Guardiola ameiumbua E.P.L

Guardiola ameiumbua E.P.L

Nimejikuta nacheka kwa sauti hiyo sehemu ya msalaba wa jumuiya da! Ila we jamaa hata kama ni ushabiki hii too much
 
Kwakuwa umeandika kishabiki zaidi na mahaba mazito kwa La liga, naomba nikukumbushe kuwa kuna mzunguko wa pili bado haujaanza, kumbuka msimu uliopita.

Kuhusu ubora wa Guardiola, kwangu mimi ni mtu anayetembelea michoro ya wenzake na kutegemea pesa zaidi. Timu zote alikutwa zimesukwa vyema, ni kama Vicente Del Bosque alipopewa Spain akatwaa ndoo kubwa, kazi yake kubwa ilikuwa nini?
Kocha gani A list sahizi hategemei pesa mkuu..

Mpira ni pesa, kuanzia mourinho, zidane na wengineo wote angalia gharama za vikosi vyao.

Kimsingi hoja yako ya pesa haina mashiko, maana timu kibao zimesajili ikiwemo ile iliyotoa paundi milioni 70 na zaidi kupata kina lukaku na morata lakini perfomance hamna kitu.
 
Liga haijaisha lakini, kumbuka hili. Uwe na akiba ya maneno.
Tuone nani atamfunga Man city
Kengele, sio kwa hivyo vichapo anavyogawa nyumbani kwa timu zenye reputation kubwa namna ile.
 
nakumbuka msimu wa 2011/12 Man U walikuwa mbele kwa point 8 kumzidi Man City huku zikiwa zimebaki mechi 6 tu ligi kwisha.
badala yake ni Man City ndiye aliyebeba ndoo ya EPL.

sasa hivi Man City wapo mbele pointi 11 na mechi zimebaki zaidi ya 20.

wacha EPL iitwe EPL!
Unasema hivyo wakati huko La liga karibia kila msimu bingwa anapatikana siku ya mwisho.

E.P.L ingekuww inatokea hivyo tungesema ama kweli ligi ngumu ila kwa vile ni la liga tunachukulia poa tuu
 
Wewe unamatatizo wewe, Hujui kuwa Pep anashinda kwa bahati tu ? alimfunga Man U kwa bahati tu, amemfunga Swansea leo kwa bahati tu 4-0, ila mpira upo man U, kashinda Goli moja tu leo na Bounemouth, kachukua point tatu kashinda 1-0 , yeye hajashinda kwa bahati bali hua anapiga mpira.

Kwa ujumla Top 4 ya EPL inampira mzuri sana tatizo ni pale wanapoamua ku pack Bus,
Hahaha
 
Siyo kweli!!.... Hajakutana na Big sam akiwa na timu,Hajakutana na Allan Pardew Akiwa na Timu....nnachotaka kukwambia ni hivi kwa England bado Usimuhesabie kama ni bingwa huyo Ligi bado sana hiyo
Yaani ampige Jurgen kloop goli 5, amtandike Mourinho old trafford, ampige Conte stamford bridge..

Halafu umtishie Big Sam[emoji1] [emoji1] [emoji1] .. you cant be serious!!
 
Mleta hana kumbukumbu vizuri ya mpira wa ulaya. Huyo guardiola alikula kichapo KWA Chelsea drodga akitupia, kule KWAo tulitoka mbili mbili, Chelsea tuichukua ndoo ya ulaya, huyo guardiola yupo. Hata msimu uliopita, sisi Chelsea jiwe la uingereza tulimgonga nje ndani, tena pale KWAo alikula tatu moja, tena walianza kutufunga sisi, hii timu imetumia FEDHA nyingi kusajiri wachezaji wazuri tu
Chelsea haijawahi kuifunga barca ya guardiola goli 3 bwana, wala guardiola kuifunga chelsea akiwa Barca.

Kuna mechi iniesta alisawazisha, Barca wakapita kwa goli la ugenini, ile game nyingine Torres alipiga goli dakika ya 90+ ikawa 2-2, chelsea wakapita maana home walishinda goli 1-0.

Sasa waulize wenzako wa England, Arsenal na Man united kilichokuwa kinawatokea wakikutana na Guardiola alivyokuwa Barca
 
Kwani bingwa mtetezi ni Nani, ni yeye????, Yaaani kufanya vizuri msimu mmoja tena ambao bado haujaisha tayari makelele yameshaanza, mnataka mumpe na ufalme kabisa, akae muda aliokaa na Barça halafu Baada ya hapo ndio uje kutoka Hiyo tathmini yako, vinginevyo utakuwa unaleta ushabiki tuuuu
Pep hachukui tuu ubingwa ila anauchukua in style..

Kushinda mechi 15 mfululizo kwa ligi inayoitwa ngumu unadhani ni mchezo?

Halafu hakuna cha kupaki basi wala daladala, ni mwendo wa kushambulia tuu mwanzo mwisho
 
Ungesubili mpaka mwakani kuanzia mwezi March ndo ufungue huu uzi....kama vipigo tu unavoviongelea au kama ni kutokufungwa kwa mechi 15...basi tayari mzee Wenger alishaimbua EPL kitambo sanaaaaa...yeye alichukua ligi bila kufungwa mechi hata moja.
Ipo tofauti ya kutofungwa mechi 15 na kushinda mechi 15 mfululizo..

Kipindi wenger anatamba timu zilizokuwa kali zilikuwa ngapi, sahizi chelsea, man city, Tottenham na wengineo wanawasha moto wa hatari
 
wewe
Pep hachukui tuu ubingwa ila anauchukua in style..

Kushinda mechi 15 mfululizo kwa ligi inayoitwa ngumu unadhani ni mchezo?

Halafu hakuna cha kupaki basi wala daladala, ni mwendo wa kushambulia tuu mwanzo mwisho

Wewe ni mfia guardiola tu kama wafia guardiola wengine tuliowaona kule barca

Time will tell
 
Uzuri mmoja EPL hutambi mara mbili, subiri mwakani uone.

Nakataa EPL sio ligi ya timu moja. kuongoza ligi haimaanishi ni timu moja. Mbona Championship group stage timu zote za EPL zimeongoza katika hayo makundi isipokuwa Chelsea ambayo nayo ni kwa sheria mbaya za UEFA ndizo zimemnyima kuwa top. Utaona mpaka semi final EPL zitatawala tu.

Uwepo wa makocha 5/6 bora duniani kwenye EPL sio mchezo bana
Unapokataa sio ya timu moja utuambie nani aliyeipa au anayeipa Man city challenge huko England..

Au nitajie katika Ligi unazojua ngumu,nani anaongoza kwa pointi nyingi kama Man city
 
Uzuri mmoja EPL hutambi mara mbili, subiri mwakani uone.

Nakataa EPL sio ligi ya timu moja. kuongoza ligi haimaanishi ni timu moja. Mbona Championship group stage timu zote za EPL zimeongoza katika hayo makundi isipokuwa Chelsea ambayo nayo ni kwa sheria mbaya za UEFA ndizo zimemnyima kuwa top. Utaona mpaka semi final EPL zitatawala tu.

Uwepo wa makocha 5/6 bora duniani kwenye EPL sio mchezo bana
Ukisema hutambi mara 2... unasahau Man untd ile ya kina Cr7 ilishachukua ubingwa mara 3 mfululizo
 
Ki ukweli Pep anajua hilo halipingiki. Ila napata kigugumizi kuamini kwamba anaweza kumaliza ligi hajapoteza hata game moja.

UEFA, EPL, Carabao, FA

Hata wachezaji wenyewe siyo vyuma wale watachoka. Hizo rekodi ziliwekwa kitambo si kwa sasa na EPL hii. Kuhusu ubingwa ana asilimia kubwa mpk sasa lakini mechi bado ni nyingi mno. Time Will Tell
weee uyo pep kunyanyasa vigogo mwisho hukoooo epl na FA, huku UEFA huku kuna wenyewe.mark my words, and subiri uone hii hatua ya 16 bora.
UEFA ndo kuna maajabu yasiyofikirika kufanyika.
 
Wewe unamatatizo wewe, Hujui kuwa Pep anashinda kwa bahati tu ? alimfunga Man U kwa bahati tu, amemfunga Swansea leo kwa bahati tu 4-0, ila mpira upo man U, kashinda Goli moja tu leo na Bounemouth, kachukua point tatu kashinda 1-0 , yeye hajashinda kwa bahati bali hua anapiga mpira.

Kwa ujumla Top 4 ya EPL inampira mzuri sana tatizo ni pale wanapoamua ku pack Bus,

Mkuu wazungu wana msemo wao wa "Fortune Favors the Brave".

Hapo sihitaji kuelezea zaidi.
 
Kwakuwa umeandika kishabiki zaidi na mahaba mazito kwa La liga, naomba nikukumbushe kuwa kuna mzunguko wa pili bado haujaanza, kumbuka msimu uliopita.

Kuhusu ubora wa Guardiola, kwangu mimi ni mtu anayetembelea michoro ya wenzake na kutegemea pesa zaidi. Timu zote alikutwa zimesukwa vyema, ni kama Vicente Del Bosque alipopewa Spain akatwaa ndoo kubwa, kazi yake kubwa ilikuwa nini?
Hio michoro mbona inawashinda wengine?
 
Back
Top Bottom