Usidanganyike kaka hakuna ugumu wowote ule kwenye kupata greencard. Kama nilivyosema green card ni aina nyingine ya soko la watumwa, mahali ambao wafanyakazi wa bei rahisi wanapatikana kwa urahisi. Hata wakati ule wa utumwa sio kila mtu alifaa kununuliwa na kusafirishwa kwenda ulaya na marekani, bali walikuwa wanatakiwa watumwa wenye nguvu na vijana barobaro. Hata kwenye soko hili la utumwa mamboleo (green card) kuna vigezo ambavyo ni lazima uwe navyo ili kufanikiwa kusafirishwa huko kwa ndege. Na vigezo hivyo ni pamoja na:
1. Umri wako - lazima uwe kijana (sifa hii haijabadilika tangu enzi zilee za utumwa)
2. Uwe na nguvu, usiwe mlemavu (sifa hii pia haijabadilika tangu enzi zilee za utumwa)
3. Uwe na elimu kubwa kumudu kufundisha vyuo vikuu au ujuzi maalum kama fundi bomba kuzibua vyoo, uuguzi kutunza wazee, mifugo kuhudumia wanyama, mazingira, ujenzi, IT. HIzi ni sifa muhimu za ziada ambazo ukiwa nazo uwezo wako wa kupata green card ni mkubwa mno mno mno ajabu kama kumsukuma mlevi.
4. Kujua kuongea Kiingereza kizuri. Hii nayo ni sifa muhimu ya ziada sawa na kuweka siagi kwenye mkate. Ndio maana utakuta Wakenya, Wamalawi, Wazimbabwe, Wahindi, Waphilipino, waninigeria, Wazambia wengi wanapata green card kuliko watanzania. Kaka anza kwenda pale British Council ukajifunze kiingereza chao.
5. Wenye mitaji ya kuwekeza Marekani. Sifa hii ni muhimu kweikwei.
6. Usiwe nkorofi wa nhalifu (unlawful)
Kaka kama unasifa hizi hukai foleni sana, wasikudanganye kuwa ni bahati na sibu, sioooooo kweeeeli, vigezo na masharti huzingatiwa hata kama wanatafuta manamba.