kavulata said:
mimi nina akili nyingi balaa, passport yangu imejaa safari za kuja na kutoka Marekani, lakini sio kukaa na kulipa kodi huko kama zuzu, I proud of my homeland.
Akili nyingi balaa ni Passport kujaa! Nawajua watu kama nyinyi wamejana Wizarani na safari nyingi nje ya Nchi bila tija yoyote! Na kinachosikitisha zaidi hakuna chochote wanachojifunza! Katika watu waharibifu wa pesa za Umma ni kama ninyi!
Ina kera zaidi pale umeona dunia unakuja na mwazo duni kama haya! Shule umekwenda! Ila umekuwa Zuzu! Elimu za Africa hizo ziko kwenye display! Unawakilisha wasomi wengi! Sindano! Viberiti, karatasi za chooni! bado tunaagiza toka nje! Na bado tunawaita watujengee vyoo vya kunya watoto wetu! Hivi kweli kuna mategemeo watu kama ninyi wakichukua nchi!
Kweli unazidii kujiumbua. sasa wewe na Mwanakijiji aliyeko Litembo una tofauti gani!Au na mtu aliyekomea standard 7 tofauti kubwa na wewe ni ipi hasa?
Miaka 60! HAKUNA UMEME, HAKUNA MAJI na kuna jitu linajisifu Passport kujaa! Wazungu wanatucheka sana! Sasa kama kila siku unadhurura Duniani nini hasa umejifunza? Ndio kuleta uzi huu? Mbona unajiumbua mkuu!
Unasema hutaki kukaa Marekani kulipa kodi! Huna haja kabisa! Maana kuna kodi za wanyonge ambao umeshirikiana na Chama tawala kuwagawiya fulana za njano/Kijani na khanga, kuiba uchaguzi, hata dhamira na haya hunazo!
Akili balaa ni kujaza Passport! Sio kutatua tatizo la ajira au nishati! Na vijana tunaowajaribu kuwapa uthubutu wa kujaribu nje unawatisha! Najua unajua wazi wakitoka watafunguka macho! Ndio maana mna hofu na uraia wa nchi mbili!
Sijui hata kama una imani ya dini! Maana dhamira ingekuhangaisha! Akili imekufa kiasi cha kwamba akili inapimwa kwa kujaza karatasi za Passport! Na kwako mgao wa maji na umeme ni kitu cha kawaida! Hufikirii hata utambuzi! Unangoja Warsha na semina za kimataifa!
Huwa nawaona watu kama ninyi Airport! mmevaa Kaunda suti, au Suti za safari, na briefcases mikononi! Utafikiri mnakuja kufanya ya maana kumbe shopping!
Siwezi kuwa najibisha na mweye akili anayoipima kwa kujaza Passport!