GSM na Hersi mmekivuna mlichokitaka kwa Manara

GSM na Hersi mmekivuna mlichokitaka kwa Manara

vibertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
2,474
Reaction score
4,726
Manara hajawahi kuwa na weledi hata siku moja katika kauli zake, hajawahi hata kuonesha ni kama mtu mzima mwenye busara ni kama bado kijana wa under 18 anayejifunza baya kipi na zuri kipi. Kaharibu shughuli yote iliyokuwa imefana kwa uswahili aliuokuwa na hilo mmelifuga wenyewe GSM na Hersi Saidi na mbaya zaidi anapenda kulazimisha kujiona ndio kila kitu asitishwi wala asikii mpaka anachotaka yeye kitekelezeke.

Tukio la leo kuna wageni mbalimbali wengine walikuwa uwanjani wengine walikuwa wanafuatlia kupitia TV na mitandaoni, Manara alichokifanya hakihusiani na tukio la leo bali ni mambo binafsi ya faragha za watu yeye anamtambulisha Mobeto kama ni nani kwenye taasisi ya Yanga? Analeta mambo ya mapenzi ya mbele ya kadamnasi kupitia image ya taasisi ya Yanga. Sasa kumlea kwenu kumeleta aibu kubwa kwa taasisi ya Yanga.

Watu walipiga kelele sana kumpa nafasi huyo kirusi lakini hamkutaka kusikia sasa leo kaamua kuharibu image ya taasisi kwa tukio linalofatuatiliwa na watu wengi kwa leo.

Mnachokifuga ndicho hicho na bado
Soma Pia: FT: Yanga 2-1 Red Arrows | Siku ya Wananchi 2024 | Mkapa Stadium


 
Biashara ile wewe...Kila kitu ulichokion kiko planned...Itifaki ilizingatiwa...Yanga Bingwa.
Unprofessional planned. Watu wenye akili timamu hamuwezi kufedheheshana mbele za watu waliopo uwanjani na wanaofuatilia. Acha kutetea ujinga, mimi ni Yanga kindaki ndaki ila lile tukio ni aibu ukiangalia hata wahusika wenyewe hawakuridhika nalo.
 
Unprofessional planned. Watu wenye akili timamu hamuwezi kufedheheshana mbele za watu waliopo uwanjani na wanaofuatilia. Acha kutetea ujinga, mimi ni Yanga kindaki ndaki ila lile tukio ni aibu ukiangalia hata wahusika wenyewe hawakuridhika nalo.
Msamehe babu yetu, umri ukienda akili inakuwa kama ya mtoto
 
kwamba unadhani kina Eng. Hersi hawakujua kuwa Hamisa ataitwa leo?
Kwamba una uhakika kuwa alijua, kwa vigezo au uthibitisho upi? Kilichofanyika ni ujinga mno kuna mambo ya ovyo ovyo vinapoteza muda kama hayo. Mtu unalazimisha Mobeto Mobeto mara siondoki mpaka Pacme aje. Upuuzi mtupu mbaba mtu mzima akili za ovyo.
 
Back
Top Bottom