(Gregorian calendar) Is he pious?

Sema tu mimi huwa natumia hiyo calender katika kazi na masomo maana taifa linaiiga kalenda hiyo, kiukweli kiimani mimi ninaitumia Ethiopian Orthodox Tewahedo Calender ambayo next sunday ndio pasaka. Bless. Ila ningependa kujua ni kwanini waliamua kuikataa kalenda ya Egypt wakaiweka hiyo? Huyo papa alikuwa na malengo gani? TUjuzane maana hapa naona kila mtu analeta lake, ninaomba ushahidi.
 
Vodka na Apollo,naomba mfahamu kuwa tatizo langu sio imani ya Apollo kwa sababu imani yake siijui,lakini pia kama angeniambia kuwa yeye ni mpagani wala nisingekuwa nazungumza sasa kuhusu jina lake na upagani kwani ningejua anatumia jila lililo sahihi na imani yake,tatizo linakuja pale anapotafuta excuse kuhusu uhalisi wa jina lake,Apollo ni mungu wa wapagani na jina hilo lina maana yake na linapotumika linatumika kwa maana hiyohiyo.Pia yeye kuitwa jina hilo kuna mahusiano na jina na imani hiyo kutokana na alietoa jina hilo na mazingira aliyokuwepo.Mimi nafahamu asili ya jina langu na maana yake sijakurupuka ndugu.Pia shetani ni shetani hawezi kuchangamana na Mungu!!
 
tusemeje kwa wale wasiojua kule vijijini? Wanaoita watoto wao majina kutokana labda na kupendezwa na mtu mwenye jina hilo hata kama si wapagan? Imani na jina ni vitu viwili tofauti,unaweza ukaitwa ndizi ila wewe ni binadamu au ukaitwa simba wewe si simba bali ni binadamu..Labda utoe rai kwa wana jf kwamba tujitahidi kuwachagulia wenetu majina yenye maana tunazozijua dhahiri na si kukulupuka.
 

Labda mimi niulize kitu kimoja pengine kinaweza kunisaidia kuelewa hoja yako; Hii kalenda ambayo ilikuwapo kabla ya Gregory, aliyeitunga aliitunga kwa ajili ya kumtukuza Mungu au kwa sababu zingine za kiunajimu?

Mwanzo nilidhania mada yako inabeba mjadala wa kisayansi lakini kadiri mnavyojadiliana na Kichuguu nagundua una jambo lingine nyuma ya kalenda ambalo nitalitolea mfano hapa chini kwa kifupi.

Ikiwa leo Kanisa limeamua kuchukua dhamana ya ukarabati wa majengo ya shule ya kijiji, inalazimu Askofu abadili na jina la shule?


Mimi binafsi sioni mantiki ya swali lako kuhusu kwa nini Pope hakufanya hivi na vile, labda uje straight nitakuelewa. Gregory si aliyetunga kalenda, na aliyeitunga hakuitunga kwa ajili ya Mungu. Kama kalenda ni ya Cesar, basi na tumwachie Cesar kalenda yake. Kanisa katoliki lina kalenda yake na ndio inatoa mwongozo wa dominika zote kwa mwaka, ukihoji majina yaliyotumika kwenye kalenda hii ndio nitaona mantiki lkn sio kwa hii ambayo hata wewe umekiri kuwa ni ya kaisari.
 

Nimejitahidisana kukuelewesha kuwa jina lina nguvu na linaathiri tabia ya mtu,na majina hayo yanavuta na kutengeneza nguvu kutokana na asili ya jina ndo maana unatakiwa ulijue jina lako ili ujue uko connected na nguvu ipi!Kuhusu watu wa vijijini nani amekuambia hawajui maana ya majina yao?Kama kuna mahali watu hawajui maana ya majina yao ni mijini ambako umagharibi umejaa,mtu anamuita mtoto wake Obama kisa amezaliwa siku Obama amechaguliwa.Pia kutokujua maana hakuondoi madhara au faida ya jina,ni kama gari unapoenda kukaa sehemu ya dereva sio kazi ya gari kukuuliza kama unajua kuliendesha ama la wewe ndo ujiulize kama unajua kuliendesha!Jina nalo ni hivyo hivyo,sio kazi ya jina kujua kama wewe unajua kazi na maana ya jina!Nadhani umenielewa!
 
dunia imejaa lila na fila... Kamwe lila na fila havitangamani.
 
kina realness Eiyer Kituko Vodka na wengine naomba mnijuze...

Ivi kwa nini Waislamu wanatumia mwezi na nyota kwenye alama zao??

Je dini ya Islamu yenyewe haina mahusiano na secret societies ??

Wamisri wa kale tunaowasoma kwenye mahandiko ni kweli hawakuwa waharabu??kama walikuwa weusi mbona wa sasa ni waharabu??


Mnasema USA inaongozwa na misingi ya secret societies,pia mnahiusianisha Katoliki na Secret societies.....sasa mbona hawa wamarekani hawataki kuongozwa na Rais mkatoliki??mfano JFK walimuua sababu ni mkatoliki...pia kwa nini Marekani inaanzisha madheebu mengimengi kujaribu kudhoofisha kanisa katoliki??mfano madheebu ya kilokole,ikiwa mnasema USA na Katoliki ni lao moja..
 
Last edited by a moderator:
Nimekupata ma2mbo Kuhusu Waislam kutumia nyota naomba umtafute mmoja umuulize maana ni alama za kipagani na zilitumiwa Babeli ya kale.Kama dini hiyo ina uhusiano na vyama vya siri sijui.Wamisri wa kale walikua sio waarabu hawa waarabu wa leo walikuja wakati wa utumwa.maswali yako mengine nitayajibu baadae kidogo
 
Last edited by a moderator:

nimekupata mkubwa,nasubiria.
 
Last edited by a moderator:
ma2mbo,kuhusu kanisa katoliki na Marekani ni kwamba hakuna uhasama wowote kati yao,ndo maana Bush alienda kwenye mazishi ya Papa John Paul.Huku kutokuelewana unakokusikia ni danganya toto tu hakuna kitu,lao moja,kuutawala ulimwengu na Lucifer awe mungu wao.
 
Last edited by a moderator:
Hii thread ni ya zamani sana ila kuna mtu kanirudisha hapa. Niliposoma post hii nimecheka sana; nadhani kwa mantiki hii watu wote waliozaliwa tarehe 11 mwezi wa 11 wana nguvu sana za kishetani. Nakumbuka kuwa vita ya kwanza ya dunia ilikwisha tarehe 11 mwezi wa 11 saa ya 11 (the eleventh hour of the eleventh day of the eleventh month); je vita hiyo ilimalizwa kwa nguvu za kishetani?. Kuna article nimesoma hapa inayozungumzia hiyo namba 11
 
Huu uzi niliusoma zamani ulikuwa nondo kweli. Wakati huo jf ilikuwa jf kweli aio hii ya sasa yenye kila viashiria vya face book virus. Mkuu Kichuguu upo nondo sana. Nashukuru umeupandisha na wale ma-under ground wauone.
 

Dah, kaka umeufufua huo uzi? Kweli ni balaa, tulijaribu kuuliza ni namba gani Lucifer anazitumia?, za kichina, kihindi, Kiarabu au Kirumi?, maana hiyo 11 kwa kirumi ni namba mbili, eleven kwa kirumi ni XI
 

Aisee
 

Mkuu bora umeufufua huu uzi maana sikuwahi kuusoma kuna uzi unaelezea mambo yaliyotekea 9/11 ni connect the dots.
 
Mkuu,siyo kila kinachofanyika tarehe 11 kinakuwa na maana hii niliyoisema hapa isipokuwa kinachoangaliwa ni lengo la mfanyaji....

Kuna watu wanafanya hesabu ili mtoto azaliwe tarehe 11 kwasababu zao wenyewe na huwa wanakuwa wamenuia jambo hilo na wanakuwa wameweka wakfu mzaliwa hivyo linakuwa na maana maalum....

Wewe ambaye unazaliwa huko kwenu ambaye hata hujui mambo haya na unazaliwa tarehe hii,suala hili halikuhusu kabisa.....
 
JFK hakuuawa kwasababu ya Ukatoliki wake mkuu....

JFK aliuawa kwasababu zingine kabisa na siyo ukatoliki wake.JFK alichaguliwa kwenye mwaka unaoanza na sifuri,kabla ya George W.H Bush kuchaguliwa mwaka 2000,marais wote wa Marekani waliokuwa wanachaguliwa mwaka unaoishia na sifuri waliuawa wakiwa madarakani na Bush pekee ndiye hakuuawa na hili lina sababu zake....

Kwa kukupa changamoto hebu soma hizi simmilarity za maisha ya JFK na Abraham Lincoln kisha uanze kufikiria upya.....

Jisomee hapa: Nani aliyepanga haya mauaji ya hawa Marais Abraham Lincoln na John Kennedy?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…