Mkuu hawa watu wapo tayari kubaguliwa na kusimangwa bila kujali lolote kisa maisha bora, whites wanamwona mtu mweusi kama mtu duni, mwenye kubeba magonjwa, asiye muungwana wala mstaarabu, hata kama hawatakuonyesha kwa nje, ule ubaguzi upo kwa ndani. Wakati nilipokuwa huko masomoni nilihakikisha naishi eneo karibu na chuo ili niwe natembea kwa miguu nisipande mabasi yao, maana kwa ule ubaguzi ni kawaida kupitwa kwenye kituo sababu upo mweusi peke yako, au kususiwa siti ili usikaribiane na mzungu kwenye zile siti mbilimbili......kunga'ng'ania maisha bora katika mazingira ya kubaguliwa na kusimangwa wakati hujafukuzwa kwenu sioni kama ni akili, zaidi ya kuonekana kama ni utumwa wa kifikra zaidi.