika mitaani.

Tunaamini kwamba kama serikali ikisema leo ifanye uchunguzi wa kina kwa kila kiongozi hapo wizarani kwako, kuanzia wewe na wengine, hakuna atakayebaki, kutokana na ukweli kwamba wengi wamejichotea mamilioni ya fedha zetu.

Wakati sasa umefika kwa Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko katika Wizara ya Fedha na Uchumi, kwa kumwondoa Mgonja, wakurugenzi na wasaidizi walio chini yake, kwa kuwa naamini kabisa kwamba wanao mtandao, hivyo usipovunjwa tutabaki kulalama tu.

Mgonja, sitakuacha hata kidogo. Nitaendelea kupambana na wewe hadi utakapoondoka kwenye wadhifa huo.


Mungu ibariki Tanzania.
 
Shutuma dhidi ya Mgonja ni za Kweli.Sio siri kwamba kwa njia moja au nyingine amewatumbukiza watanzania kwenye dimbwi la umaskini.Sasa ata achwa je huru?Kama angetaka kuwa salama asinge wadokolea watanzania.Kauli yake haikubaliki.
 
Only In Tanzania Kiongozi Jambazi kama Gray Mgonja anaweza kuongea maneno ya kipumbavu kama hayo na hakuna implications zozote dhidi yake, kusema ukweli we are doomed.
 
Na yeye "atuachie hazina yetu" akatumbue mapesa yake US huko...
 
Tunahitaji mfumo wa uongozi nchini ambao umma utakuwa na uwezo wa kuwawajibisha hata wateule wa rais
 
Only In Tanzania Kiongozi Jambazi kama Gray Mgonja anaweza kuongea maneno ya kipumbavu kama hayo na hakuna implications zozote dhidi yake, kusema ukweli we are doomed.

Geeque,
Good to see you again. Usiwe una lost muda mrefu hivyo.
 
Geeque,
Good to see you again. Usiwe una lost muda mrefu hivyo.
Nipo nipo Mazee Jasusi ila nilikuwa busy kidogo na mihangaiko ya hapa na pale lakini bado tupo tupo sana hapa kuendeleza mapambano, good to see u too my brotha.
 
Mgonja: Niacheni na ufisadi wangu

Kwa kuzingatia uzito wa tuhuma zilizotolewa kwa nia mbaya ya kunipaka matope na hasa nikizingatia uadilifu wangu wa miaka 33 bila kuwa na shutuma au kashfa ya aina yoyote, ili haki itendeke nimeamua kutumia mkondo wa sheria kwa kufungua kesi mahakamani dhidi ya Dk. Slaa, gazeti la Mwana Halisi na Kiwanda cha Printech kilichochapisha matoleo hayo,” alisema.


Mkuu hapa sijamuelewa kabisa hive ni uadilifu au uanamtandao wa miaka 33
Tunavyo fahamu sisi kazi kafanya miaka 10 tu na hiyo miaka 23 amekua dhalimu tuu
 
..nadhani kwa suala la Gray Mgonja wananchi tutapiga kelele mpaka makoo yapasuke.

..ubadhirifu anaohusishwa nao unaihusu CCM na kampeni za kumchagua RAISI wetu wa sasa hivi.

..Gray Mgonja angekuwa ameiba bila kuwashirikisha CCM, na kuwagawia mtandao, basi angeingia kwenye matatizo kama yale yaliyomkuta Balozi.Costa Mahalu.
 
Mgonja: Niacheni na ufisadi wangu
.....
Najaribu kuikumbuka hii kauli...

Mgonja alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki, alipotakiwa kueleza hatima ya azima yake ya kutaka kufungua kesi dhidi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na wenzake.
Hii kesi sijui anaifungua lini...
Akijibu swali hilo kwa jazba, Mgonja alisema hana cha kueleza juu ya sababu iliyomfanya ashindwe kufungua kesi hiyo hadi leo na kuwataka waandishi wa habari kumwacha na ufisadi wake.

“Bwana hilo ni langu, niache na ufisadi wangu, sina lolote la kukueleza,’’ alisema.
Nice to read these stuffs at this moment!

Alipobanwa zaidi ataje ni kitu gani kimemchelewesha kufungua kesi na lini anatarajia kuifungua baada ya mwaka mzima kupita, Mgonja alikataa katakata kuzungumzia suala hilo.

“Tafadhali niache na ufisadi wangu, maana sitaki kabisa kuzungumzia hilo, wewe nenda, niache na ufisadi wangu, lakini uadilifu wangu ndio ulionifanya niwe kazini kwa miaka 33 sasa,” alisema Mgonja.
Uadilifu wangu...

Septemba 26 mwaka jana, 2007, Mgonja alifanya mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa hatajiuzulu wadhifa wake na kwamba anakusudia kumshitaki Dk. Slaa na wenzake kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi yake.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha, Mgonja alisema shutuma za Dk. Slaa na wenzake si za kweli, bali ni uzushi na upotoshaji uliolenga kuchafua jina lake.

“Kwa kuzingatia uzito wa tuhuma zilizotolewa kwa nia mbaya ya kunipaka matope na hasa nikizingatia uadilifu wangu wa miaka 33 bila kuwa na shutuma au kashfa ya aina yoyote, ili haki itendeke nimeamua kutumia mkondo wa sheria kwa kufungua kesi mahakamani dhidi ya Dk. Slaa, gazeti la Mwana Halisi na Kiwanda cha Printech kilichochapisha matoleo hayo,” alisema.
Maneno hayo...!

“Nitafungua kesi mapema iwezekanavyo na si lazima mjue kampuni itakayosimamia kesi yangu na wala siwezi kutaja kiasi cha fidia nitakachodai, nitasema mahakamani fidia nitakayodai,” alisema Mgonja.
Mkwara mkali... Na soon atafungua kesi dhidi ya serikali...

Wengine waliotajwa katika kashfa hiyo na kuahidi kufungua kesi ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Patric Rutabanzibwa.
Hawa bado tu...

Wengine waliotajwa katika kashfa hiyo lakini hawakusema kama wangekwenda mahakamani ni Rais Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.
Am speechless...

Yumo pia aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Basil Mramba, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), marehemu Daudi Ballali.
List hiyo hapo juu inanikumbusha mengi... Kumbe mmoja hatunaye! Lakini wengine taratibu tunaweza kuwafikia...!

Just recalling 🙂
 
Only In Tanzania Kiongozi Jambazi kama Gray Mgonja anaweza kuongea maneno ya kipumbavu kama hayo na hakuna implications zozote dhidi yake, kusema ukweli we are doomed.
Hapana, serikali yetu haijalala...
 
Wakuu,

Mbona siyo mimi niliyepost hii thread? Sijui mods na tecnician mnaseamaje hapa.Kuna mtu katumia jina langu
 
Back
Top Bottom