Guinea-Bissau yapitisha katiba inayomzuia Rais wa mpito kugombea uchaguzi

Guinea-Bissau yapitisha katiba inayomzuia Rais wa mpito kugombea uchaguzi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Utawala wa kijeshi wa Guinea-Bissau, umepitisha Katiba ya mpito ya miezi 12 ambayo inawazuia Rais wa mpito na Waziri Mkuu kugombea katika uchaguzi ujao, wiki mbili baada ya maafisa wa Jeshi kufanya Mapinduzi ambayo yaliisimamisha Katiba.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters, hati hiyo yenye vifungu 29, iliyochapishwa Jumanne, inataka Uchaguzi wa Rais na Wabunge ufanyike mwishoni mwa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja, na tarehe ya kupiga kura itawekwa na Rais wa mpito.

Maafisa wa Jeshi nchini Guinea-Bissau, walimpindua Rais Umaro Sissoco Embalo Novemba 26 na kumteua Meja-Jenerali Horta Inta-a kama Rais wa mpito siku iliyofuata.

Ilidio Vieira Te, mtumishi wa umma na Waziri wa zamani wa fedha, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu siku moja baadaye.

Mapinduzi hayo yalifanyika siku moja kabla ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais na Wabunge.

Uongozi wa Kijeshi utadhibiti mageuzi ya kisheria na kitaasisi wakati wa mpito, ikiwa ni pamoja na kuandaa marekebisho ya Katiba iliyosimamishwa, kuunda Mahakama Mpya, kubadilisha kanuni za Vyama vya siasa na kusimamia uteuzi wa wasimamizi wapya wa uchaguzi, kwa mujibu wa hati hiyo.

Baraza la Kitaifa la Mpito lenye watu 65, wakiwemo maafisa 10 wakuu wa jeshi wanaowakilisha Kamandi Kuu ya Kijeshi, watafanya kazi kama chombo cha kutunga sheria cha mpito, hati hiyo inasema

1765436328825.png

=============

Guinea-Bissau's military junta adopted a 12-month transitional charter that bars the interim president and prime minister from running in the next elections, two weeks after officers staged a coup that suspended the constitution.
The 29-article charter, published on Tuesday, requires presidential and legislative elections to be held at the end of the one-year transitional period, with the polling date to be set by the transitional president

Army officers in Guinea-Bissau, branding themselves the Military High Command, toppled President Umaro Sissoco Embalo on November 26 and installed Major-General Horta Inta-a as interim president the following day.
Ilidio Vieira Te, a civil servant and former finance minister, was named prime minister a day later.
The coup came one day before the electoral commission was due to announce the results of presidential and legislative elections.

The Military High Command will control legal and institutional reforms during the transition, including drafting revisions to the suspended constitution, setting up a new Constitutional Court, changing regulations for political parties and overseeing the appointment of new electoral officials, according to the charter

A 65-member National Transition Council, including 10 senior army officers representing the Military High Command, will serve as a transitional legislative body, the charter says.

Guinea-Bissau, a small West African coastal nation wedged between Senegal and Guinea, has experienced repeated instability since gaining independence from Portugal in 1974, with only one president ever completing a full term in office

Following a coup in Guinea in 2021, a transitional charter stipulated that coup leader Mamady Doumbouya would not be able to run in that country's next elections.
However the country adopted a new constitution in September that dropped that provision, and Doumbouya is on the ballot in an election scheduled for December 28.
 
Akili kubwa sana hii kwa majeshi yenye akili
 
Back
Top Bottom