GSM na Hersi mmekivuna mlichokitaka kwa Manara

Mimi na mpira nimeshindwa kabisa hasa huu wa Bongo watu kama huyu manara ndiyo mtihani mkubwa,zamani nikiwasikiliza yule alikuwa Ruvu na yule wa Mtibwa maarufu wazee wa Manungu hawa hata kama mpira huuelewi unapenda zile tambo zao.

Nilikuwa namsikiliza sikumbuki ni efm au wasafi akihojiwa kuhusu siku ya yanga na kitenge wakizungumza kitu kama alifunguliwa kifungoni sasa alivyokuwa anaongea dizain kama jamaa siyo mzima sanaa,nahisi ana shida somewhere au uswahili umemzidi!
Una maana Bwire na Kifaru?
 
Manara hajawahi kuwa na weledi hata siku moja katika kauli zake, hajawahi hata kuonesha ni kama mtu mzima mwenye busara ni kama bado kijana wa under 18 anayejifunza baya kipi na zuri kipi. Kaharibu shughuli yote iliyokuwa imefana kwa uswahili aliuokuwa na hilo mmelifuga wenyewe GSM na Hersi Saidi na mbaya zaidi anapenda kulazimisha kujiona ndio kila kitu asitishwi wala asikii mpaka anachotaka yeye kitekelezeke.

Tukio la leo kuna wageni mbalimbali wengine walikuwa uwanjani wengine walikuwa wanafuatlia kupitia TV na mitandaoni, Manara alichokifanya hakihusiani na tukio la leo bali ni mambo binafsi ya faragha za watu sasa kumlea kwenu kuleta aibu kubwa kwa taasisi ya Yanga. Watu walipiga kelele sana kumpa nafasi huyo kirusi lakini hamkutaka kusikia sasa leo kaamua kuharibu image ya taasisi kwa tukio linalofatuatiliwa na watu wengi kwa leo.

Mnachokifuga ndicho hicho na bado
Manara si mtu sahihi kupewa uongozi popote pale, kwa kifupi hafai.
 
Tokea lini hawa Uliowataja hapa wakawa / waliwahi kuwa na Akili? Wenye Akili ni Mo Dewji na Ahmed Ally pekee Mkuu.
 
Back
Top Bottom