Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Mkuu najua sana ninachoongea......wewe una mtazamo wa maisha bora ugenini, everything coming from that ni utumwa na ukimbizi maana umeacha nchi yako na jamii yako nyuma ukikimbia matatizo.
Tatiana matatizo basi! Kwa mawazo hayo sijui utatua nini, rather than moving the nation into backwardness
 
Kufanya kazi halali ni kuadhirika?
Ukikaa hapa bongo huna kazi itakusaidia nini? Unashangaa watu kufanya kazi zaidi ya moja, wewe itakuwa ni mvivu.
Acha watu wapambane.
"ukikaa hapa bongo huna kazi itakusaidia nini" hivi ni kweli hapa bongo hakuna kazi? kuwaza namna huu ni msiba mkubwa kwa vijana wetu kama ilivyo misiba mingine. Hivi hata bongo ukifanya kazi zaidi ya 2 kama wanavyofanya huko mliko hutoki kimaisha? Siku moja nilikuwa kule Durban beach, nikakuta vijana wa bongo kwenye gazebo moja wanavyoa watu, nikawatazamaaaaaaaa, hadi nikajisikia kizunguzungu. Hivi kweli kutoka bongo kuja hadi SA kuwa kinyozi kweli?
 
Mkuu najua sana ninachoongea......wewe una mtazamo wa maisha bora ugenini, everything coming from that ni utumwa na ukimbizi maana umeacha nchi yako na jamii yako nyuma ukikimbia matatizo.
Ila mimi sijui ninachoongea! Nadhani hujanielewa kabisa!
 
Mkuu najua sana ninachoongea......wewe una mtazamo wa maisha bora ugenini, everything coming from that ni utumwa na ukimbizi maana umeacha nchi yako na jamii yako nyuma ukikimbia matatizo.
Hayo matatizo jiandae kuyatatua mpaka utakapo ingia kaburini! Miaka 60 tuna deal na tatizo moja tu: UJINGA! Ndio nao uona kwa wasomi kama wewe! Mwenzio anasema ni critical thinker ukimpa facts, anasema unadharau ulikotoka! Miaka 60 bado tunashindana na ujinga! Tena sasa ni kwa wasomi! Iko kazi!
 
Nakuuliza tu na wewe unakimbiza mbio za Mwenge? Mwanga wa utambi na mafuta ya taa unaamini inaweza kuleta mshikamano? Huu sio utumwa wa akili? Ambao ni mbaya zaidi kuliko utumwa wowote!
wewe kaka huna akili kabisa, sasa nimeanza kuelewa. Kila taifa lina utamaduni wake unaokuwa kama alama yao hata kama kwa wengine unaonekana kama kichekesho na ujinga. Mfano, hapo Marekani wana kile kitu chao wanakiita Halloween, mimi kwangu nilikuwa nawaona kama wapuuzi vile kwakuwa sisi kwetu kula maboga sio kitu cha maana. Mazishi ya malkia Elizabeth kule UK ulimuona beberu mweuzi kwenye parade. sasa unachoshangaa mbio zetu za mwenge na kuona kula maboga na beberu ni sawa ni nini? Kijana toka huko uliko, labda uniambie kuwa na wewe umekumbwa na utamaduni wa ushoga huko.
 
Halloween ni sikuukuu ya Kitaifa, ni hata public holiday? Kwa Mwenge ni utamaduni wetu, tokea wapi! Safari bado ndefu!
 
Hayo matatizo jiandae kuyatatua mpaka utakapo ingia kaburini! Miaka 60 tuna deal na tatizo moja tu: UJINGA! Ndio nao uona kwa wasomi kama wewe! Mwenzio anasema ni critical thinker ukimpa facts, anasema unadharau ulikotoka! Miaka 60 bado tunashindana na ujinga! Tena sasa ni kwa wasomi! Iko kazi!
Mkuu sipingani na wewe, kutafuta maisha ugenini bado ni option nzuri......watu wengi wanaoishi na kufanya kazi katika mataifa yaliyoendelea siyo wenyeji asili wa mataifa hayo, wale wenye fursa hiyo wanaweza kwenda kujaribu, siyo jambo baya, ila ndo hivyo kukumbuka jamii ulikotoka kwa hali na mali panapo mafanikio.....​
 
Halloween ni sikuukuu ya Kitaifa, ni hata public holiday? Kwa Mwenge ni utamaduni wetu, tokea wapi! Safari bado ndefu!
Utamaduni wa mwenge umeanzia kwa wazungu wenyewe, kumbuka kuna mwenge wa malkia wa mashindano ya olympiki. Ni utamaduni wa kipagani ulioanzia kwenye jamii za kale sana....
 
Nyumisi: Nilidhani umeelimika!bado thinking yako iko twisted, unaposema cheap labour sijui una maana ipi! Hivyo mtu aliyekuja soma US, sio kutoka Tanzania tu au nchi yoyote kama professional,yeye analipwa kidogo sawasawa na mzawa!
Nauliza unajua unachokisema? Nilimtembelea recently Mtanzania ambaye alikuwa BOT akaja kusoma huku, baada ya kuwa na experience amewekwa kuwa mkuu wa kitengo fulani katika IT company, mshahara alioutaka yeye baada ya kuangalia wenzake wanalipwa nini IBM,dau alilotaka walimpa,siwezi kuweka hapa maana hatuaamini!
Sasa narudi kwenye mfano binafsi, my son ni IT person, alipokuwa semester ya mwisho yeye na wenzake wawili walikuwa approached na Institution fulani, waliopoajiriwa, yeye Mtanzania, mmoja kutoka Nepal na kijana mzungu wa hapa wote walianza na scale moja! Maana shirika liliwaonyesha entry level package.
Sasa sijui habari hizi mnaokoteza wapi?
Anyway, let say nikubali argument yako, nimetoka Tanzania nakuja kusoma US, mshahara wangu Tanzania ni $ 1500/ Baada ya ku graduate, shirika la US likaona nafaa, na kunilipa mara tano ya Tanzania, na position hiyo hiyo yuko mzawa analipwa more than me, kwa hiyo unashauri nirudi nyumbani kuchukua $1500/ yangu sababu ya uzalendo! Uzalendo upi hasa!
Hivi huo uzalendo mnaouzungumza hapa mbona hatuuoni ukifanya kazi na kubadili nchi?
Mnaishia kulalamika juu ya tozo, ukosefu wa maji, umeme, mbona huo uzalendo uliowakimbiza ulaya umeshindwa kubadili nchi!
Hebu acheni porojo!
Jambo jingine ni kwamba wazungu wanafanya brain drainage kutoka mataifa mengine kwa wale vijana wenye utaalamu hasa ambao wanaona kuna uhaba, wako very strategic...
 
Ni sawa kujichagulia kutokana na mipango na pengine background yako, lakini kusema nyumbani kwenu hakustahili kuishi mtu ni kuvuka mipaka. Hatuwezi kuipiga mnada Tz na watu wote tukahamia nchi za waliokuwa na umeme wa uhakika. Nilikuwa na jamaa yangu hivi majuzi tu alikuwa akijisifu kuwa watoto wake wako Marekani, lakini alikuja ikafikia hatua anatuhitaji sisi na watoto wetu ambao tuko tanzania tumsaidie kumuuguza, kumgeuza na kumvalisha. Hata alipokufa watoto wake jamii iliwaona sio kitu kwakuwa hawakuwepo around jamii inawahitaji. Hela sio kila kitu bro, haiwezi kununua kila kitu binadamu anachokihitaji all the time everyday.

kama umepata nafuu sawa lakini usiwape hope iliyopitiliza kuwa huko hakuna tatizo mambo yote ni tambarare kwa lengo la kuvutia vijana wapande boti wafie majini. Mimi nimeishi huko miaka 15 kwa kushawishiwa lakini nikaona sio sawa, na kila mke wangu akipata ujauzito nilikuwa namwambia nenda kajifungulie nyumbani ili watoto wetu wawe watanzania, fahari yao kama watanzania, maana hata Nabii Yusufu alikwenda Misri ambako alifanyakazi za kitumwa hadi akafanikiwa lakini hakuwahi hata siku moja kukashifu nchi yake na watu wake na hakuwa kuchukua uraia wa Misri. Lakini wewe ni mtu wa ajabu kidogo na kaulimbukeni kidogo.
Huku Tz tunawaacha watu wenye akili mgando kama ww.
 
Utamaduni wa mwenge umeanzia kwa wazungu wenyewe, kumbuka kuna mwenge wa malkia wa mashindano ya olympiki. Ni utamaduni wa kipagani ulioanzia kwenye jamii za kale sana....
Jamaa anaona mwenge wa olympic, beberu na sikukuu ya kula maboga ni ustaarabu kwakuwa unafanywa na wazungu, kazi ipo. Hapendi bongo kwakuwa hakuna umeme!! cheap reasoning.
 
Jambo jingine ni kwamba wazungu wanafanya brain drainage kutoka mataifa mengine kwa wale vijana wenye utaalamu hasa ambao wanaona kuna uhaba, wako very strategic...
Kwa nini na ninyi msifanye brain drainage! Maana unajua tunahitaji technology! Umejua siri yao, tuna miaka 60 toka tupate uhuru! Tumeshindwa nini kufanya hivyo! Sana sana brain drainage ni kuchimbiwa vyoo vya shimo! Is just pathetic! Kuwa strategic mkaona ni kuomba vyandalua vya mbu!
Hao ni wataalam kama wewe waliojazana wizarani!
 
Huku Tz tunawaacha watu wenye akili mgando kama ww.
mimi nina akili nyingi balaa, passport yangu imejaa safari za kuja na kutoka Marekani, lakini sio kukaa na kulipa kodi huko kama zuzu, I proud of my homeland. Na wapo wengi tunaofanya hivyo, kuingia na kutoka, kuchuma ugenini na kwenda kulia nyumbani na watu wa kwetu huku tukifurahia kuujenga uchumi wa kwetu kwa kunywa bia yetu ya safari larger kwa pesa kutoka huko.

Siku moja nilimuita rafiki yangu mzungu kutoka huko aje anitembelee kwetu. Unajua nini alifanya? alibeba hata maji ya kunywa, juice, chocolate, biscuits, candy (cookies), perineal pads, apples, na wine kwa kujua kwamba huku bongo hakuna kitu kabisaa na ni maskini kupitiliza na njaa plus plus hivyo asijekuja kuteseka, Alipofika airport akashituka kuona kila kitu alichokibeba anakikuta kwenye maduka ya airport, siku ya pili nikaenda nae mitaa ya posta, kariakoo na Mlimani city mall, akashangaa kwelikweli kuona vitu teleee na maduka makubwa kama ya Kroger na Walmart yaliyojaa bidhaa safi na fresh kabisa na vinywaji vya moto na bites kama hot dogs na pizza. Akakuta watu wanakunywa na kufurahia kwa pamoja huku wakiangalia mpira kwenye open spaces bila kudaiwa tips na wahudumu, alishangaa na kushangaa na kuniuliza kwanini mna furaha hivi kuliko sisi ingawa mnasema nyie ni nchi maskini? mbona mna kila kitu? mbona mnakunywa na kula pamoja kama watu mnaojuana? Alivyorudi kwenye apartment alipofikia akavitupa baadhi ya vitu alivyokuja kama majuice akaanza kununua vitu fresh kama matunda ambayo hayakuwekewa mbolea hata moja, na ulikuwa msimu wa maembe dodo na mapapai kutoka vijijini ambayo ni matamu kuliko maembe na mapapai ya marekani.

Ussidharau kwenu na chenu hata kidogo.
 
Jamii anaona mwenye wa olympic, beberu na sikukuu ya kula maboga ni ustaarabu kwakuwa unafanywa na wazungu, kazi ipo. Hapendi bongo kwakuwa hakuna umeme!! cheap reasoning.
Kwa sababu nyumba yako ina kunguni, basi suluhisho ni kuhamia kwa jirani......jirani akikuwekea masharti ya kukudhalilisha utamlalamikia nani? wakipita na maandamano yao yale ya mashoga basi na wewe kama zuzu unaenda kuungana nao usije kuonekana unaenda kinyume na mila zao wakakufungasha virago, ukimwambia mtu huo ni utumwa anafikiri unamwonea wivu.​
 
Safari za kuja Marekani ndio akili!
Hakuna mtu mwenye akili anaependa kuwa mkimbizi (refugee), labda kidoogo mwanamke ambae anaweza kuolewa na kuishi kokote. Lakini mwanaume (hazina ya ukoo) kuwa mkimbizi ni msiba mzito sana na laana kwa ukoo husika na hata taifa. Hata Nabii Yusuf alirudi kwao pamoja kuwa aliuzwa utumwani. Nawashangaa hawa watu wetu weusi waliokuwa wameuzwa utumwani kukataa kurudi kwao hata baada ya kufahamu asili yao ilikuwa wapi, shame upon them.
 
Back
Top Bottom