Ng'wanamangilingili
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 5,778
- 4,859
Umemjibu kitaalamu zaidi huyo poyoyoKavulata:
Kitu ambacho Kavulata hakifahamu, hata vigezo vya kupima umaskini vinatofautiana kati ya Mataifa yaliyo mbele katika maendeleo ya viwanda na nchi maskini: ( Indicators and Monitoring Framework)
Ukitumia vigezo hivi Marekani, watu wote ni matajiri! Lakini maana hakuna mgao wa maji, maji ni safi (Mamlaka za maji zinapoleta maji yenye athari yoyote ile ni kosa kubwa sana) Hakuna ukosefu wa Umeme, kuwa Tv, gari ni kitu cha kwaida kabisa, Hivyo vigezo vinayotumika kupima umaskini Marekani ni tofauti kabisa!
- Adult or child malnourishment
- Disrupted or curtailed schooling (a minimum of years 1-8)
- The absence of any household member who has completed 6 years of schooling
- Child mortality within the household within the last 5 years
- Lack of access to safe drinking water
- Lack of access to basic sanitation services
- Lack of access to clean cooking fuel
- Lack of basic modern assets (radio, TV, telephone, computer, bike, motorbike, etc.)
- Lack of access to reliable electricity
Kwa kifupi nitakupotezea muda tu nikikuletea charts za Umaskini wa Marekani! Au mtu wa kipato cha chini Marekani kisheria, nachukulia anayefanya kazi kama waiters ( inategemea naye anafanyia wapi)au waafanyakazi wa kawaida viwandani, gas stations etc, wasio na skills kabisa. Ukiwachukua watu hao hao ukiwalinganisha na mtu wa kazi hizo Tanzania utaona kitu tofauti kabisa!
Kwenye interview ya kazi ya kawaida( au ya chini) kama hapa Texas swali muhimu unaloulizwa, je una reliable transport! Ukiwa na maana una gari? Maana yake wanataka kujua attendance yako itakua ni reliable. Kwa Tanzania mtu wa chini, anayeuza mafuta Petrol stations, au mhudumu hotelini huwezi kumuuliza swali hilo!
Leo hii ukija Marekani kama miji ya Houston, Dallas, San Antonio, na mingineyo, kitu cha kwanza ni kujifunza ni kuendesha gari, au kumiliki gari! Gari sio luxury ni necessity! Tofauti kabisa na Tanzania, hapo ndio utajua mtu akikuambia Maskini wa Marekani na Tanzania!
Naona ukija Marekani na kukutana na omba omba basi una piga kelele kuna Maskini! Na Marekani pia kuna maskini! Hilo jambo huwezi kuzuia, ni matakwa ya mtu binafsi, maana huwezi kumzuia mtu kulewa, au kutumia madawa ya kulevya, kuwa malaya, kwa ukijinga wako ukashindwa kulipa kodio ya nyumba!
Umepewa nyumba karibu na bure na serikali ya kuishi kwa kuwa na kipato duni, wewe ukageuza danguro au kuuzia madawa ya kulevya! Ukifukuzwa lazima utakua omba omba! Lazima utaishi chini ya madaraja! Asiliamia kubwa ya hao omba omba wamefika hapo kwa uchaguzi mbaya dhidi ya maisha yao! Ni vigumu kabisa kwa mimi na wewe tuliotoka Tanzania kuja kutafuta hapa kuingia katika ujinga huo! Nimesikia kuna Mtanzania mmoja alijiingiza kwenye madawa ya kulevya akaishia hapo! Hayo ni maamuzi ya mtu binafsi!
Kavulata:
Labda nikusaidie list ya Vitabu vikufungue macho: ( Viko vingi mno) Na vingine vingi vimeaandikwa na waafrica wenyewe.
1. The Wealth and Poverty of Africa States: Morten Jerven
2.Poverty and Wellbeing in East Africa- A multifaced Economic Approach
3.Inside Poverty and Development in Africa-Africa Dynamics
Lakini kama unataka kutengeneza hoja ya umaskini USA basi soma kitabu hiki;
1. Poorly Understood: What Americans get wrong on Poverty ( Several authors) Kitakupa angalau hoja ya kulinganisha maskini wa USA na hao wa nchi kama Tanzania, itabidi uangalie vigezo tofauti kabisa!
Panua wigo wako wa kuangalia mambo!
Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app