kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Wakoloni walitusafirisha kwa majahazi kama watumwa kwenda kwao kuwafanyia kazi bure (manamba) kwenye mashamba, viwanda na majumbani kwao, history mbaya sana hii kukumbukwa, maana sio tu kwenda kuwafanyia kazi wazungu bure lakini wengi wao walikufa njiani wakati wakisafirishwa kwa kutoswa majini, msongamano mkubwa, njaa na ugonjwa njiani.
LEO hii miaka 60 baada ya uhuru sababu zilezile za kusafirisha manamba kwenda Marekani, Ulaya na uarabuni ndio sababu hizihizi za watu kwenda huko kwa Green card lottery, Jamani hali hii ni mpaka lini? what are you looking for? Kilichobadilika tu leo ni kitu kimoja tu kutoka manamba walionunuliwa kwenye masoko ya watumwa hadi kwenda kwa green card na baadhi ya sifa za watu wanaohitajika kusafirishwa na aina ya usafiri. Wakati ule walihitaji watu vijana wenye nguvu za kufanya kazi za wakati ule na sasa hivi kwa kutumia green card wanahitaji watu vijana wenye afya wenye elimu na ujuzi maalum kwaajili ya kufanya kazi za wakati huu.
Hii ni kujitafutia balaa wewe mwenyewe na familia yako kwa matumaini feki kabisa huku ukijua kuwa utakwenda kule kufanyakazi kubwa na nyingi sana ili upate chochote kitu wakati nguvu, juhudi na akili hizo ungeweza hata kuziwekeza hapahapa nchini kwako na kupata mafanikio makubwa sana ya ajabu pamoja na kutoa mchango kwenye ujenzi wa taifa lako kwa njia za kodi, tozo na huduma kwa jamii yako.
Jaamaani, Si shauri uombe hiyo kitu, nyambafu!!!!