Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Unasahau kabisa mababu zako, kama wewe ni mbantu walitokea Benue, West Nigeria! kutafuta malisho ya mifugo na mengineyo ndio wewe uko Tanzania! Wangeng'ang'ania huko sijui wewe ungelikuwa wapi! Na kama wewe Nilotic mngekuwa mmenga'ngania Gezira Sudan, hali duni, vita iliwasababishia kuondoka!

Nimekujibu hapo chini, Kwako wewe Uzalendo ni kukaa nchi yako katika hali ya duni na shida na kukataa options nje ya nchi yako, ambazo zinaweza kubadili maisha yako! Huo sio uzalendo ni udwanzi!

Sijui kama umesoma historia kuhusu Human migration " People may choose to migrate for variety reasons, such as employment opportunities, to escape violent conflict, environmental factors, educational purposes, or to reunite with family" Na kwenda wengine kama unachanganya na adventures!
Unatakiwa ubadili hali ya mambo kwenye jamii yako, siyo kupenda kuteleza kwenye ganda la ndizi kwenye jamii ambazo wao walipambana kupata maendeleo waliyo nayo, kifupi unakuwa huna tofauti na mkimbizi na ukimbizi kama ulivyo utumwa siyo jambo la kujivunia.​
 
Nyamisi: Kama una wito wa kufanya hivyo , kila la heri! Join CCM, Chadema, NCCR, una options nyingi mkuu! Za kuibadili nchi yako!
That is not my calling! Kila la heri! Pambana mkuu! Acha mimi niteleze kwenye Ganda la ndizi!!
 
Unatakiwa ubadili hali ya mambo kwenye jamii yako, siyo kupenda kuteleza kwenye ganda la ndizi kwenye jamii ambazo wao walipambana kupata maendeleo waliyo nayo, kifupi unakuwa huna tofauti na mkimbizi na ukimbizi kama ulivyo utumwa siyo jambo la kujivunia.​

Unatakiwa ubadili hali ya mambo kwenye jamii yako, siyo kupenda kuteleza kwenye ganda la ndizi kwenye jamii ambazo wao walipambana kupata maendeleo waliyo nayo, kifupi unakuwa huna tofauti na mkimbizi na ukimbizi kama ulivyo utumwa siyo jambo la kujivunia.​
Unasema pambana kubadili nchi yako, huku unalalamika tozo! Nalipa kodi US, kodi yangu inajenga miundo mbinu, nikiita ambulance haichukui dakika 10 roughly, watoto wanakula shule! Maji au umeme sio tatizo! Public packs na recreational centers ziko kibao, ni kodi yangu hiyo!
Sasa wewe unatoa tozo, V8 ndio zinashamiri! Pambana mkuu! Maisha mafupi haya! Labda utaikwamua Tanzania! Kila la kheri!
 
Ingependeza kama ungewatumia huu ujumbe kwenye official site mail yao kuliko kuandika hapa maana hakuna mchezaji atakayekusikiliza
Wakoloni walitusafirisha kwa majahazi kama watumwa kwenda kwao kuwafanyia kazi bure (manamba) kwenye mashamba, viwanda na majumbani kwao, history mbaya sana hii kukumbukwa, maana sio tu kwenda kuwafanyia kazi wazungu bure lakini wengi wao walikufa njiani wakati wakisafirishwa kwa kutoswa majini, msongamano mkubwa, njaa na ugonjwa njiani.

LEO hii sababu zilezile na manamba ndio hizihizi sa Green card lottery, Jamani hali hii ni mpaka lini? what are you looking for?

Hii ni kujitafutia balaa wewe mwenyewe na familia yako kwa matumaini feki kabisa huku ukijua kuwa utakwenda kule kufanyakazi kubwa na nyingi sana ili upate chochote kitu wakti nguvu, juhudi na akili hizo ungeweza kuziwekeza hapahapa nchini kwako na kupata mafanikio makubwa sana ya ajabu.

Si shauri uombe hiyo nyambafu
 
Unasema pambana kubadili nchi yako, huku unalalamika tozo! Nalipa kodi US, kodi yangu inajenga miundo mbinu, nikiita ambulance haichukui dakika 10 roughly, watoto wanakula shule! Maji au umeme sio tatizo! Public packs na recreational centers ziko kibao, ni kodi yangu hiyo!
Sasa wewe unatoa tozo, V8 ndio zinashamiri! Pambana mkuu! Maisha mafupi haya! Labda utaikwamua Tanzania! Kila la kheri!
Huwezi hamia nyumba ya jirani kisa kwako pana kunguni, kila mtu atakushangaa...
 
Huwezi hamia nyumba ya jirani kisa kwako pana kunguni, kila mtu atakushangaa...
Kitendo tu cha kuwa na kunguni ni aibu! Mkuu nakutakia kila kheri, pambana kulipa tozo! Jipange barabarani kuwashangilia wenye ma V8! Ni hatua nzuri hiyo ya kuleta maendeleo! Kila la kheri mkuu!
 
Huwezi hamia nyumba ya jirani kisa kwako pana kunguni, kila mtu atakushangaa...
Sio kunguni tu, chawa, mende, inzi, mbu, buibui! Nyoka, popo, mijusi! Pambana mkuu, is more than kunguni unazopambana nazo!
Viongozi wa nchi wao wanajua wanapambana na nini, ndio maana wanatafuta wadau angalau walete vyandalua, na kuchimba Massimo ya choo! Huwa inaumiza sana! Sasa kama wewe umejitoa mhanga, kila la kheri!
 
Kitendo tu cha kuwa na kunguni ni aibu! Mkuu nakutakia kila kheri, pambana kulipa tozo! Jipange barabarani kuwashangilia wenye ma V8! Ni hatua nzuri hiyo ya kuleta maendeleo! Kila la kheri mkuu!
Unatakiwa kuondoa aibu ndani ya nyumba yako, siyo kuhamia nyumba ya jirani........unapohamia jamii ya watu wengine unapoteza identity na unakuwa hauko huru na maisha yako.
 
Unatakiwa kuondoa aibu ndani ya nyumba yako, siyo kuhamia nyumba ya jirani........unapohamia jamii ya watu wengine unapoteza identity na unakuwa hauko huru na maisha yako.
Ondoa mkuu hiyo aibu! Sijui identy gani nimepoteza! Ni wabongo wangapi hawajitambui! Ukiona donors wanakuchimbia vyoo vya shimo, wanaleta vyandalua na wawekezaji wanakuja kuuza maua ya plastics,huko ndio kupoteza identity...
 
Mkuu, ndugu yetu kajaa negativity kubwa! Marekani is not a paradise, lakini ukiwa na makaratasi ukakomaa utapata unachokitaka!
Jamaa yetu hakubali, amekaririshwa hataki kabisa kusikia unaweza ukafanikiwa Marekani.
Nadhani hata hapo bongo kila anayefanikiwa kwake ni Illuminati!Au mchawi!
Mkuu,Hebu usijichoshe kubishana na hawa wapinga green card wana matatizo ya kisaikolojia na Uwehu akilini mwao.
 
Unatakiwa kuondoa aibu ndani ya nyumba yako, siyo kuhamia nyumba ya jirani........unapohamia jamii ya watu wengine unapoteza identity na unakuwa hauko huru na maisha yako.
Ondoa mkuu hiyo aibu! Sijui identy gani nimepoteza! Ni wabongo wangapi hawajitambui! Ukiona donors wanakuchimbia vyoo vya shimo, wanaleta vyandalua na wawekezaji wanakuja kuuza maua ya plastics,huko ndio kupoteza identity
 
Ondoa mkuu hiyo aibu! Sijui identy gani nimepoteza! Ni wabongo wangapi hawajitambui! Ukiona donors wanakuchimbia vyoo vya shimo, wanaleta vyandalua na wawekezaji wanakuja kuuza maua ya plastics,huko ndio kupoteza identity...
Mkuu, nimeishi huko for at least miaka 3 wakati nipo masomoni.....sipachukulii kipaumbele sana kiasi kwamba nikose usingizi kisa nimeshindwa kufanikiwa kuhamia majuu. Mimi nachulia hapa nilipozaliwa ndo jamii yangu ilipo na ni mahali sahihi zaidi pa mimi kuishi.....ikitokea nafasi ya kutafuta huko kwingine itokee, but home is always the best place to be.​
 
Nyumisi, hapo umezungumza la maana,naheshimu perspective yako! Mimi nilianza kuja Marekani miaka ya nyuma kikazi, na kwa upande wangu nikaona ni mahali sahihi pa kufanya nachotaka kufanya, na hata kuchukua uraia,
Sasa sioni hiyo Diana ya utumwa na kukosa uzalendo inatokea wapi! Wewe unajua fika, hali mojawapo ya kukosa maendeleo hapo nyumbani ni kwa viongozi hao hao mlio nao kukosa uzalendo!
Viongozi hao hawajaja Marekani,bali wanaibia wananchi mchana kweupe!
Hivyo acha kila mtu atafute mstakabali wake wa maisha Kadri anavyoona mwenyewe! Msiwakatishe tamaa wanaotaka kujaribu.Kila la kheri!
 
Watz tuna akili dumazi sana. Mi ingekuwa ni uwezo wangu ningewatoa watanzania waende huko mbele angalau mwaka mmoja watz wanatakiwa wapate exposure ni wajinga mno huwez kuendelea bila kutoka ukajifunze mapya.
hata usijaribu maana sku ya kuwarudisha kwao hakuna hata mmoja atayetaka arud zaidi utakimbiwa
 
Daah! umenena, nini nafahamu kuwa furahi ya mtu haitokani na kuwa na pesa nyingi tu bali mjumuiko wa mambo mengi na hela ikiwemo. Nimekutana na kijana ambae huko majuu ambae analala kwenye gari yake maisha, nilipomuuliza kwanini kwanini huna chumba chako aliniambia ninafanya kazi shift 3 kwa siku hivyo muda wa kulala sina, hata hiyo nyumba naona nitapoteza pesa zangu bure wakati silali humo. Akanambia ana madeni mengi yanayohitaji ku service (kulipa) hivyo lazima afanye kazi zaidi ya 1 ili apate ziada. kaka kijana huyu hajawahi kula chakula cha nyumbani kwake zaidi ya kule fast foods mitaani, makato mengi na anashindwa kutuma pesa nyumbani maana wafyeka hela nyingi sana. kaka kuna mitaa/maduka/malls ukiingia mwenye ngozi nyeusi wanadhani huna pesa ya kuingia hapo bali unataka kuiba, ubaguzi bado haujakwisha tunalazimisha tu.

Nguvu, muda, juhudi, maarifa na akili mnazozitumia kumudu kuishi huko hata zingewekezwa japo nusu tu kwenye jangwa zingetoa matunda. Vijana wetu huku ni wavivu sana ni wavivu sana na ni wavivu sana ndio maana wanapata tamaa ya green card wakidhani huko US pesa ziko kwenye viroba tu ni za kuzoa na kutumia.

Kama asili na chanzo kikuu cha ushoga huko ni maisha magumu, watu wanaunganisha nguvu ili kumudu maisha bila kulazimika kuwa na watoto wa kutunza, yaani kuona mwanamke ni kuongeza ugumu kwenye ugumu. bahati mbaya mimi nimeishi huko sana tena vijijini kabisa ambako maisha ni kama haya hapa ya tandika na kwamtogole, kuchafu na idadi kubwa ya ombaomba wazungu mitaani ambao wanapatiwa nguo kule salvation army na kwingineko kwenye malls kama vile Walmart zenye madirisha ya watu maskini (wazungu) kupatiwa misaada.

kaka usiwadanganye watu ukawapa hope na kuja kuishia kuolewa na wanaume wenzao, wanaofanikiwa ni watu kidogo sana kati ya hao wahamianji. Wengi wao wanaishia kwenye vyombo vya usalama kufungwa na hata kuuliwa.
Japo sijawahi kuishi huko lakini mzee bongo life ni tough sana.

Huenda wewe ni mwenyeji wa dar, huko vijijini hujaenda kuona watu wana maisha magumu kiasi gani.

Sikiliza tu story ya majaliwa, uone maisha ya familia ya dogo yalivyo magumu, pesa anapata kwa kuanika dagaa ambayo huenda hata yeye tu haimtoshi.

Ajira hakuna, wati viwandani wanalipwa buku 3 kwa siku ndgu yangu, si bora huko walau ela unaiona japo gharama za maisha zipo juu lakini somehow haki za binadamu zinafuatwa.
 
Unachosema wewe ni sawa na house girl ambae anafanyakazi kwa boss wake kuanzia alfajiri na kulala saa 5 usiku baada ya kumalizia kumfungulia na kumlisha mbwa kutoka bandani kwa ujira wa TZS 60,000 kwa mwezi. Lakini msichana huyu alipokuwa kwao alikuwa anaamka saa 2 asubuhi, kuzurura, kuangalia TV na kwenda kulala saa 2 usiku.

Nguvu, juhudi na muda anaotumia kufanyakazi kwa boss kama angetumia nusu tu ya nguvu,juhudi na muda kufanyakazi akiwa nyumbani kwao hata kwa kuchoma vitumbua na maandazi na kuyauza angepata pesa nyingi zaidi hukohuko kwao kuliko hizi 60,000 za boss.

Fursa ziko hapahapa nyumbani Tz ni kuacha uvivu. Nilimkuta kijana mmoja Marekani anaona aibu kurudi Tz kwakuwa wenzake aliowaacha TZ walikuwa na maendeleo makubwa sana kuliko yeye. Wenzake wameoa, wana mashamba ya miti Iringa, wamejenga kule Goba, shamba kubwa la kuku, wana magari na ardhi kubwakubwa tu. Visa yake na passport vimekwisha lakini anashindwa kurudi kurudi kwa kuogopa kuwa atadakwa kwa makosa hayo pia.

Hebu waambieni ukweli vijana wenu.
Yaani nyie mnaoonaga ambao hawajafanikiwa ni wavivu huwa nawashangaa sana aisee.

Labda kama huishi hii tz, na kama umebahatika shuruku Mungu mkuu. Ila ufikiliavyo sivyo mkuu.
Mapambano kitaa ni makali mno ni vile vikwazo haviishi.
Na sometimes familia hubebesha mizigo mizito pia.
Futa hii mentality yako ya kijuaji(kajua yote).
 
Wakoloni walitusafirisha kwa majahazi kama watumwa kwenda kwao kuwafanyia kazi bure (manamba) kwenye mashamba, viwanda na majumbani kwao, history mbaya sana hii kukumbukwa, maana sio tu kwenda kuwafanyia kazi wazungu bure lakini wengi wao walikufa njiani wakati wakisafirishwa kwa kutoswa majini, msongamano mkubwa, njaa na ugonjwa njiani.

LEO hii sababu zilezile na manamba ndio hizihizi sa Green card lottery, Jamani hali hii ni mpaka lini? what are you looking for?

Hii ni kujitafutia balaa wewe mwenyewe na familia yako kwa matumaini feki kabisa huku ukijua kuwa utakwenda kule kufanyakazi kubwa na nyingi sana ili upate chochote kitu wakti nguvu, juhudi na akili hizo ungeweza kuziwekeza hapahapa nchini kwako na kupata mafanikio makubwa sana ya ajabu.

Si shauri uombe hiyo nyambafu
Hii nchi ina watu wajinga wajinga kama wewe wengi sana.

Punguza ujuaji.
 
Back
Top Bottom