Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Huu ni ukweli tupu, huwezi kuwa na uhuru wa kifikra kama unaishi ugenini........kama ulivyosema kwa wanawake inaweza isiwe tatizo, lakini mwanaume halisi kitu anachojitahidi sana kulinda katika maisha yake ni identity na uhuru wa kifikra.
 
kavulata said:
mimi nina akili nyingi balaa, passport yangu imejaa safari za kuja na kutoka Marekani, lakini sio kukaa na kulipa kodi huko kama zuzu, I proud of my homeland.

Akili nyingi balaa ni Passport kujaa! Nawajua watu kama nyinyi wamejana Wizarani na safari nyingi nje ya Nchi bila tija yoyote! Na kinachosikitisha zaidi hakuna chochote wanachojifunza! Katika watu waharibifu wa pesa za Umma ni kama ninyi!
Ina kera zaidi pale umeona dunia unakuja na mwazo duni kama haya! Shule umekwenda! Ila umekuwa Zuzu! Elimu za Africa hizo ziko kwenye display! Unawakilisha wasomi wengi! Sindano! Viberiti, karatasi za chooni! bado tunaagiza toka nje! Na bado tunawaita watujengee vyoo vya kunya watoto wetu! Hivi kweli kuna mategemeo watu kama ninyi wakichukua nchi!

Kweli unazidii kujiumbua. sasa wewe na Mwanakijiji aliyeko Litembo una tofauti gani!Au na mtu aliyekomea standard 7 tofauti kubwa na wewe ni ipi hasa?

Miaka 60! HAKUNA UMEME, HAKUNA MAJI na kuna jitu linajisifu Passport kujaa! Wazungu wanatucheka sana! Sasa kama kila siku unadhurura Duniani nini hasa umejifunza? Ndio kuleta uzi huu? Mbona unajiumbua mkuu!

Unasema hutaki kukaa Marekani kulipa kodi! Huna haja kabisa! Maana kuna kodi za wanyonge ambao umeshirikiana na Chama tawala kuwagawiya fulana za njano/Kijani na khanga, kuiba uchaguzi, hata dhamira na haya hunazo!

Akili balaa ni kujaza Passport! Sio kutatua tatizo la ajira au nishati! Na vijana tunaowajaribu kuwapa uthubutu wa kujaribu nje unawatisha! Najua unajua wazi wakitoka watafunguka macho! Ndio maana mna hofu na uraia wa nchi mbili!
Sijui hata kama una imani ya dini! Maana dhamira ingekuhangaisha! Akili imekufa kiasi cha kwamba akili inapimwa kwa kujaza karatasi za Passport! Na kwako mgao wa maji na umeme ni kitu cha kawaida! Hufikirii hata utambuzi! Unangoja Warsha na semina za kimataifa!

Huwa nawaona watu kama ninyi Airport! mmevaa Kaunda suti, au Suti za safari, na briefcases mikononi! Utafikiri mnakuja kufanya ya maana kumbe shopping!

Siwezi kuwa najibisha na mweye akili anayoipima kwa kujaza Passport!
 
Mimi nishapambana sana bongo lakini mpaka leo bilabila sasahivi ndoto zangu kubwa nikutoka hapa shimoni ,kila nikiangalia mbele naona giza sioni kama kutakuwa na unafuu wowote sana sana naona machafuko mbeleni baada ya watu kuchoka kubuluzwa na CCM.
 
Mimi nishapambana sana bongo lakini mpaka leo bilabila sasahivi ndoto zangu kubwa nikutoka hapa shimoni ,kila nikiangalia mbele naona giza sioni kama kutakuwa na unafuu wowote sana sana naona machafuko mbeleni baada ya watu kuchoka kubuluzwa na CCM.
Mkuu pole, unajaribu kutoa mawazo anakuja jamaa anasema ana akili kibao! LAKINI haonyeshi hata njia ya kutatua tatizo kama hilo! Amebakia kusema Manamba, manamba! kumbe ni zuzu anayezura duniani kwa pesa za wananchi! Na anajisifu kwa kujaza Passport! Ndio uwezo wake wa akili umekomea hapo!
 
Itoshe kusema ty wewe jamaa uloanzisha huu uzi ni PIMBi
Dumbi aliyeanzisha uzi huu anasema ana akili balaa! Kisa kajaza karatasi za Passport! Ndio kipimo cha akili yake! Dumbi Tanzania tulilogwa! Sijui na nani! Huyu ndio msomi nguli! Anayezunguka Duniani
 

kavulata said:
mimi nina akili nyingi balaa, passport yangu imejaa safari za kuja na kutoka Marekani, lakini sio kukaa na kulipa kodi huko kama zuzu, I proud of my homeland.

Mwenye akili balaa ni wewe uliyejaza Passport! Umetembea nje imeshindwa hata kubadili tone la akili yako! Ni ile ile ya Standard Seven!

Elimu inapimwa kwa kubuni kuondoa matatizo, wewe kipimo chako ni kujaza Passport! Mmejazana watu kama ninyi mawizarani! tunawaona ndani ya ma V8! Na Kaunda suti! kwa nje mnapendeza kumbe ndani ni kama makaburi mmejaa mifupa mitupu!

Kama kurudi nyumbani na kukutana na watu kama wewe, itakuwa ni kurudi Jehanamu! kwa kifupi haimpeleki popote nchi, ni walaji wakubwa kwa kutumia migongo ya wananchi! Lugha za siasa za Nyerere mlikuwa mnaitwa kupe!

Na kinachoumiza zaidi ni kuwakatisha tamaa Watanzania wenye nia ya kuthubu! Hofu ni kwamba tunakupunguzia watu wa kuwapanda migongoni!

Umekaa ukafikiri ukaleta mada hii, nilikuwa najiuliza sasa msukumo wako wa kuleta hii mada nini! Unaogopa hasa hiki kipindi cha Greencard itakupunguzia unawanyonya!
 
kavulata said:

mimi nina akili nyingi balaa, passport yangu imejaa safari za kuja na kutoka Marekani, lakini sio kukaa na kulipa kodi huko kama zuzu, I proud of my homeland.

Akili nyingi katika ubora wake! In full display!
 


kavulata said:
mimi nina akili nyingi balaa, passport yangu imejaa safari za kuja na kutoka Marekani, lakini sio kukaa na kulipa kodi huko kama zuzu, I proud of my homeland.

Akili nyingi ikiwa kwenye full display! Passport yake imejaa safari za Marekani! Msaidie mwenzetu!
 
Asee nimecheza Lottery ya mwaka huu.. Ikitiki ntakutafuta mkuu unipe ABCs..
 
Mleta Mada sema tuu hujui kizungu bana!! aaah! kule kutamu hakuna kutekana weweee! mara mutwe wafanyakazi hewa!! mara mbanwe na vibaka temeke mara mkose elimu nzuri!

viongozi wakubwa woote watoto wao wanasoma nje! hata rjiv gandhi, watoto wa Rais wa syria wamesomea huko wewe nani nyau kabisa usiende hukooooo! acha ujinga! umekuwa mkubwa sasa!
 
Ahsante kwa kunifurahisha
 
Huu ni ukweli tupu, huwezi kuwa na uhuru wa kifikra kama unaishi ugenini........kama ulivyosema kwa wanawake inaweza isiwe tatizo, lakini mwanaume halisi kitu anachojitahidi sana kulinda katika maisha yake ni identity na uhuru wa kifikra.
Mwanaume halisi! Huna aibu! Mnaita watu kuwachimbia choo! Hakuna maji wala umeme,mwanaume halisi haoni kuna tatizo mahali! Nchi ina miaka 60! Kuna mito na maziwa! Kila mwaka mnakimbiza mwenge uzidi kudumaza akili! Bila kujua true identity iliisha potential siku nyingi!
Na cha kusikitisha kabisa wasomi kama wewe, ambao tungetegemea mawazo mapya, mtoe hybrid ya shule mlizokwenda, na experience ya kutoka nje ya nchi, nyie ndio mnakuja na ideas ambazo zinarudisha nyuma taifa zaidi ya 1960!
Angalia msomi mwenzio, anadai ana elimu balaa, kwa sababu kajaza page za passport!
Sasa International air hostesses watasemaje! Huo ndio uwezo wa IQ yake ulipofika!
Tunajaribu kutoa tu options za wale walioshindwa kufikisha ndoto zao Tanzania, mnawatisha bila kutoa alternative! Ni roho mbaya au uchawi!
Mara unajua uzalendo! Wazalendo kina Sokoine wako wapi! Kina Magufuli wako wapi! Hata uko China kina Mao wako wapi!, kina Lumumba Congo wako wapi!
Mwisho wa siku ni wewe na maisha yako, na mipango yako!
Usiku Mwema!
 
Tulitegemea vijana kama nyie mnaochukia mngejiopenyeza kwenye siasa ili mtatue shida za umeme, maji na ajira badala ya kuwa wakimbizi ughaibuni kufanywa manamba, Bro huwezi kutajirika kwa kuajiliwa kufanya kazi za mtu mwingine. Hakuna tajiri duniani ambae amesajiliwa na mtu mwingine.
 
Akili fupi hiyo! Nani kakwambia natafuta utajiri! Kuna utajiri zaidi pesa! Kavulata, naona wewe ni mshamba mkubwa!
Safari za nje ambazo hujawahi hata kutoa senti mfukoni mwako unakuja kujianika mtandaoni!
Shame on you!
 
Mkuu toka atoke kijijini kwao na kupata ajira serikalini kapofuka macho! Hakutegemea kabisa kufika hapo, na kajaa na roho mbaya na wivu!
Tunajaribu kutoa options kwa wale ambo wanaona bongo opportunities zimebuma anakuja na blah blah zake!
Anajiona super genius kwa kujaza Passport kwa ziara za kiserikali! Ushamba mkubwa!
 
Maisha niliyokuwa Tanzania kabla sijaja US sidhani hata sasa umeyafikia! Na si kwa Per Diem za serikali!
Wigo wako wa maisha duni sana! Ni reflection ya background yako!
 
huyo jamaa anaesaidia kuwajazia hiyo green card mwenyewe muonekano hashawishi kama kuna life huko la kueleweka.
Ni porojo tu,kusubiria hela za viewers youtube.
Mtu serious huko US unapataje muda kuja hamasisha watu kuomba green card?
kuna asiyejua hiyo green card toka enzi na enzi ipo.
mwenyewe anakiri we mpaka ufike huko na kusettle na family andaa dola 10,000!
mtu ana dola 10000 kweli atawaza kuhama aende huko kuanza upya badala ya kujiendeleza hapo alipo.
Sijamwelewa huyu jamaa
 
Akili fupi hiyo! Nani kakwambia natafuta utajiri! Kuna utajiri zaidi pesa! Kavulata, naona wewe ni mshamba mkubwa!
Safari za nje ambazo hujawahi hata kutoa senti mfukoni mwako unakuja kujianika mtandaoni!
Shame on you!
Akili ndefu ni kuwa mkimbizi na kulikana taifa lako na uraia wako? shame. Ikitokea xenophobia unatetemeka na kutafuta pa kujificha. PATA SEMA lakini Mimi ni maskini jeuri, sijuti kuwa mtanzania Wala kuishi Tanzania.
 
Hata tofauti na akina tiptip waliokuwa wanatafuta watumwa/manamba wa kusafisha wanakohitajika, tofauti Yao ni kwamba Tiptip alitumia nguvu ya bunduki lakini hawa wanaotumia nguvu ya kushawishi na kuhadaa vijana kuwa Kuna kazi kibao huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…