Greenhouse katika video

Status
Not open for further replies.
Asante kwa mawazo yote mazuri. Naomba kujua Green House ni nini na nini faida zake? Ni mazao gani unayolimia Green House? Mimi nataka kuanza kulima kwenye kabusatani kangu kadogo lakini nataka kujua nini hiyo GH na inawezaje kunisaidia.
 
Katika 600,000 hii kuna gharama ya watu wa kukukatia nguzo hizi. Wakati mwingine kila kitu si lazima ununue.

kweli mkuu,
nia ni kupunguza gharama kumwezesha mtu wa kipato cha kawaida kumudu hii kitu, nimekukubali mkuu.
pamoja.
 

Mkuu Hata mie namuunga mkono kwa juhudi zake, na alinielewesha nikaelewa vizuri
Ni kwamba tu nilikuwa sijamuelewa vizuri kumbe yeye alikuwa anazungumzia material only mie nikaelewa ni kujenga complete GH, ndio maaana ukaona natilia mashaka kwa hili...
Tupo pamoja
 

Nakushukuru sana kwa kunielewa tupo PAMOJA Mkuu.
 
Mimi huku nilipo hakuna haja ya kununua hizo nguzo. Unampa hela kijana ya mboga anakukatia chap chap. Leo kijana huku ameshaanza hiyo kazi

Hebu tueleze mpaka sasa umefikia hatua gani ya ujenzi wa GH yako
 
Hebu tueleze mpaka sasa umefikia hatua gani ya ujenzi wa GH yako

Ujenzi umeshaanza. Ila si unajua tena ujenzi wa ki TZ ulivyo, taratibu taratibu. Taratibu ndio mwendo wa kinyonga. Mpaka sasa nimetoa order ya insect netting na polythene UV plastics hivyo nasubiria vifike nianze ujenzi.

Ila nimeipenda ile teknolojia ya kumwagilia ya gharama nafuu ya bwana Biashara2000. Itaniokolea zaidi ya sh. 300,000 za kununua drip pipes kwa ajili ya umwagiliaji.
 
Ofa bado ipo ni sh. 25,000 tu unaipata kwa email

Nashukuru. Ntakupigia baada ya dakika chache maana juzi jpili kwenye amka na badilika niliona jamaa anahojiwa anasema kuwa greenhouse wanajenga kwa sh. mil. 5 sasa mimi ntazitoa wapi, ila laki 6 naweza zikusanya kusanya
 
Nashukuru. Ntakupigia baada ya dakika chache maana juzi jpili kwenye amka na badilika niliona jamaa anahojiwa anasema kuwa greenhouse wanajenga kwa sh. mil. 5 sasa mimi ntazitoa wapi, ila laki 6 naweza zikusanya kusanya

Usijali hayo maisha ya kukusanya kusanya ndio maisha ya asilimia 85 ya watanzania, hivyo usijione uko pekee yako. Na watu wengi walioendelea kimaendeleo walianza kwa kujikusanyakusanya tu
 
Usijali hayo maisha ya kukusanya kusanya ndio maisha ya asilimia 85 ya watanzania, hivyo usijione uko pekee yako. Na watu wengi walioendelea kimaendeleo walianza kwa kujikusanyakusanya tu

Asante kwa kunipa moyo
 

Ni mazao gani mengine unaweza panda katika greenhouse?
 
Biashara2000 Insect netting material, Polythelin, Barb wire

Vifaa hivi vinapatika duka gani hapa Dar es Salaam na gharama zake zikoje, nataka nianze kununua vifaa vya ujenzi kidogo kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Ni mazao gani mengine unaweza panda katika greenhouse?

Lakini ningekushauri upande mazao yanayoota kwenda juu kama vile nyanya kwa kuwa utapata mazao mengi kuliko mazao yanayoota kwa kutambaa chini
 
Mkuu nimekuwa nikiifuatilia hiyo technology ya greenhouse kwa umakini mkubwa na leo ndo nimebahatika kuiona hii post na nina maswali machache kama ifuatavyo:
!. Je hizo DVD unazotoa zinaelekeza jinsi ya kuaandaa udongo katika greenhouse
2. Nilikua nikihitaji greenhouse kwa kilimo cha nyanya, Je hiyo DVD yako ina maelekezo hayo?
3. Je gharama za soil test na water test zipo inclusive kwenye hiyo 600,000/= ?
4. Je gharama za tank la maji + fertilizers zipo ndani ya hiyo bei (maana umesema inaexclude poles pekee)
5. Je una miaka mingapi katika hiki kilimo cha greenhouse na je unawezanisaidia moja kwa moja kwa makubaliano maalum kama nikipata matatizo kwenye greenhouse yangu?

Suggestions:
1. Ungepost atleast picha kadhaa za greenhouse yako ili utuongezee imani kuwa jambo hili linawezekana
2. Ungewapa wanaJF japo list ya masupplier ambayo wewe au mtu yeyote alitumia ili tusihangaike mno maana huwezi enda hardware store yeyote ukavikuta.

Vinginevyo BIG UP sana kama hii kitu inawezekana maana utakuwa umekomboa wengi maana m5 ni pesa kubwa kwa wengi wetu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…