GUMZO la Magufuli Uchaguzi Wa Kenya

GUMZO la Magufuli Uchaguzi Wa Kenya

Habari Jamvini?,

Uchaguzi Mkuu wa Kenya [emoji1139] umefanyika siku ya Jumanne Agosti 8, 2017 ambapo kulikuwa na mchuano mkali kabisa kati ya Uhuru Kenyatta mgombea wa Jubilee na Raila Odinga mgombea wa NASA ambapo matokeo yanaonyesha Uhuru Kenyatta kumzidi Odinga kwa asilimia 10 ya matokeo mpaka sasa.

Uchaguzi wa Kenya umeshirikisha jumla ya wagombea 8 waliokuwa wanawania kiti cha urais.

Mchuano ulikuwa mkali sana na tangu mwanzo kulipoanza kampeni ambapo jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [emoji1241] Dkt.John Pombe Magufuli lilitawala sana. Kwa upande wa wagombea Urais jina la Dkt. Magufuli lilitawala na kuwa gumzo kwenye kampeni zao kwa zaidi ya asilimia 98, si Odinga wala si Kenyatta wote walikuwa wakimtaja Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli mara kwa mara kabla hawajashuka majukwaani.

Utawasikia,"Tunataka mabadiliko kama yanayotokea Tanzania ya kupambana na wezi na ufisadi katika serikali ya Magufuli", wengineo utawasikia,"Nikishinda nitaongoza nchi kama Magufuli ". Yaani lilikuwa linapotajwa jina la Magufuli uwanja mzima unalipuka kwa shangwe.

Inawezekana kabisa kushinda kwa Kenyatta ama kutikisa kwa Odinga na kuleta ushindani mkali na wa dhahiri kunatokana na wote wawili (Uhuru na Odinga) kusafiria nyota ya Rais Magufuli wakati wa kampeni ambaye alikuwa nyota ya uchaguzi wa Kenya.

Kung'ara kwa Rais Magufuli kwenye siasa zinatokana na ukweli Wakenya wengi wanampenda mno Rais Magufuli kwa namna anavyoienda nchi yake Tanzania [emoji1241].

Wakenya wengi wanavutiwa na Rais Magufuli kwa namna anavyopambana na rushwa na ufisadi Serikalini ambao umekuwa kero Kubwa kwa Wakenya wengi ambao kiwango cha rushwa na ufisadi ni kikubwa mno wanatamani wangempata Magufuli awasaidie kuondoa tatizo hilo.

Wakenya wanavutiwa na namna ambavyo Rais Dkt. Magufuli anavyotengeneza fursa za ajira nchini kwa kuhakikisha viwanda vingi vinaanzishwa, kilimo kinaboreshwa, kuwaondoa maofisini wenye majina na vyeti feki wanaoziba fursa za wenye vyeti halali. Wakenya wengi sana ni wasomi lakini wengi wao hawana ajira, wanamtamani Magufuli awatengenezee fursa za ajira.

Wakenya wanavutiwa na Magufuli kwa namna anavyotetea rasilimali za Taifa zimnufaisha Mzawa husika na si mwekezaji au mgeni. Uzalendo wa Rais Magufuli katika kulinda rasilimali za nchi ya Tanzania zimewafanya Wakenya wengi kuzidi kuongeza mahaba kwa Rais Magufuli.

Wakenya wengi wanampenda Rais wa Tanzania [emoji1241] Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyotekeleza Ilani ya uchaguzi kwa kusimamia kauli zake nyakati za uchaguzi.

Wakenya wengi wanavutiwa na Rais Magufuli kwa namna alivyoboresha nidhamu na uwajibikaji kwa Watumishi wa umma.

Kiukweli kila mgombea aliyesafiria nyota ya Rais Magufuli ameonekana kupata kura za kutosha za kushinda na wengine kuleta ushindani mkali kabisa.

Jina la Dkt.Magufuli sio tu lilikuwa likitumika Kenya bali hata kwenye Uchaguzi wa Rwanda, wametumia sana jina la Rais Magufuli wakati wa kampeni.

Mnyonge, mnyongeni haki yake mpeni. Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekuwa nyota na kipenzi cha walio wengi kwa uzalendo, uchapa kazi, usimamizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Majalida mbalimbali Afrika na Duniani wamekuwa wakimtaja Rais wa Tanzania Dkt.Magufuli kama Kiongozi wa Mfano barani Afrika.

Kuna Faidi unapokuwa Mzalendo wa kweli katika nchi yako.Rais Dkt Magufuli mfano wa kuigwa nje na ndani ya Tanzania [emoji1241].

Na Emmanuel J. Shilatu.

bc46f3997e4ed86ec424ceaa665adf82.jpg
My friend Shilatu,
Pamoja na kuandika kishabiki sana, nakupinga kwa herufi kubwa. Huku Tanzania kuna wakenya wengi sana!!! Kwa taarifa yako wanatazama na kuona na kufanya judgement ya kila kinachoendelea. Yapo yanayofanyika ambayo yanastahili kupongezwa kwa kuwa yanaonesha uthubutu wa kiongozi. Kwa bahati mbaya yapo yanayofanyika ambayo yanaleta picha mbaya si ndani tu hata nje. Ukizingatia desturi ya ubaya huwika kuliko wema ndg yangu. Ukimpa mtu sh.10,000 anaweza asimwambie mtu kuwa chakula anachokula ni wewe umempa hela, lakini ukimyang'anya hata sh.1000 tu utashangaa kila kona mtaani wanajua. Chuki, visasi na ukanyagaji wa uhuru wa kujieleza/habari ni moja ya mambo yaliyochangia kwa kiwango kikubwa sana kumuangusha yeyote aliyesema ataongoza kama jpm. Odinga alikuwa wazi kabisa kuhusu kuongoza kama jpm. Kenyatta alimtaja lakini siyo kwa namna unavyotaka kuaminisha watu hapa jukwaani. Wote walimtaja na walieleweka kwa namna tofauti. Unaposema utaongoza kama jpm maana yake ni nini? kuwakamata matajiri kuwaweka ndani ili wakupe pesa, kupambana na upinzani kwa nguvu zote, kuzuia mikutano ya kisiasa nchini kote, (mwanzoni iliruhusiwa ya ndani lakini naona na ya ndani nayo inawatia hofu), kuhakikisha mawaziri hawakohoi yaani wewe ndo mtendaji peke yako, kuhakikisha walio nacho wanaishi kama mashetani, kuhakikisha fedha yote ya umma inakuwa chini yako taasisi za fedha zikaukiwe. SIYO KENYA mkuu. Waliliona hilo, wanalielewa. Wakaona bora zimwi likujualo ambalo halikuli....! Kenyatta ana kaudikteta wake fulani lakini comparatively waliona hapana. Unajua kwanini? Kuna vita nyingine ni ya ubinafsi mno. Ni wapumbavu tu watakoshangilia matajiri wakinyanyasika na kukosa uwezo huku wakisahau matajiri hao wameajiri watu kwa mamia. Sipingi hatua za kupambana na ufisadi, lakini hizi za huku kwetu hapana ni zaidi ya upambanaji huo.Pen down!
 
Kila Tatizo lina njia zake za kutatua pia Ufisadi tulikuwa nao ni tofauti na uliyopo kwa jirani zetu hivyo basi busier mwepesi wa kupambanisha mambo hilihali ukakosa uona utafauti wake.

JPM kwa anachokifanya kwa Tanzania yetu iliyokuwa imeanza kupoteza dira ni sahihi na wengi tunamuunga mkono.
 
Muda ni jambo zuri. Muda utaamua, ila usije ukakimbia tena wakati huo, hata kama utakuwa umejifungua kuwa karibu na keybod yako
 
Wtz tumebobea kuongea na kuchambua mambo,lije suala me kufanya kazi sasa excuse kibao as if ulifanya kazi unamfanyia mtu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wtz tumebobea kuongea na kuchambua mambo,lije suala me kufanya kazi sasa excuse kibao as if ulifanya kazi unamfanyia mtu,

Sent using Jamii Forums mobile app
Likija suala la maendeleo tunapinga au tunakubali kwa kejeli,naweza kuthubutu kusema hakuna watu waajabu kama wtz sisi,tunapenda kujitawala na ujinga mambo yakiwekwa kwenye mstari milio kibao...wenye akili zao timamu wanaelewa lakini wale walioamua vinginevyo sawa!! Huyu raisi ukiweka mabaya yake na mazuri mazuri ni mengi,siasa tunazozilizia ziliwah kutusaidia nn uko kabla...watu kazi hatutaki Ila kupiga makelele tunaweza....ni bora niseme tu JPM anastahili kupongezwa sana kwa waliotayari ambao wanaumia sana wengi wao ni wale wale ambao ata angekua nani wasingekosa la kusema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom