GTV: Ndio tumekula hasara au?

GTV: Ndio tumekula hasara au?

TCRA wanapambana na kivuli! Hivi mtu unaweza kupambana na kitu ambacho hakipo na ukapata majibu? Nadhani TCRA wanataka kuonekana kuwa wananchi kuwa wanafanya kazi yao barabara. Ni vema wachukulie suala hilo kama somo tu kwa siku zijazo
 
Nauliza hivi? lile liungo na decoder(sijui kama inaandikwa hivi) litakuwa na kazi gani tena? unaweza ukanunua receiver uakalitumia kwa kutumia ule ungo? au kwa ufupi unaweza kutumia kwa njia nyingine? je kama halina kazi tena unawza ukarudisha na wakakulipa hela zako?

Nadhani hapa kuna hoja ya msingi. Gharama za kurudishiwa wateja isiwe tu zile za monthly subscription bali hata vifaa kama decoder na satelite dish. Hata kama vifaa hivi vitaweza kutumika na kampuni nyingine, sio lazima kwamba kila mteja anataka kuvitumia tena. Naamini wengi watakuwa hawavihitaji tena. GTV inapaswa pia kuwafidia gharama za vifaa hivi.
 
Waheshimiwa mimi ningependa kumfahamu huyo Mtanzania anyyemiliki asilimia hamsini ya hisa zote za GTV- Tanzania Ltd. Kumfahamu kutatusaidia kuweza kujua way forward
 
Hapa kuna jambo la ziada la kuzingatia. Je, inawezekana vipi kampuni ikafunga virago bila kuwasiliana na wadau? Kingine ni vipi mtu unaweza kuingia mkataba na mtoa huduma bila kujua hatma yako kama huduma itasitishwa?

Hili jambo si kwa GTV pekee, tujiulize tunapopanda magari ya kwenda mikoani, kuna mkataba gani kati ya mwenye basi na abiria katika swala zima la fidia endapo ajali itatokea?

Kuna maswali mengi na mengi zaidi ya kujiuliza katika maisha yetu ya kila siku kama Wadanganyika.
 
GTV kama imefilisika,taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwekwa chini ya Mfilisi (Receivaship) zifanywe, ili kama ina asset zozote zitumike kulipa madeni yalipo ikiwa ni pamoja na advances za subscribers! TCRA hawawezi eti kuwaambia GTV walipe wakati wamefilisika, bali wafuate sheria zinavyosema!
 
Siijui TCRA wanapambana na nani hapa na wanategemea nini. Labda waiombe GTV bailout serikalini
 
Hakuna kitu hapo, mafuta mkwara washushe, hadi leo hawajashusha, hao ndo watarudisha hayo mapene?
 
Ndugu zangu Watanzania, tunaelekea wapi? Mashirika au makampuni yanasitisha huduma zake bila wananchi kuelezwa. Nimepokea kwa mshtuko kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa kampuni ya GTV imefunga huduma zake hapa Tanzania na kwingineko Afrika. Je ina maana hii kampuni haikujua kwamba imefilisika au itasimamisha huduma zake karibuni au ni makusudi? Nimesikia hata juzi kama si wiki iliyopita walikuwa wakifanya kazi kama kawaida? Je hatima ya waliolipia huduma mbalimbaili zikiwemo za kuangalia au kuonyesha michezo mbalimbali ikiwemo mipira hatima yao itakuwaje? Je kitendo cha kihunihuni kama hicho kitokeapo sheria inasemaje au itamlindaji alieonewa?
 
Ndugu zangu Watanzania, tunaelekea wapi? Mashirika au makampuni yanasitisha huduma zake bila wananchi kuelezwa. Nimepokea kwa mshtuko kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa kampuni ya DSTV imefunga huduma zake hapa Tanzania na kwingineko Afrika. Je ina maana hii kampuni haikujua kwamba imefilisika au itasimamisha huduma zake karibuni au ni makusudi? Nimesikia hata juzi kama si wiki iliyopita walikuwa wakifanya kazi kama kawaida? Je hatima ya waliolipia huduma mbalimbaili zikiwemo za kuangalia au kuonyesha michezo mbalimbali ikiwemo mipira hatima yao itakuwaje? Je kitendo cha kihunihuni kama hicho kitokeapo sheria inasemaje au itamlindaji alieonewa?

Mkuu umetokea wapi...ni GTV na sio DSTV...DSTV bado wako hewani....nilifikiri wataka kusema kuwa zile mechi ambazo GTV walikuwa anaonyesha kwa sasa DSTV..

Kazi njema....Mods mnaweza futa hii thread
 
Duh! Naona mkuu umechanganya service providers DsTV ni wale wa MNet na bado wapo, waliofunga ni GTV. Pole!
 
mhache inaelekea hujui tofauti kati ya gtv na dstv.......do research mr kabla ya kuongea.
 
C gtv pekee kumbe hata dstv ?

Sina hakika kama ni kweli kwa sababu dk 10 zilizopita nilikuwa naangalia skynews na lunch yote nimepata naangalia skysport

Tafadhali thibitisha source basi!
 
Ndugu zangu Watanzania, tunaelekea wapi? Mashirika au makampuni yanasitisha huduma zake bila wananchi kuelezwa. Nimepokea kwa mshtuko kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa kampuni ya DSTV imefunga huduma zake hapa Tanzania na kwingineko Afrika. Je ina maana hii kampuni haikujua kwamba imefilisika au itasimamisha huduma zake karibuni au ni makusudi? Nimesikia hata juzi kama si wiki iliyopita walikuwa wakifanya kazi kama kawaida? Je hatima ya waliolipia huduma mbalimbaili zikiwemo za kuangalia au kuonyesha michezo mbalimbali ikiwemo mipira hatima yao itakuwaje? Je kitendo cha kihunihuni kama hicho kitokeapo sheria inasemaje au itamlindaji alieonewa?

Bwana Mkubwa Mhache, hapo naona umekurupuka. Vyombo vya habari gani hivyo unavyotaka kuvisingizia? Muda huu niko home najiriwadha kwa kuangalia kipindi murua channel ya AMAGIC toka DSTV. Kama una maana ya GTV basi ungesema hivyo!!!
 
Hata hivyo kufungwa gafla kwa GTV ni kielelezo tosha cha kuifanya serikali iwe makini inawakaribisha wawekezaji kwani ni hatari kwa uchumi wa nchi huduma kufungwa gafla bila kuwataarifu wadau.
 
Mzee umeropoka, sio DStv ni GTV (General Television)
 
The mix up here is the same as when all petrol stations are reffered to as sheli in tanzania, chewing gums Big G and the like
 
Duh!!Mwanewane radio mbao yako inatisha!!au wamekukatia wewe tu??jaribu wasiliana nao ukute hawajapata malipo!!!pole sana!!
 
Back
Top Bottom