kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #701
Sure, sure!! Cross ya goli ilitoka kule kwa mababu zetu kukubali kutawaliwa. Lakini hiyo pekee sio sababu ya sisi wajukuu tuinue mikono yetu juu ya kushindwa kujipapatua na ku correct mistake zao. Unaweza kuzaliwa masikini na kufa tajiri sana kama wanavyofanya wenzetu waliotawaliwa pia kule China, India, Pakistan, Indonesia, Malaysia, nk.Kavulata:
Hivi Prof Lumumba kamsaidia nani hasa.....Ukienda Kenya ndio wanaongoza kuomba Greencard....Kenya ina watu wa kila kada Marekani, Wasomi na watu wa kawaida.....Kadri anavyotoa mihadhara ndio waombaji Greencard wanazidi....Na unajua Kenya ndio inaongoza kupeleka wafanyakazi Uarabuni......Katika mahangaiko yangu nje ya Tanzania, ukiondoa Wanigeria, kenya inaongoza kuwa na wahangaikaji wengi mno nje ya nchi.
Haya maneno ya Lumumba awapigie kelele wale walioko African Union......Huwa nakukumbusha tena na tena Babu yako na babu yangu waliposhindwa kumzuia mtu mweupe asiweke nanga kwenye pwani zetu walituingiza mkenge mkubwa mno...! Mpaka leo hatujitambua......tutabadili mabwana tu.....! Kama sio beberu wa Kimarekani....basi Mrusi au mchina......Mwarabu nk.....! Hatuna akili za kujiendesha wenyewe, sisi ni tegemezi kwa kila kitu.....Ni uchungu mkali kuumeza......Lakini ndio Ukweli......Kimaendeleo bado tuko kwenye "Take off stage" na tumeganda hapo... Lumumba anatwanga maji kwenye kinu....
Kenya ni taifa la kulionea huruma sana, hawana options nyingi sana kama Tanzania na Uganda. Wakenya wamenyang'anywa kila kitu na mabeberu. Options walizobaki nazo ni kufanyakazi kwenye mashamba makubwa na viwanda vya mabeberu, michezo na Sanaa, elimu na kuendesha matatu. Ardhi Yao yowevu na yenye rutba kwa kilimo Iko mikononi mwa watu wachache sana na ardhi kubwa iliyobaki imehifadhiwa kwa national parks na misitu tangu wakati wa ukoloni na hata baada ya ukoloni; "Not yet Uhuru". Wakenya ni wakimbizi tangu enzi hizo za ukoloni mpaka leo, na Wala sio sifa nzuri ya kupigia mifano. Wakenya ni manamba ndani na nje ya nchi Yao. Hawaombi greencards kwa furaha.