Hata hapa Tz kazi zipo telee, tatizo ni kwamba huku ushoga haulipi kama huko, huko mwanaume unaweza kuolewa ukaishi vizuri tu, huku watu wana mapesa na wanunua kila kitu kwa cash, ndio maana unaona magari yapo barabarani, maduka yapo, watu wanajenga, watu wanasomesha, watu wanajenga shule binafsi, vyuo binafsi, nk. Tatizo sisi majeshi yetu ni ya ukombozi tu na kulinda mipaka, wakati huko majeshi yao ni ya kujenga uchumi, uporaji na wizi kwenye mataifa mengine na kupeleka kwao. KInachosaidia watu manamba kama nyinyi ni vitu vifuatavyo:
1. Ratiba ngumu (tight) za siku, wiki, mwezi na mwaka (kujilipua), huku watu hawako serious na matumizi ya muda wao (time management)
2. Kubana matumizi kwa kununua vitu vikuuvikuu au vilivyopitwa na wakati/msimu/fashion - mitumba/fast foods/clearance. Huku 95% wanapika wenyewe vyakula fresh, matunda fresh na nyama fresh, sio canned foods.
3. Kuwa mbali na extended families, ni wewe tu peke yako basi, lakini huku kuna ndugu wengi sana watakuhitaji uwasaidie na kutunza wazee wako waliozeeka.
4. kukopa.
5. wabongo Hamchagui kazi mkifika huko, huku kazi zipo lakini watu wanachagua .
Hata hapa bongo kama utaishi maisha kama hayo lazima utakuwa na financial freedom wakati huohuo ukiendelea kulijeng taifa lako kwa kodi, tozo na huduma. Furaha sio kuwa na pesa tu bhana wewe.