Dawa ya hiyo sio Green Cards. Yaani iko hivi, Wamerekani wanatafuta cheap labour kwa njia hii ya Green card, watu ambao watafanyakazi bila kulalamika wala kudaidai ziada. Zamani walikuwa wakitumia watumwa kufanyakazi lakini sasa watumwa hakuna. Ndio maana kwenye Green card sio kila mtu anaweza kupata hiyo nafasi kwakuwa wanafanya kitu kinaitwa job matrix kuona ni kazi zipi zipo zinazohitaji watu wenye sifa zipi na hakuna watu wa kuzifanya. Sponsor wakubwa wa Green cards ni chama cha waajili ambao wanatuma nafasi zilizowazi kwenye makampuni yao zinazohitaji watu wangapi wenye sifa gani.
Mara nyingi hizo ni kazi ambazo wazawa hawazipendi, hivyo zinakosa watu wa kuzifanya sio kwakuwa hakuna wamerani wa kuzifanya lakini hawapendi kuzifanya, yaani hata kwenda kusoma kozi za kufanya aina hiyo ya kazi hawasomi kabisaaa.
Lakini kuna jambo lingine hapo pia lazima ulifahamu kuwa, mfumo wa elimu Marekani ni kwamba Elimu ni rahisi sana kwenye shule za msingi na sekondari na vyuo vya kati (non degree programs) vya serikali ili watu wengi wamudu kusoma na kuishia hapo. Elimu ya vyuo vikuu wameifanya iwe ghali sana kusoma ili watu wachache hasa wale wa makabwela washindwe kuipata. Huu ni mkakati madhubuti wa kuwapata cheap labour (non degree holder workers) katika job market. Kwa hiyo kuna uhaba mkubwa wa wataalam wenye elimu ya juu kwenye maeneo mengi muhimu kama walimu wa vyuo vikuu, IT, uchumi, nurses, dk, etc, Hivyo watu wenye elimu kubwa ni rahisi kupata visa au hata hiyo Green card kuliko mtu mwenye elimu ya kati. Huu ni umanamba wa hali ya juu na wizi wa wataalam waliosomeshwa na nchi maskini kabisa.