Guinea-Bissau's President Assassinated

Guinea-Bissau's President Assassinated

Contents Removed, not acceptable by JF Administration!
 
Raisi Joao Bernado Vieira wa Guinea Bissau ameuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi massa machache baada ya kuuawa kwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo.

1ecc521edeb4652c4a9615f4b3656557_article.jpg
Marehemu Joao Bernado Vieira akiwa na raisi Wade wa Senegal.

Bwana Joao Bernado Vieira alikuwa katika jitihada za kutoroka makao ya raisi na ndipo kikosi cha askari wanaomtii mkuu wa majeshi alieuliwa bwana Tagme Na Waie walipomshambulia na kumuua nyumbani kwake ikulu.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo spika wa Bunge ndie atakeshika madaraka mpaka utakapofanyika uchaguzi ndani ya siku sitini.

Nchi ya Guinea Bissau ni moja ya nchi maskini magharibi mwa Afrika na iliwahi kutawaliwa na Ureno.

Nchi hiyo yenye watu milioni 1.6 na iliosumbuliwa na mapinduzi ya kijeshi, miaka ya hivi karibuni imekuwa ikitumiwa kupitisha madawa ya kulevya yanayotokea marekani ya kusini kuelekea Ulaya.


Chanzo: AFP
 
Jamani mauaji ya viongozi Afrika yatamalizika lini? Hii ni kutokana na kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Rais wa Guinea Bissau katika makazi yake.
 
Hayo ni mauaji ya kisasi kabla ya hapo mkuu wa majeshi aliuwawa -- huyo mkuu alikuwa haelewani na raisi aliyeuwawa ndio maana

hata hivyo raisi huyo amewahi kuuwa watu kibao wakati alivyofanya mapinduzi miaka ya 80
 
upanga kwa upanga na jino kwa jino, wansiasa wanavuna wananchopanda
 
Wamechoka na ufisadi na huo ndio mwisho wa kuvumiliana kwani hili lichama litawala lililokubuhu kwa ufisadi kiasi ya kwamba wanashindwa kuchukuliana hatua usizani wanatuumiza sisi tu hata hao walioko ndani ya vyombo vya usalama wakiwemo majeshi na mapolisi nao wamo wanaozalilika ,kuchoka kwao ndiko kunakozaa mapinduzi maana hata humo wamo wanaobanwa na kuteswa ,uchuguzi mkuu uliopita watu walikaribia kufyatuliana risasi katika makambi ya jeshi baadhi wakiwa wakereketwa wa CCM na baadhi wakiwa wakereketwa wa CUF ,walianza ubishi tu na kuponda sera za kila mmoja akijitetea upande wake.
Hivyo wananchi tutapiga makelele sana za kuwanadi mafisadi lakini wapo wasioweza kukaa na kushindana kwenye majukwaa ,ole wenu mafisadi endeleeni kulinda.
 
Bwana Raimundo Pereira ambae alikuwa spika wa bunge la nchi hio, ameapishwa kuwa raisi wa muda siku ya jumanne iliopita.

5c65d9555d601646576613da6e144f4c_article.jpg
Raisi Raimundo Pereira

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hio yenye watu wasiozidi milioni 2, raisi wa muda anatakiwa aandae uchaguzi wa raisi ndani ya siku sitini.

Hali katika mji wa Bissau ni shwari na wananchi wameanza kurejea kufanya shughuli zao za kila siku ingawa wanunuzi wamekuwa na wasiwasi wa vurugu zingine.

Source: AFP
 
Last edited:
Bwana Raimundo Pereira ambae alikuwa spika wa bunge la nchi hio, ameapishwa kuwa raisi wa muda siku ya jumanne iliopita.

View attachment 3747
Raisi Raimundo Pereira

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hio yenye watu wasiozidi milioni 6, raisi wa muda anatakiwa aandae uchaguzi wa raisi ndani ya siku sitini.

Hali katika mji wa Bissau ni shwari na wananchi wameanza kurejea kufanya shughuli zao za kila siku ingawa wanunuzi wamekuwa na wasiwasi wa vurugu zingine.

Source: AFP

Nchi ina watu 1.6 m angalia data zako tena!
 
Guinea Bissau imelala katika pwani ya bahari ya Atlantic Magharibi mwa Afrika. Nchi hii ina deni kubwa la nje na uchumi wake unategemea sana msaada kutoka nchi za ulaya.

Nchi hii yenye eneo la kilomita za mraba 35,125 inazalisha mazao ya korosho na karanga. Pia inazalisha nyuzi za mbao na nazi pamoja na samaki wa aina ya chuchunge.

Sasa katika kuangaliaangalia nchi hii naifananisha na nchi ya Estonia ambao ni moja ya nchi mpya zilizojiunga na umoja wa ulaya.

Nchi ya Estonia ina watu milioni 1,305,605 na ina eneo la mraba karibu 45,125 kilomita za mraba.

Nnachokipenda kuhusu maendeleo ya kainchi haka ka ulaya ni matumizi ya garimoshi ziitwazo Tram ambazo hupita katika barabara za kawaida zipitazo magari.

tallintram.jpg
garimoshi ya kisasa ikikatiza katikati ya mji wa Tallin huko Estonia.

Nchi ya Estonia ni ndogo sana kiasi cha kuwa vijibarabara ambavyo imebidi vijengwe kukidhi neno maendeleo.

tallinstreet.jpg
Kamtaa katika mji wa Tullin.

Neno moja tu ambalo napenda kulisema ni kwamba maendeleo hayajali umekaa vipi, ni ubunifu, mipango madhubuti na malengo. Sisi waafrika kama hatutaweza kufanya haya, tutaendelea kuwa na mizozo na kukosa dira na mwelekeo na kubakia kuwa picha za kujifurahisha kwa wengine.
 
Back
Top Bottom