Guinea Bissau imelala katika pwani ya bahari ya Atlantic Magharibi mwa Afrika. Nchi hii ina deni kubwa la nje na uchumi wake unategemea sana msaada kutoka nchi za ulaya.
Nchi hii yenye eneo la kilomita za mraba 35,125 inazalisha mazao ya korosho na karanga. Pia inazalisha nyuzi za mbao na nazi pamoja na samaki wa aina ya chuchunge.
Sasa katika kuangaliaangalia nchi hii naifananisha na nchi ya Estonia ambao ni moja ya nchi mpya zilizojiunga na umoja wa ulaya.
Nchi ya Estonia ina watu milioni 1,305,605 na ina eneo la mraba karibu 45,125 kilomita za mraba.
Nnachokipenda kuhusu maendeleo ya kainchi haka ka ulaya ni matumizi ya garimoshi ziitwazo Tram ambazo hupita katika barabara za kawaida zipitazo magari.
garimoshi ya kisasa ikikatiza katikati ya mji wa Tallin huko Estonia.
Nchi ya Estonia ni ndogo sana kiasi cha kuwa vijibarabara ambavyo imebidi vijengwe kukidhi neno maendeleo.
Kamtaa katika mji wa Tullin.
Neno moja tu ambalo napenda kulisema ni kwamba maendeleo hayajali umekaa vipi, ni ubunifu, mipango madhubuti na malengo. Sisi waafrika kama hatutaweza kufanya haya, tutaendelea kuwa na mizozo na kukosa dira na mwelekeo na kubakia kuwa picha za kujifurahisha kwa wengine.