Kama Ni mwenyeji wa Nachingwea utakubaliana na Mimi mpk sasa hakuna shule kubwa ya bweni kuanzia kidato Cha Kwanza Hadi Cha sita
Mkuu kwanza niwapongeze kwa juhudi mnazochukua na kunitoa hofu kwamba mnashughulikia changamoto nyingi kwa kadri ya uwezo wenu.
Nawaombea kwa Mungu muzitatue changamoto hizo.
Kama Ni mwenyeji wa Nachingwea utakubaliana na Mimi mpk sasa hakuna shule kubwa ya bweni kuanzia kidato Cha Kwanza Hadi Cha sita
Hapa naomba nichangie kuwa lengo sio kuwa na shule ya boys form one -form six hapana.
Lengo ni kupata elimu bora.
Suala la wanafunzi kuchanganyika na watu wengine hili sio suala ambalo unaweza kulijengea hoja kuwa eti suala hili liwashawishi ninyi kufanya mradi wa kujenga shule ati kwa kuwa watoto wa nachingwea watachanganyika na watoto wa mikoa mingine.
Hili la kuchanganyika hitakiwi liwe kipaumbele,bali hili libaki kama faida ya ziada huku faida kuu ikiwa ni kupata elimu bora na kukuza ufaulu katika wilaya ya nachingwea.
Aidha shule hii utaweza kuwa Kama chachu ya wilaya Yetu kujulikana zaidi kwa kuwa ukamilifu wa shule hii itachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini baada ya makubaliano na serikali kuu
Hii pia haitakiwi kuwa hoja na faida ya kipaumbele ya kuwafanya nyie muhamasike kujenga shule hiyo.
Hii itakuwa mnatumia nguvu kubwa sana kwa ajili ya kutafuta faida ndogo ambayo ingeweza kupatikana katika mambo mengine ya kijamii huku nguvu mliyotumia mngewekeza katika mambo mengine.
Hamuwezi kutumia nguvu kubwa kwa kutaka mkoa ujulikane zaidi wakati kuna mambo ya msingi sana ambayo mashuleni wanafunzi wanakosa alafu mtu unakuja kuongeza hsule zingine kwa wakati huu badala ya kutatua changamoto zilizoko mashuleni.
Aidha shule hii utaweza kuwa Kama chachu ya wilaya Yetu kujulikana zaidi kwa kuwa ukamilifu wa shule hii itachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini baada ya makubaliano na serikali kuu
Nachimgwea girls pale benki mbele ipo,mumetumiaje shule hii kujulikana zaidi kama ambavyo mtatumia hiyo shule tarajiwa kujulikana.
kama we Ni mdau wa maendeleo ya wilaya yetu na upo tayri kushiriki nasi, basi njoo inbox nikuunge ktk group
Asante sana mkuu.
Kwa sasa sipo nachingwea kimakazi acha nijumuike na watu wa huku niliko kujenga taifa huku nyumbani nikijenga familia. Wa nachingwea jengeni taifa nachingwea sisi wa huku tutajenga taifa huku kwa sababu tunajenga jengo moja ila tunatofautiana huyu kashika ukuta ule huyu ukuta ule
lakini pia shule za bweni zinampa mwanafunzi muda mwingi wa kujifunza
Sio kweli mkuu.
Nataka kusema kuwa tatizo sio kwamba shule za kata hazimpi mwanafunzis muda mwingi wa kujifunza.
Tatizo ni hawa wanafunzi wenyewe,tataioz ni wanafunzi na mindset za wazazi na wala tatizo sio shule kabisa.
Nakupa mfano.
Katika shule moja hapo wilayani kuna kijana wangu amefaulu vizuri akamshinda rafiki ake ambaye anasoma shule ya bweni nje ya nachingwea.
Kwa nini huyu wa mbweni akapitwa ufaulu na huyu wa kata ?
Shida ni bweni au juhudi ya mwanafunzi ?
Na hapo jumlisha na changamoto za uhaba wa waalimu utaona kuwa shina la tatizo sio shule bali shina la tatizo ni wanafunzi wenyewe.
Sasa hapo nawapa challenge wana nachingwea mnajipanga vipi kutatua hili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na juhudi kwanza ya kusoma.
Aproach mtakayoitumia nitaona tena kama mna maono ya kweli na vijana au mnawekeza kwenye majengo tu.
Shule za bweni hazipunguzi utoro kabisa kabisa mkuu.mnachotakiwa kujua ni kuwa majengo hayambadilishi mwanafunzi bali kitakachombadilisha kwanza ni aina ya watu na utayari wa mind yake.
Usitegemee kuwa mtoto fulani akihamishwa shule ya kata huku alikuwa mtoro kisha akapelekwa bweni ukadhani atakuwa mtulivu sio kweli.
Kwani hakuna kesi za kupatikana kudoji kwa vipindi watoto wanaosoma bweni ?
Kama zipo kesi hizo kwa nini zitokee katika shule za bweni alafu wewe unahamasika kujenga mbweni kwa kutaka kuondoa jambo hili ?
hata kumuepusha mwanafunzi na mazingira hatarishi
Naomba kusema tena nachingwea hakuna mazingira hatarishi ukilinganisha na mazingira mengine ya nchi kama vile dar es salaa..
Naomba uniambie mfano wa hayo mazingira hatarishi ambayo yamekuwa na ulazima mkubwa wa kujenga shule za bweni ?
Kuna shule kama azania inafanya vizuri sana na ni day tu lakini imezungukwa na mazingira hatarishi kabisa lakini vijana wanasoma sana tofauti hata na nachingwea.
Katika sekta ya elimu hasa nachingwea changamoto sio shuele wala majengo.
Changamoto ni waalimu na mindset za wazazi na wanafunzi.
Leo tuna vijana kibao ambao wamemaliza shule wamefaulu vizuri sana lakini hawana ajira yeyote,na vijana hawa wanaweza kuwasaidia wanafunzi waliopo mashuleni.
Mnawaangalia vipi hawa vijana kuhakikisha kuwa wanawasaidia wenzao kufaulu (msijekutaka wafanye kazi ya kanisa)
Nachingwea day na nambambo day ni shule zilizoko mjini ni mfano kwa shule nyingi hapo nachingwea,lakini shule hizi unaweza ukaenda ukakuta mwalimu wa mathematics ni mmoja shule nzima.
Masomo ya sayansi kabisa walimu ni tatizo.
Nyie mnafocus katika majengo wakati kinachofanyika katika hayo majengo bado kinahitaji sapoti kubwa sana.
Wekezeni rasilimali watu,tumieni vijana wanaomiza kukuza elimu,msitumie pesa zenu kukuza majengo mkuu.
Badala ya kuboresha vilivyokuwepo mnataka kuanzisha vipya ambavyo vitakutana na changamoto inayokutana navyo hivi vilivyokuwepo