Green Card Makulilo Lottery

Green Card Makulilo Lottery

Ni hatua tu ya maisha kama ambavyo mwingine anaanza umachinga kabla ya kuwa na duka.

Caregiver kiwanja ana hela kuliko mkurugenzi wa taasisi kubwa tu hapo bongo.
Sijaongea as a joke mtu wangu wa karibu anafanya hiyo shughuli, najua na ninajua Tena
 
Zamani nilikuwa na ndoto kama hiz!? Lkn sasa nitaenda kutembea tu nikipta nafasi, hata nisipopata Wala Sina wenge Nako.
Vijana changamkieni fursa adhimu ya kwenda na Kuishi Marekani. Full Raha kule hakuna mateso kama Nangurukuru
 
Living cost ya US inafanana na Uyui?
Nahisi jamaa uliye mtag hapa ni sahihi Bufa atakupa mrejesho wa kila kitu kuhusu America maana inaonekana wewe huna experience yoyote ile ndio kwanza una anza kukusanya taarifa na data kuhusu America.
 
Watu wengi wanadhani ukishashinda lottery unapewa green card! Thubutu😁 hapo katikati kuna documents nyingi utatakiwa kutuma na pia kuna interview, kwenye interview utalazimika kuelezea ukienda marekani utaishi wapi na utaingizaje kipato, lasivyo mchezo umeishia hapo.

Inabidi uwe Kilaza first class kushindwa interview baada ya kushinda GC. Wangapi umesikia wameshindwa interview baada ya kushinda?

Mitanganyika mnaogopa Kila kitu ndo maana hamuendelei.
 
Mkuu sijui Kwa nn unapanik hv. Relax. Lengo letu Ni moja, nafurahi kuona vijana wanakamata fursa nje ya nchi Ila sio wakaaibike kwa kukosa taarifa sahihi
Sasa vijana kutokuwa informed siyo kosa la huyo jamaa ni kosa la hao vijana wenyewe kushindwa kufanya research kabla ya kuchukua hiyo hatua maana siku hizi kila kitu kiko mitandaoni kutotafuta taarifa ni uzembe
 
Mwamba kaoa senior citizen ili kujihami kimaisha. Anawachuuza vijana eti Green card ndo itawatoa kimaisha bila kuwapa ukweli wa maisha.
Siyo kweli bana. Hajaoa senior citizen. Kwa age yake wanaendana.

Mwamba huyo ni mjanja sana. Alipofika tu akaingia jeshini (Navy). Kazunguka zunguka kwenye ma meli ya Wamarekani kwenye ma bahari huko miaka miwili mitatu akaachana na jeshi lakini njia ya kupata uraia ikawa wazi...na ni veteran anayepata mapochopocho yote ya maveteran. Na uzuri mwingine jamaa kapiga sana kitabu. Hapo nadhani ana Masters anakwenda Ph.D sasa kwenye Military Strategies na International Relations.

Hii foundation yake na channel ya YouTube ndiyo inamsaidia kupiga hela lakini pia siyo mtu mwenye njaa kivile. Na tangu anaanza haya mambo alisema tu ilikuwa ni passion yake kusaidia watu.

Binafsi namwelewa sana tu maana...
 
Jamaa anatambaa na fursa hii ya kuchanja 20,000/= kumsaidia ku-apply imemshushia thamani zaidi. Kama angekua kweli ana Nia ya nn kuokota senti za vijana?
Alinijibu instagram kwamba 20000 ni cost ya picha quality tuu. Nilikuwa nabishana na mtu kwamba hajaja kusaidia watanzania ila kaona fursa ndio akaja kujibu hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ashalamba uraia kamili, ni mwanajeshi mstaafu, wa US Navy, passport yake ya marekani roho inamuuma kuona wanaigeria wengi anataka avute wabongo wengi sijui kama atafanikiwa maana kwa ubishi tu tunajiweza
Mwanajeshi mstaafu wa US Navy lini tena wakati yeye hana miaka zaidi ya 10 huko
 
Mkuu inaonekana huyu jamaa hamumfuatilii kwa makini sijui huwa mnahisi anajulikana hapa bongo tu

Mbona alishaelezea sana kwamba kwenye interview ukiulizwa swali kama utaingizaje kipato unaweza taja kazi yoyote halali hata kama utadanganya mfano unaweza hata kusema nitaenda kujiunga na jeshi la marekani hawatajali sababu baada ya hapo hawatakufuatilia kama kweli utaenda kufanya hiyo kazi

Kuhusu kuulizwa utaishi wapi alisema pia unaweza taja state yoyote au pia kwenye kutafuta host unaweza tafuta mtanzania mwenzio aishiye huko ambako mitandaoni utawapata wengi tu kisha mkubaliane kwamba yeye ndiyo aplay kama host wako hata kama hautaenda kufikia kwake hawajali

Mkuu mitanganyika inatafuta sababu ya kuona how something WON'T work ili wasifanye badala ya kuangalia what if it works out.

Sijawahi kusikia mtu kashinga DV lottery halafu akafeli interview. Inabidi uwe kilaza pro max.

Leo mitanganyika ikifika Kenya au Nigeria wanaona kama wamefika London lakini wanigeria na wakenya kila siku wanajazana US na nchi zingine. Nchi zao zinapiga hatua kwa diaspora kutuma hela kwao (remittances) ila wabongo wenyewe kazi kukatishana tamaa na kuhalalisha kubaki kwao ili waendelee kuwa nyuma wakati wenzao wanapiga hatua.
 
Jamaa anatambaa na fursa hii ya kuchanja 20,000/= kumsaidia ku-apply imemshushia thamani zaidi. Kama angekua kweli ana Nia ya nn kuokota senti za vijana?

Wewe ndo zero kabisa. Watanzania wengi kasoro wewe hawana uelewa wa haya mambo na ndo maana wanaishia kudharau fursa. Huyu Bwana kajitoa kawapa watu ajira na kuwasaidia watanzania kwa hiari yao kujaza Form na picha sahihi kuapload. Sio jambo dogo Labda Kama wewe huwajui watanzania.

Lakini wewe mkuu umeenda kwenye makundi ya watanzania ya WhatsApp mambo ya kijinga wanalipia elfu kumi kujiunga na group wanabet nk. Kuapply Green lottery tickets Sio ushindi wa moja kwa moja Ila ndo maisha. Ohne Risiko no kuwin.

Sasa ukija huku Nchi za nje is not all honey und milch lakini jasho lako ukifanya kazi na kuwa sparsam unaweza kufanya jambo fulani nyumbani. Nampa Hongera sana Bwana EBM Ila wewe sikushangai watanzania wengi tuna umimi sana hatupendi sio tu kuvutana mkono bali hata kuona wengine wanafanikiwa. It’s very bad. You are leider one of them. Hamfanyi kitu Ila mtu akifanya tu UZI.
 
Hakuna anayempinga mwamba, na anafanya vizuri Ila afafanue zaidi kushinda lottery sio final. Kwa wastani ujiandae eg. Documentations (kupima Afya), Nauli, viza na pesa ya kujikimu ukifika US.
Pia Apunguze jazba akiulizwa kitu
Yote unayouliza ashasema mara kibao na kuwaalika watu waliopata hiyo kitu waelezee vizur jinsi walivyopenya.
Huo mchakato unakuhitaji sio chini ya mil 7 mpaka unatia mguu wako US, Health check up, Visa, Insurance, tickets etc.
Ila ukweli yote ameyasema na hajasema ni rahisi ila anahamasisha watu waombe kwa wingi na pia kawaeleza waombaji chungu na mbivu za US, So ni chaguo lao.
 
Mkuu mitanganyika inatafuta kila sababu ya kuona how something WON'T workout ili wasifanye badala ya kuangalia what if it works out.

Sijawahi kusikia mtu kashinga DV lottery halafu akafeli interview. Inabidi uwe kilaza pro max.

Leo mitanganyika ikifika Kenya au Nigeria wanaona kama wamefika London lakini wanigeria na wakenya kila siku wanajazana US na nchi zingine. Nchi zao zinapiga hatua kwa diaspora kutuma hela kwao (remittances) ila wabongo wenyewe kazi kukatishana tamaa na kuhalalisha kubaki kwao ili waendelee kuwa nyuma wakati wenzao wanapiga hatua.
Tuna tatizo mahali. Si kwa roho mbaya hii na kukatishana tamaa. Wanaijeria na Wakenya haya mambo wako sharp sana na ndo wamejazana huko. Halafu hawa hawa wa kwetu ndo utawakuta wanalia ajira hakuna.

Maisha haya ni kupambana kwa hali yo yote ile. Lakini hata watu wanaojaribu kutufungua macho nao tunawaponda. Sioni kwa nini vijana wa Kenya waenee duniani kote wakipambana lakini wa kwetu wapo tu wanalalamikia serikali iwapatie ajira; na kuporomosha matusi mitandaoni humu.

Tuna tatizo mahali!
 
Back
Top Bottom