CalvinPower
JF-Expert Member
- Nov 25, 2008
- 1,634
- 1,001
Kwa mwenendo wa ligi unavyoenda na nikilinganisha na uwezo wa Pep Guardiola katika kukinoa kwake Kikosi cha Man city nashawishika kabisa kuwa Mkufunzi huyu mahiri wa soka pasipo na shaka wala wasiwasi wowote atamaliza nje ya Top 4 hivyo kukosa nafasi ya kushiriki UEFA Champions League msimu ujao.
Kwanini nasema hivyo? Ni kwasababu Guardiola bado hajajua jinsi ya kukabiliana na soka la Kiingereza ambalo hutumia nguvu nyingi kuliko akili, kuna muda unahitaji point 3 muhimu hata kama timu haichezi mpira, yeye analazimisha timu icheze vizuri kisha ndio ishinde. Ligi ile si Ujerumani au Uhispania pale ni Uingereza ligi ya kibabe. Kwahiyo kama asipobadilika top 4 ataisikia kwenye bomba tu.
TOP 4 yangu mwisho wa msimu:
1.Chelsea
2.Liverpool
3.Spurs
4.Arsenal
Du yaani hata man u haipo?
round ya kwanza ndo hiyo inakata. Table inasomeka hivi, wanaopewa nafasi ya kuchukua kombe ni hao kwenye red.
Top 4 kwa harakaharaka ni hao kwenye red.
Mpira sio fikra zako wewe kama wewe bali ni hatua wanazochukua hao waalimu wa mpira, kwenye mechi ya man city na man u, mou alikuwa na kalamu na daftari mkuu.
Jana kuna mtu alifungua uzi akasema jinsi Man city atakavyofungwa na Hotspur akaja na mawazo yake, leo ameufanyia editing. hakuwa na tofauti na wewe.
1. Kuhusu man city kutokuingia top 4 kwasababu anashinda kila mechi hata zisizo na maana anashinda, hapa unamaanisha kuwa atakuwa amechoka, kwani angeshindwa mechi ndo hatachoka?
2. nipe majibu ya kwanini hujaiweka man u kwenye top 4 yako?