Ni sawa kujichagulia kutokana na mipango na pengine background yako, lakini kusema nyumbani kwenu hakustahili kuishi mtu ni kuvuka mipaka. Hatuwezi kuipiga mnada Tz na watu wote tukahamia nchi za waliokuwa na umeme wa uhakika. Nilikuwa na jamaa yangu hivi majuzi tu alikuwa akijisifu kuwa watoto wake wako Marekani, lakini alikuja ikafikia hatua anatuhitaji sisi na watoto wetu ambao tuko tanzania tumsaidie kumuuguza, kumgeuza na kumvalisha. Hata alipokufa watoto wake jamii iliwaona sio kitu kwakuwa hawakuwepo around jamii inawahitaji. Hela sio kila kitu bro, haiwezi kununua kila kitu binadamu anachokihitaji all the time everyday.
kama umepata nafuu sawa lakini usiwape hope iliyopitiliza kuwa huko hakuna tatizo mambo yote ni tambarare kwa lengo la kuvutia vijana wapande boti wafie majini. Mimi nimeishi huko miaka 15 kwa kushawishiwa lakini nikaona sio sawa, na kila mke wangu akipata ujauzito nilikuwa namwambia nenda kajifungulie nyumbani ili watoto wetu wawe watanzania, fahari yao kama watanzania, maana hata Nabii Yusufu alikwenda Misri ambako alifanyakazi za kitumwa hadi akafanikiwa lakini hakuwahi hata siku moja kukashifu nchi yake na watu wake na hakuwa kuchukua uraia wa Misri. Lakini wewe ni mtu wa ajabu kidogo na kaulimbukeni kidogo.