Guys kuweni makini na wake za watu.

Guys kuweni makini na wake za watu.

Wengi huwa wanaingia Kwa wake za watu Kwa sababu wanawake wengi sio waaminifu, mtu unamuuliza umeolewa, anakijibu hapana yupo single, Sasa hapo unategemea nini?
Lakini kama uko makini Utajua tu kua huyu ni mali ya mtu
 
Katika kutimiza majukumu kadha wa kadha nilipita wizara flani, sasa hapa nimekutana na officer wa hiyo ambae pia ni mshikaji wangu kitambo sana.

Huyu jamaa ni mate wangu wa chuo enzi zile tulikua tukimtania kwa kumuita sadam husein, jamaa ni mwenyeji wa mafia yani ni mtu wa dini saaana.

Sasa katika story nikawa namuuliza vipi kaka mbna kama hauko sawa kuna tatizo, au magu anakupumulishia mirija, tukacheka na nini ila bado ilikua wazi jamaa anasumbuliwa na kitu.

Sasa katika maongezi na udadisi juu ya wizara yao nikamgusia kuna mshikaji flani ambae hapo ni bosi..

Jamaa si akapasuka kua huyu jamaa anapiga mke wake yeye anajua ila wao hawajui kama anaelewa kinachoendelea na jamaa kakili anampenda mke wake hawezi kumuacha kwani amezaa nae ndicho kinachomuuma.

Nikamshauri kua si akae wazungumze na mke wake kau hapendi hayo mambo, heee jamaa kakataa katakata akawa anasema wa kuongea nae si mke wangu dawa ni huyo anaejidai kidume, yeye amepanga kumsafiria tu kwenda kwao mafia ili amuadabishe, nikabaki mdomo wazi.

Nikachoka zaidi aliposisitiza kua unafikiri namuua wala hata simuui kaka, wala kumnyong'onyesha ila namtia upofu kwani hayo macho ndio yanampa kiburi sasa tuone, kama atafanya kazi, au ataitajika tena hapo wizarani.

Nikabaki duuh kaka dhambi unafanya, akawa ananiambia sasa unapochokoza vita ya mawe na nyumba yako ya vioo unatakaje.

Nikabaki kumuonea huruma tuu jamaa kua si muda mrefu upofu unamuingia.

Nb: kama upo humu kaka jipange au peperusha bendera nyeupe jamaa,nimeileta humu makusudi maana upofu usawa huu duuh.
Asimuhukumu kihivyo , japo jamaa kakosea sana
 
pole ila muheshimu anayekupigia muulize nini anampa mkeo..mimi nilikuwa napigiwa na konda wa daladala ilibidi nimfuate anipe maujuzi mpaka leo ndoa imepona...kumbe mke alikuwa anataka Mauno hivi sasa tukiwa chumbani ni mauno tuuu....hivi nataka hata niende Twanga pepeta kumbe jamaa alinisaidia kugundua na kipaji changu.
 
Well say... Sema kabla ya kuweka huu uzi niliongea na jamaa kwa kina nimefupisha tuu, huyu jamaa tulimpa Jina la Saddam Hussein yani anamisimamo balaa.

jamaa anaekula mali za Watu namfahamu vizuri nilishakutana nae katika semina flani flani, Labda nitenge muda nikae nae chini huyo Labda lakini sio huyu mjaidina ni ngumu na nasikitika tuu kua ata kama jamaa atapepeza bendera nyeupe Nafikiria kukubali kwa huyu mjaidina anamisimamo sio mchezo
Ndo mana nilitaka akutane na Sheikha na walimu wale wanaweza mpa mawaidha ya kupunguza kasi ya hasira, ila kama huyo mwizi wa mke wamfahamu, uangalie jinsi ya kupeleka hiyo taarifa kwake. Usiseme kama wataka kufanywa kipofu, ILA MWAMBIE KITU UNACHOFANYA NI CHA HATARI NA MUMEWE AMESHAJUA ACHA MARA MOJA.
 
pole ila muheshimu anayekupigia muulize nini anampa mkeo..mimi nilikuwa napigiwa na konda wa daladala ilibidi nimfuate anipe maujuzi mpaka leo ndoa imepona...kumbe mke alikuwa anataka Mauno hivi sasa tukiwa chumbani ni mauno tuuu....hivi nataka hata niende Twanga pepeta kumbe jamaa alinisaidia kugundua na kipaji changu.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tena amfanye awe Kaoge kabisa huyo, haiwezekani watu tunaoa halafu lije jitu kuharibu ndoa.
 
Daa!,, umenikumbusha ile nyimbo nahsi ya feruzi, " mkasa wa bosi " yani maudhui ni sawa kabisa, but huyo jamaa achunguze vizuri kwanini mkewe anachepuka na MTU flani labda mambo so mazuri hapo home labda hamna mshiko nawe ndo ukaamua umwache aende ili update mteremko wa majukumu
Kama kweli unampenda mke wako jaribu kumwendea kwa utaratibu umweleze hao huwa waelewa pale wanapojua ushagundua wanachofanya

Ila jamani watu tunapenda mteremko, MTU namhangaikia mke wangu labda nishamsomesha kila kitu mie then lijamaa linakuja linamchukua kirahisi tuu , then nami namfahamu heee,

Fanya umrudishe make wako mkuui
 
Wanatutaka Wenyewe mradi tu Usikamatwe *Hainaga Mke wa mtu si Kitu hata Chuma huliwa na Kutu*
 
Aaaah jamaa kiburi, si unajua wale itakad kalii hawataki ushenzi
Itikadi Kali na ushirikina wapi na wapi? Jambo la msingi aongee na mke wake na kumpa ushahidi wa kutosha kisha aachane nae.Miongoni mwa vitu kwavyo sisi waislamu tumeruhusiwa kutoa talaka kwa mke ni kama mwanamke ni mzinifu kama mwanamke ni mshirikina kama mwanamke hapendi dini na mengineyo ruksa kumtaliki...
 
Back
Top Bottom