wewe unafikiri kwanini huko marekani mtoto anaweza kuingia darasani na bunduki na kuua kila mtu humo? unafikiri hawana akili? hujiulizi mara mbilimbili? Upweke (loneliness) na stresses zimejaa huko. Wewe hujiulizi hata akina Kelly wako jela na wana mihela mingi? sio hela tu bali fikiria na mambo mengine kaka.
Kavulata, nadhani kidogo umesema , tunaangalia mambo mengi tunapotaka nje ya nchi, wewe huangalii mambo mengi kama unavyoonyesha, nikiangalia kwa mtazamo wako huo Afrika hapakaliki pia! Sina haja ya kusema wewe unajua wazi!
Napoangalia shule za msingi, madarasa ya vijijni. kukosa maji. umeme, huduma za afya, ukosefu wa ajiri ambao unaleta burden ya extended family, kwani kila anayejaribu kujikwamua kwenda juu, unaanza kazi ukoo mzima kukuvuta chini, kibinadamu unahitajika kutoa msaada, wewe mwenyewe unataka kusonga mbele, ni tatizo linalomkabili kila mwafrika, lakini bado watu wanaishi.
Kwa kifupi adha za maendeleo na kero zake zipo, lakini faida yake ni kubwa kuliko adha za umaskini, na watu wanaishi! Niko Marekani sioni tabu kabisa na hiyo unayosema loneliness! Siwajui majirani zangu, na wao hawanijui, tunapungiana mikono tunapokutana nje tukiingia kwenye magari yetu kila mtu akienda kwenye shughuli yake! Kuna sehemu nyingi mno Marekani za kuondoa hiyo unaita loneliness! Kuna community functions ukitaka! Unapenda kusoma, library ziko kila kona za bure utapata kitabu unachotaka, CDs za Movies za kuazima kwa kadri yako, Gyms, parks za kutembea na kupumzika nk!
Hivyo Mkuu tunapokuja huku tunafikiri mambo mengi pia! Kama na mimi nikitaka kurudi Tanzania inabidi niangalia mambo mengi pia! Mgao wa umeme/Maji, unreliable internet, siwezi kutaka kitu Amazon nikakipata kwa siku mbili! Na ningekuwa na watoto wadogo ningehangaika kuhusu elimu yao! Marekani hilo halina shina kabisa! Kusaidia ndugu zangu, ambao karibu kila Mtanzania ana msururu mrefu wa kusaidia! Dola zangu 400- 500 nazotuma Tanzania kusadia ndugu zangu kwa mwezi, ingekuwa ni ngumu mno kuwasaidia nikiwa bongo! labda ningekuwa Waziri!
Hivyo naomba uwe na broader perspective ya kuangalia mambo! Halafu inanisikitisha mno kuona mtu wa leo unataka kuua spirit ya adventure kwa wale ambao wanataka kujaribu! ! Nawaheshimu wazungu kwa hilo, wanatoka, wanatembea, wanajaribu, ni risk takers! Wengi wetu hata hapo Tanzania ni mikoa michache umefika, tena kikazi, sio kutembea, kuona maisha mbali mbali.
Kwa kifupi sikuja Marekani nikitokea bongo! Nimekatisha West Africa, Far East na nikatua Marekani! Bado nataka kutembea na kuona! Is part of my DNA!
Waacha wanaotaka kujaribu wajaribu! Usiwe mwoga! Maisha ni popote pale, hata bongo kwa upande wako!