Sijaelewa hii pesa itatolewa mfukoni kwa mtu anayeitwa GSM au itatolewa na kampuni inayotambulika kama GSM group of Companies.
Motive ya hii nini?
Hizo fedha zikitoka huko zinakotoka zitatambulika zimetoka kama nini? Sponsorship, advertisement au Aidful?
Utaratibu wa nchi yetu hasa ni upi juu ya mtu au kampuni itakapoamua kugawa kiasi kikubwa kama hiko cha fedha kwa Third parties?
Kwamba ni rahisi mtu au kampuni kuinject pesa kutoka outsource kiasi hiki?
Inawezekana vipi kiasi cha bil 1.9 kitolewe tu kama zawadi?
Au wamemaanisha hii itakuwa pesa ile ya ZAWADI ya ushindi yaani Bil 4.7 ndio katika humo watatoa kiasi hiko kwa kila mchezaji.
Hii taarifa ndio nimeiona muda si mrefu, ila bado napata mashaka ni kama hii taarifa haijakamilika.
Siamini kama nchi hii unaweza kuwapa watu zawadi bil 1.9 bila kuulizwa source ya hiyo pesa and how gharama hii itereheshwa?
Wadau naomba tuiweke hii kitaalam zaidi. Nimeshtuka sana na habari hii.
Nani halisi atatoa pesa hii, na itatoka kutoka kwenye Source ipi, na let say kwenye financial statements how will it be recorded so as to qualify as an expense.