Guardiola ameiumbua E.P.L

Guardiola ameiumbua E.P.L

Nadhani watu wengi tunakumbuka ile Barcelona ya 2009-2012 ambayo kwa wengi ni timu bora kabisa katika kizazi hiki cha soka, kuanzia ugawaji wa vipigo,kandanda safi na uwezo binafsi wa wachezaji.

Wakati Guardiola akiiongoza Barcelona kugawa vichapo vya hatari hadi kumtetemesha mzee wetu Ferguson kwenye fainali ya Uefa 2011 wengi walikuwa wanammbeza kwa kusema anacheza ligi ya timu 2, ooh mara kabebwa na messi, wengine wakasema ana bahati.

Guardiola akaondoka zake kwenda Bundesliga, huko nako akagawa vichapo vya kutosha, ila wadau wa England wakaendelea kumponda kuwa anaiogopa England maana sio size yake [emoji23](wakajisahaulisha kilichokuwa kinazikumba timu za England zilipokutana na Barcelona).

Haya sasa , mara Guardiola akaja hapo England, ni kweli msimu wa kwanza hakufanya vizuri ila wadau wa England wakatamba sana eti alidhani yupo la liga au ligi nyingine nyepesi, hii ndio England bwana, timu zote kali!!!!

Msimu wake wa pili, akaanza kwa kasi ndogo, wakaongea sana,alipoanza kugawa vichapo wakasema ngoja tumuone, hawezi fika mbali hii ndio England, mara kashinda game 10 mfululizo, akashinda nyingine 5(still counting), humo kagawa vichapo na kuupiga mpira mwingi mno ikiwemo nyumbani kwa timu vigogo kama Man untd na chelsea.

Sasa hivi England ni ligi ya timu moja tuu, Man city imegeuka kama msalaba wa jumuiya ambao unapita kila nyumba, Guardiola hajawahi kuwa na timu iliyokusanya pointi nyingi hivi ndani ya mechi 16 za kwanza, cha kushangaza huku ambapo Guardiola anajipigia tuu watu ndio tunaambiwa ni ligi ngumu lakini kule ambapo alikuwa na timu ya Dunia alikuwa hashindi hivi tunaambiwa ile ligi ni mbovu/rahisi.!!

Kinachotokea sahizi si kingine bali ni E.P.L kuumbuka, tayari Pep amejipigia vigogo wote wa E.P.L wengine kwa aibu ya goli 5....,tungojee mwisho wa msimu tuone mambo yatakuwaje ila without doubt Man city watanyanyua makwapa
Mapema mno.
 
Kubali tu na kumpa Heshima yake Pep. Jamaa yuko vizuri,anajua anachokifanya.
Kama siyo kocha bora huwez kuwa na mafanikio. Cha msingi anajua kutumia pesa kununua wachezaji watakao msaidia. Timu zingine kubwa kama Chelsea,Man U nazo zinatumia pesa nyingi tu. Badala ya kucheza mpira wa kufunguka,wa kufurahisha,unapaki basi na mambo mengine. Pep ni zaidi ya kocha!
Siyo kweli!!.... Hajakutana na Big sam akiwa na timu,Hajakutana na Allan Pardew Akiwa na Timu....nnachotaka kukwambia ni hivi kwa England bado Usimuhesabie kama ni bingwa huyo Ligi bado sana hiyo
 
Siyo kweli!!.... Hajakutana na Big sam akiwa na timu,Hajakutana na Allan Pardew Akiwa na Timu....nnachotaka kukwambia ni hivi kwa England bado Usimuhesabie kama ni bingwa huyo Ligi bado sana hiyo
Yawezekana,lakini jamaa anajua,tukiondoa mambo mengine
 
Watu wanaosema et ligi bado mmeona mpira anaocheza man city kweli?jamaa anapiga mpira kuliko timu yoyote hapo na hamna aliomfikia kwa mpira anaopiga.ushindi wake sio wa kibahati huyu jamaa analitaka hili kombe kufa kupona na hatolikosa in anymeans wachezaji wake wana njaaa kuliko wachezaji wote epl.
 
Ki ukweli Pep anajua hilo halipingiki. Ila napata kigugumizi kuamini kwamba anaweza kumaliza ligi hajapoteza hata game moja.

UEFA, EPL, Carabao, FA

Hata wachezaji wenyewe siyo vyuma wale watachoka. Hizo rekodi ziliwekwa kitambo si kwa sasa na EPL hii. Kuhusu ubingwa ana asilimia kubwa mpk sasa lakini mechi bado ni nyingi mno. Time Will Tell
 
Sawa pamoja na kugawa vipigo mfululizo,lakini bado nsiona mancity sio timu stable moja kwa moja.
Lazima huko mbele kuyatokea badiliko
 
Mleta hana kumbukumbu vizuri ya mpira wa ulaya. Huyo guardiola alikula kichapo KWA Chelsea drodga akitupia, kule KWAo tulitoka mbili mbili, Chelsea tuichukua ndoo ya ulaya, huyo guardiola yupo. Hata msimu uliopita, sisi Chelsea jiwe la uingereza tulimgonga nje ndani, tena pale KWAo alikula tatu moja, tena walianza kutufunga sisi, hii timu imetumia FEDHA nyingi kusajiri wachezaji wazuri tu
 
watu kukiri tu kuwa pep anajua anachokifanya wanaona kama watapungukiwa damu [emoji23] [emoji23] .

ila ndo ukweli huo jamaa anajua na ni kocha mzuri sana.

naanza kuona man city ikipata mashabiki wengiiiii [emoji3] [emoji3] [emoji3] hasa kutoka Arsenal na Liverpool
 
Walisema Hajakutana na timu kubwa.
Sasaivi ngoja mzunguko wa pili
kwenye mzunguko wa pili sio timu kubwa itamfunga, namaanisha ( Man u, Chelsea, Liverpool, Arsenal ) na hawa ndio wapiga kelele.
Mzunguko wa pili utakuwa mgumu, zile bahati za wachezaji wa timu pinzani kuonyeshwa red cards, wacheji muhim kutokuwepo na magoli ya offsides hayatajirudia
 
Wewe unamatatizo wewe, Hujui kuwa Pep anashinda kwa bahati tu ? alimfunga Man U kwa bahati tu, amemfunga Swansea leo kwa bahati tu 4-0, ila mpira upo man U, kashinda Goli moja tu leo na Bounemouth, kachukua point tatu kashinda 1-0 , yeye hajashinda kwa bahati bali hua anapiga mpira.

Kwa ujumla Top 4 ya EPL inampira mzuri sana tatizo ni pale wanapoamua ku pack Bus,
Mashabiki wa Man U , Eti Man City kamfunga Man U kwa bahati. Mahaba niue au ulikua unaangalia Live Score au umesimuliwa kijiweni. Tusibishane sana ingia You tube tu utaona jinsi Man City walivotakata hasa second half tena alivoingia Cadabra ni zaidi na mwishoni man u ailikua anakufa kuanzia goli 2 maana walitengea clear chances nyingi na walikua wanajiamini mno. Bahati analikua nayo Man U kufungwa goli chache. Usiwe na mapenzi ya ajabu. Na kama unabisha hili nitafute tuwekeane uone jinsi Man United atakavopigwa magoli mengi mzunguko wa pili dhidi ya Man City.
 
Kwakuwa umeandika kishabiki zaidi na mahaba mazito kwa La liga, naomba nikukumbushe kuwa kuna mzunguko wa pili bado haujaanza, kumbuka msimu uliopita.

Kuhusu ubora wa Guardiola, kwangu mimi ni mtu anayetembelea michoro ya wenzake na kutegemea pesa zaidi. Timu zote alikutwa zimesukwa vyema, ni kama Vicente Del Bosque alipopewa Spain akatwaa ndoo kubwa, kazi yake kubwa ilikuwa nini?
Sasa ndugu yangu unataka kocha awe na kikosi chepesi jmn
 
Naona wengine anawapiga kwa woga wao tu, timu sio kiwango viile, wanacheza mpira wa kawaida, wanadive na wakati mwingine wanatembelea nyota ya refa
 
nakumbuka msimu wa 2011/12 Man U walikuwa mbele kwa point 8 kumzidi Man City huku zikiwa zimebaki mechi 6 tu ligi kwisha.
badala yake ni Man City ndiye aliyebeba ndoo ya EPL.

sasa hivi Man City wapo mbele pointi 11 na mechi zimebaki zaidi ya 20.

wacha EPL iitwe EPL!
Kipindi icho man u ilikua inafifia bna usiiringanishe na city hii ambayo ukicheza nayo ww kazi yako ni kupunguza idadi ya magoal tu
 
Back
Top Bottom