kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #321
Mimi sina position yoyote, ni lumpen kama walivyo wengine, ninachotofautiana na wewe ni picha unayoichora kuhusu Marekani watanzania waione Marekani kupitia picha yako hiyo na picha unayoichora Tanzania ili Marekani waione Tanzania kupitia picha yako hiyo ofu.Kavulata, naona sasa unaingiza harufu za Ukabila! Umeshindwa kabisa kuuza hoja zako, nadhani kila mtu anayesoma hoja zako, anaona zinasukumwa na chuki binafsi tu! Hatujaona kabisa uzalendo wako, sana sana umeonyesha ulimbukeni, na ushamba, sina haja ya kuzirudia nukuu zako tena, maana zinaleta ukakasi mno kuhusu elimu yako! Na hata huko kutembea kwako kumeshindwa kabisa kukusaidia kufikiri!
Na inasikitisha mno watu kama ninyi ndio mmejaa wizarani! Anyway kwa kukusaidia tu, mimi sijatoka Kanda ya Kaskazini! Ukoo wangu ni mchanganyiko hasa, a truly Tanzanian, nimechanganya makabila mpaka dini! (Ukristo na Uislamu) Na ndugu pande zote. Hii imenisadia kumwangalia mtu kama kama mtu, bila kujali kabila, lake, dini yake, na taifa lake, nilifunzwa ubaya wa "stereotyping mapema mno maishani, hivyo iliniezesha kufanya kazi Mashirika ya Kimataifa hata kabla ya kuamua kuishi Marekani, na kunikutanisha na watanzania ambao kwa miaka mingi wamekua wakifanya kazi nje ya nchi ya Tanzania katika mashirika kama Africare UNDP, FAO, UNICEF,DFID nk katika nafasi kubwa, na ilikuwa ikituumiza sana kuona idadi ya Watanzania ni ndogo mno, ukilinganisha na wenzetu kutoka Kenya, Ghana, Nigeria, Uganda, na kila mara tunapokutana ilikuwa tunafikia, tufanyeje kuwafanya Watanzania wajaribu kutafuta kazi za kimataifa, kwa faida zao binafsi na hata mbeleni kwa faida ya Tanzania. Maana wenzetu wa mataifa mengine walikuwa wakiletana na wanasaidiana.
Nimekuja Marekani nikiwa na Financial Freedom kubwa ambayo labda kwa sasa wewe unajaribu kufikia kwa Per Diem za serikalini! Nimekulia, Upanga, Oysterbay, Masaki! Hiyo ndiyo Dar es Salaam yangu, kwa mbeleko ya wazazi wangu ambao walikuwa na broader perspective ya maisha, urithi mkubwa walioniachia, ambao najivunia! na mimi pia kuishia kutengeneza makazi yangu na biashara zangu sehemu hizo hizo Dar es Saam.
Nikiwa na miaka ya 30 to 35 tayari nilikuwa nime achieve vitu vingi ambavyo mamilioni ya Watanzania watakwenda kaburini hawata weza kupata, maana najua maisha ya vijijini kwa undani! Vijiji ambavyo bado wengi wanaona gari inapoleta mitihani ya darasa la saba, au padri anapokuja kusalisha misa baada ya ya muda mrefu, au wanapoletewa Masanduku ya kupiga kura kila baada mika mitano mitano, na wakati mwingine mbio za mwenge. Watu hao kamwe kama hakuna nguvu au neema ya Mwenyezi Mungu ni vigumu kutoka hapo walipo, Sijaona utashi wowote wa kisiasa kuwaondoa watu hao katika uduni huo wa maisha.
Hayo ndio maisha yangu! Nilifikia hali hiyo si kwa vile ni genius! Ni mipango ya mwezi Mungu tu, ambaye anakuleta duniani bila kuchagua mzazi, wala mahali pa kuzaliwa ! Na ambaye pia anajua lini na wapi nitavuta pumzi yangu ya mwisho! Ni muumini naye amini uwepo wa Mungu, hasa katika mafunzo ya Predestination! "My destiny is in the hand of God"
Mtazamo wangu wa maisha ni kuwa, baraka za Mungu na mafanikio ambayo amekupa bure jaribu kama unaweza kuwasaidia wenzako ambao unapishana nao ulimwenguni kwa muda mfupi, kimawazo na kihali, na huo ndio umekuwa msimamo wangu, kwa wale ambao wanaona Tanzania ni ngumu, au milango imefungwa, kwa kuwaambia si mbaya kujaribu nje ya nchi! Kama mimi nimeweza, kwa nini wengine wasiweze! Hivyo si mrubuni wala kumshawishi mtu! Sipati faida yoyote kwa kufanya hivyo, ni kusaidia tu watu kufikisha ndoto zao!
Hivyo tukubali kutokubaliana, wewe umewekwa kwa sasa kwenye position hiyo ya kuwasadia Watanzania, fanya unaloweza kufanya.Nami nitafanya naloweza kufanya nikiwa na nia safi na dhamira njema.
Naamini wako watakao soma posts zako na zangu pia, kwa msemo wa Mhe mstaafu Rais Kikwete, akili za kuambiwa changanya na kwako watafanyia kazi.
Siku Njema, Maisha mema!.
Unachora picha kwamba Marekani maisha ni rahisi, hakuna asiyekuwa na kazi, hakuna ombaomba, hakuna maskini, hakuna anayeshindwa kuishi, hakuna uhalifu. Kisha unachora picha ya Tanzania isiyokuwa na jema hata moja, hakuna umeme, maji, chakula, shule Wala oxygen, hivyo hakufai kuishi. Huu ndio ugomvi wangu na wewe, basi. Waambie vijana ukweli, both sides of the coin ili wawe na informed choice badala ya kuwapa matumaini bandia.