GSM, Mshindo Msola tuachie Yanga yetu

Unknown2

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2016
Posts
2,352
Reaction score
5,055
Baada ya kuangalia mechi yetu ya leo haya ndo mawazo/maoni/maswali na mapendekezo yangu

1. GSM kupitia Hersi Said kwanini wanahusika kwenye usajili wa wachezaji? Yani Hersi ndo scout wa Yanga, tangu lini akasomea fani hiyo?

2. Kwanini GSM amekuwa mtendaji wa Yanga? Vitu kama wiki ya Mwananchi karatibu yeye na mapato kachukua yeye, mishahara analipa yeye na mechi na maandalizi yake anafanya yeye, Hii ni sawa?

Matokeo yake timu imekosa weledi kabisa. Mfano, kambi ya Morocco ilikuwa na faida gani zaidi ya utalii?
Mchezaji wa kwanza kusajiliwa anakosaje ITC?

Nguvu iliyowekwa kwenye tamasha la Mwananchi kwanini haikuwekwa kwenye kuandaa timu?

Mshatuona limbukeni kwa kupania mechi ya Simba tu.
Maandalizi ya nje ya uwanja mnafanya mkicheza dhidi ya Simba tu, hivi hamjui mpira wa kiafrika ni fitina?

Hamkumuuliza hata Manara wenzenu walikuwa wanafanyaje?
Matokeo yake kimataifa hatuna tunalolifanya zaidi ya kuaibisha nchi.

Sisi ni wa kuzidiwa na Biashara?
Miaka minne timu haina hata ubingwa wa nchi afu eti tujivunie uwepo wenu kweli?

Haya yote yanafanyika Mshindo Msola yupo. Nafasi yake kama mwenyekiti ina maana gani?
Yani Hersi ana nguvu kuliko Msola?
Bwana Msola tunaomba utupishe haraka kabla hatujachukua hatua. Wewe uko ndani ya uwezo wetu. Kwenye uchaguzi huwezi shinda .

GSM tuachie Yanga yetu. Jezi tutawapa wengine. Kuitumia timu yetu kibiashara huku matokeo uwanjani yakiwa sifuri sasa basi.

Bora timu iendeshwe kwa michango kuliko uwepo wenu.
Kashfa zenu tunazijua ila tulikuwa tumewastahi tu.

Nb: Soma hii;


Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center (GSM Foundation)
 
Hakuna wanachokifanya zaidi ya maigizo.
Waondoke mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Tunaelekea kutolewa kimataifa na huenda tukakosa ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya tano mfululizo!
 
Hili ni Simbilisi.
Usifananishe wasomali na wanaija.
 
Kama unataka upewe timu, jitambulishe kwa wanachama wakikukubali timu utapewa. Onyesha uwezo wako na malengo yako, Yanga ni timu ya Wananchi atakapo ishia GSM wewe utaendeleza.
 
You guys needs to organize your club contemporaly.
1. Governance - Msola & Team.
2. Management - Aachiwe Kocha.
3. Financers - GSM + Other. Bring in more financers, this depending on GSM is a high risk option.
 
Upuuzi tu mnauwezo huo wa kuitunza timu hata kwa wiki moja?!!hizo buku tu kwa mwezi mnasubilia hadi mkutano mkuu, ndio mzilipe?!!kwanza hata cjui hawa kina Mo, na GSM, wanapata faida gani kwenye hizi timu?!!
 
Yanga haina mwanachama wala shabiki wa ovyo ovyo kama wewe, ayo mambo kamwambie mo ndo awaachie timu yenu, unajivika uyanga unatuandikia upuuzi wako apa, tuonyeshe kadi yako ya uanachama ni ngapi, mambo ya yanga waachie wanayanga ayakuhusu propaganda za kijinga hizo kamwambie babra na kanjibhai wenu mo uko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…