kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #401
Zamani zile wafanyakazi kutoka Afrika kwenda kufanyakazi za wazungu walikuwa wanapatikana kwenye masoko ya Watumwa, hapa kwetu masoko ya watumwa yalikuwa pale Bagamoyo na Zanzibar. bahati mbaya watumwa kutoka masoko ya bagamoyo na Zanzibar hawakupelekwa wengi Marekani bali walipelekwa Ulaya na Uarabuni na hii ilitokana na kuwa masoko ya bagamoyo na Zanzibar hayakuwa na watumwa wenye maumbo makubwa na nguvu nyingi kuweza kumudu soko la marekani Kusini na kaskazini. Hivyo, watumwa wengi waliopelekwa masoko ya Amerika walitoka Afrika magharibi hasa nchi za Senegal, Ghana, Mali na Bukina Faso ambako yalipatika watu wenye mili mikubwa na nguvu nyingi (gar people) waliopelekwa huko Caribbean na Amerika kwenye mashamba na viwanda. Kumbuka kuwa Wakoloni shida yao kubwa ilikuwa kupata nguvukazi ya bei nafuu (manamba na watumwa), kupata malighafi na masoko ya bidhaa zao. Ukoloni na utumwa vinaonekana kuwa vimekwiaha lakini Shida hizi 3 za wafanyakazi wa bei nafuu, malighafi na masoko bado wanazo mpaka leo.Huyo jamaa ni fala ,wala usijibizane naye
Baada ya ukoloni na utumwa kwisha na masoko/minada ya watumwa kufungwa ndio wakabuni njia nginine za kupata watumwa (wafanyakazi wa bei nafuu), malighafi na masoko ya bidhaa zao. Njia wanazotumia kupata wafanyakazi wa bei nafuu ni mbili kuu ambazo ni kuhamishia viwanda/shughuli zao kutoka marekani na Ulaya kwenda nchi maskini kwa jina la uwekezaji na kuajili wazawa kwa ujira mdogo sana, na pili kutoa vivutio(chambo) kama Greencards na scholarships za masomo ili kupata cheap labor kwa kazi ambazo ziko kwenye mataifa yao ambazo hazihamishiki. Hapa kwenye greencards ndipo panapowachanganya mazuzu wetu, wanasahau kuwa greencard ni mbadala wa soko la watumwa la bagamoyo na Zanzibar kwa jina lingine.
Siku moja nilitembelea pale Zanzibar kuona ofisi moja ambayo watu wanasajili vijana wa kike na kiume kwenda kufanyakazi Uarabuni, roho yangu iliniuma sana tena sana kuona watu wanafanyakazi zilezile kama za soko la watumwa. Wanatumia ujanjaujanja kuwapata watu kwenda uarabuni eti kuna kazi nyingi sana huko. Vijana wamejaa kwenye ofisi ile wakisubiri kusajiriwa wengine kwa vyeti vya utambulisho bandia.
Mpaka karne hii yuko mtu anashangilia kama zuzu kupata greencard ili akawe kijakazi na kutumikia taifa lingine. Yaani anaacha ardhi, mashamba na vyakula fresh kwenda ugenini akaishi kama mkimbizi maisha ya dhiki, hofu na wasiwasi kubwa. Yaani anapishana na wazungu kwenye ndege wakija kwao kukamata mapande makubwa ya ardhi yao na yeye kwenda kwao akawe kibarua wao akahudumie wazee, watoto na watu wao na kula vitu vikuukuu kama hot dog (fast foods) na kununua vitu vya kwenye clearance.
Hapa sio maswala ya wivu bali ni maswala ya ukombozi wa kifikra wa vijana wetu. Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kumshangalia kijana wetu aliyekwenda kule na kurudi kwao na mtaji, elimu, uzoefu, ujuzi na exposure kuja kubadilisha mambo (uchumi, huduma, siasa na matazamo) kwao.