Kavulata,
Najua mimi na wewe tulikubaliana kutokubaliana katika mada hiii.....lakini mkuu statistics hazidanganyi.....Unajua mwaka uliopita Walioomba Green Card walikuwa wangapi? Hasa kutoka Africa na nchi nyingine za Ulimwengu! Tanzania tu idadi ya wanaoomba Greencard kuja Marekani inaongezeka kila kukicha! Na maendeleo yote yanayozungumzwa nchi za kiafrica.....
Msimamo wangu uko wazi, maisha ni popote pale ambapo panaweza kupata unachokitaka! Na maisha ni mafupi mno! mno! Kuna jamaa namfahamu Ni Engineer na ana kazi nzuri mno Tanzania, na kwa wadhifa wake katembea nchi nyingi ulimwenguni, lakini amepata Green Card yuko US, alipoulizwa kwa nini anataka kuja Marekani alisema, sio pesa tu wala kutoboa, maana Tanzania kisha toboa! anataka "American experience" na anataka mtoto wake apate elimu hapa! Kaja na pesa zake, na yuko kwenye process ya kununua nyumba! Sasa utasemaje!
Mkuu huwezi kuzuia utashi wa mtu kutafuta anachokitaka. Mimi natofautiana na wewe, kwa vile wewe umeingiza chuki binafsi na Marekani badala ya kuwa rational! Mji naokaa US Waarabu na watu kutoka India wameongezeka sana kununua nyumba, na unajua wazi mila na desturi zao ni tofauti na watu wa Marekani in general! Lakini watu hawa kuna kikubwa wanachokitafuta ambacho hakipatikani huko wanakotoka! Marekani sio Paradiso Kavulata! Lakini ukiwa na vibali halali tu ya kuwa hapa, na ukiijua system ya hapa inavyofanya kazi, kwangu mimi ni mahali pazuri kwa kuishi na kukusadia kutimiza kile ambcho unatafuta!
Naomba usisahau msimamo wangu, ambao haubadiliki, kama unaona mambo yako Tanzania hayaendi, si mbaya kujaribu nje ya Tanzania.....kwa upande wangu jaribu Marekani ukiwa na vibali halali vya kuwa US.