Guys naombeni ushauri

Guys naombeni ushauri

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2016
Posts
2,584
Reaction score
1,885
Mambo vip waungwana mko poa!?

Daaah leo nimekutana na changamoto kwangu na naona inazidi kua kubwa na pengine inaweza kuweka dosari katika maisha yangu uko mbeleni.

Kuna mtoto mmoja wa kibantu nimempata sema kunakitu kinanikera kwa kweli na nimejitahidi kuelewa lakini wapi, nimefikiria mbali sana na kuona kua mpaka sperm zangu nisipokua makini zitaishi katika mantiki ya malezi haya, ambayo huyu binti anasimamia.

Mwanzoni niliona kama anaifanya iwe ya kiheshima sababu mwenzangu anahusisha dini sana katika mahusiano af mimi sio mtu wa kuamini dini zilizoletwa na majahazi sasa kuna wakati ananialika kanisani naenda tuu lakini moyoni siko hivyo kabisaa.

Sasa leo nimempigia asubuhi tukazungumza kidogo, lakini katika maongezi akaniomba jioni nikitoka kazini nimpitie twende kanisani, aisee aliniboa lakini sikua na namna nikakubali tuu lakini moyoni natukana na kulaani aliyetuletea dini.

Kinachoniuma mtoto nizuri lakini ni mtu wa dini sana yani no shots of liqour, no wines ni mwendo wa ulokole tuuu ninavyosema mlokole mkitoka ata sehemu mtaongea mawili lakini huyo JESUS anavyotajwa mpaka inaboa yaani daah wazungu ni wangese sana kwa kutuletea hizi dini za kimapokeo.

Binafsi sijawahi kuamini dini wala kufikiri kua kunahaja ya kwenda kuabudu dini za kimapokeo zilizo nje ya utamaduni wa mtu mweusi, sasa leo nataka nikitoka kanisani nimwambie ukweli kuhusu msimamo wangu juu ya hili lakini daaah naogopa kama ntamkosa maana misimamo yake juu ya ulokole na dini ni mkubwa na sitaki anichukulie tofauti.

Kifupi namuelewa sana lakini sielewi ulokole wake ata ncha ya sindano, yani nikipanga kuonana nae jua hiyo siku hakuna kwenda bar na nikiwa bar no kunywa, sometimes washikaji wanahoji vipi nabaki kuwazuga ila moyoni najua baada ya hapa naenda kumeet na asali wa moyo, na anataka sijui msali yani zile mambo ambazo daaah kwangu ni gunia la misumari kweli kweli.

Sio siri ni mkali haswa af msomi wa nguvu anaejitegemea na ananielewa tatizo ni hizi mambo za dini kumuacha sitaki anafaa kua mke lakini mambo zake za dini zinaninyima privace kabisaa yani daah ulokole ndio kimekua kipimo cha yeye kunipima mimi kama mume mwema ndivyo ninavyomuona na kumuelewa hivyo.

Kinachonishinda ni bora ningeigiza ili nimpate lakini hata uko kuigiza kwangu ni mtiani maana chuki niliyonayo na hizi imani za majaazi ata kwenda huko kanisani nimejikaza kiume haswa, sasa kwenda kanisani sitaki na kumuacha sitaki, guys mwenye wazo mbadala nishaurini.
 
Acha kumpotezea huyo dada muda wake hamwendani, huyo mwachie tu kuna wanaopenda mambo ya dini wataendana nae, ukisema unaigiza ili umuoe ujue kila siku utakuwa unakuja na thread nyingine kwamba ndoa imegeuka ndoano. Wasichana wazuri wasiopenda dini wamejaa sana tafadhali usije kumkosesha binti wa watu
 
Sijui kama umenilewa ndugu
 
Sijui kama umenilewa ndugu
Sasa kumuacha hutaki na dini zake pia hutaki!!!!
Unafkir kuna wazo gani la ziada? Kama huwezi kumuacha basi mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako muoane, hapo mtaishi kwa amani zaidi kulikoni umdanganye na wewe pia ujidanganye sio nzuri kwa mtu unaempenda, unless umemtamani!
 
Pole ila hamuendani na huyo mdada, na hata mkioana inaelekea utampiga stop mambo ya church.... Pamoja na malengo mengine ya mahusiano the zaidi ni kuwa na furaha, sasa kwann unajicommit kwenye mahusiano ambayo huyafurahii?? Ongea na huyo mdada then umsikie anasemaje

Usisahau pia birds of the same feathers fly together
 
Ni kweli lakini nilizani ungenipa wazp tofauti na ilo
 
You have a point ila to be honest nimefall in love hapa na anaonekana ananipenda na ananijali lakini hili la dini sio siri linanitesa si kidogo
 
Pole mkuu, Binafsi me naamini kwenye hizi dini ambazo huziamini kwahiyo automatic niko upande wa kutotaka huyo binti apate mtu wa kumtoa kwenye imani aliyonayo, japo kimsingi pia mtagombana sana kama mkioana na watoto mtawatesa maana watashindwa kuamini kanisani ama kupachukia, ndoa ya hivyo si ndoa kwakwel
 
Daah hakika shetani alaaniwe kakuongoza hadi hapa kuandika huu uzi....kijana unashetani mbaya sana ambaye kakukaa kwenye maisha yako na kama usipotubu mapema hakika moto wa milele utakuwakia nakuona kabisa moyo wako unataka kumpokea bwana kuwa mokozi wako hadi ukapenda kwa mtu anayemjua mungu lakin shetani kaitawala akili yako zaidi....kijana kama unamda nitumie namba yako tuweze kuomba pamoja ili shetani mbaya akutoke na uwe kijana mzuri na mcha bwana....nategemea shetani aliye kichwani mwako atapinga nlichokushauri lakin jitahid kunipm namba yako naweza kuomba na wew ili tumtoe shetani katika maisha yako.asante
 
Mantiki ya kuandika huu uzi sio mtoa wazo ajifunge au ashindwe kutoa wazo kwakua mimi sio beliver hapana, natamani mtu flani out there angenielewa
 
Daah hakika shetani alaaniwe kakuongoza hadi hapa kuandika huu uzi....kijana unashetani mbaya sana ambaye kakukaa kwenye maisha yako na kama usipotubu mapema hakika moto wa milele utakuwakia nakuona kabisa moyo wako unataka kumpokea bwana kuwa mokozi wako hadi ukapenda kwa mtu anayemjua mungu lakin shetani kaitawala akili yako zaidi....kijana kama unamda nitumie namba yako tuweze kuomba pamoja ili shetani mbaya akutoke na uwe kijana mzuri na mcha bwana....nategemea shetani aliye kichwani mwako atapinga nlichokushauri lakin jitahid kunipm namba yako naweza kuomba na wew ili tumtoe shetani katika maisha yako.asante
Please kama ni maombi ningeitaji ningeyapata kwa mwenzangu preacher ila nimeitaji msaada wa kimawazo so please sitaki kufika mbali ila ungenishauri vingine tuu lakini si maombi, sijui kama umeelewa thread yangu
 
You have a point ila to be honest nimefall in love hapa na anaonekana ananipenda na ananijali lakini hili la dini sio siri linanitesa si kidogo
Mkuu hamna kitu inastress n kudiscourage relationship kama mambo ya dini... At the end itabidi nyinyi mfanye uchaguzi.... ni mapenzi au dini

Hata me nna boyfriend wangu mambo ya dini hana Sana na hata mimi safari zangu za kwenda kanisani naona huwa hazimfurahishi, tunapendana kweli, lakini najua kabisa Kuna wakati utafika wa kuchagua ni mapenzi au ni Mungu, najua kabisa kwangu Mungu comes before all....you're in that situation, pole
 
Kweli unaweza kuchagua kitu ambacho hujawai kuexperince over somthing unakifeel na kukiona kila siku!?
Mkuu hamna kitu inastress n kudiscourage relationship kama mambo ya dini... At the end itabidi nyinyi mfanye uchaguzi.... ni mapenzi au dini

Hata me nna boyfriend wangu mambo ya dini hana Sana na hata mimi safari zangu za kwenda kanisani naona huwa hazimfurahishi, tunapendana kweli, lakini najua kabisa Kuna wakati utafika wa kuchagua ni mapenzi au ni Mungu, najua kabisa kwangu Mungu comes before all....you're in that situation, pole
 
Me nimekuelewa, hizo dini za walokole wale haswa wanakua wamejicommit kweli na mda wao mwingi ni mambo ya dini
Huyo hutamweza kwa kweli mana we unataka yule wa dini ya jpili tu baada ya hapo ni mtoko tu na kunywa
Apo ukute ameshaanza kukukataza uache pombe.
Btw huyo ndo yule doctor au umeopoa mwingine tena[emoji12]
 
My dear ndio huyo yani nina dozi ya kwenda kanisani kila nikitoka kazini, mpaka washikaji wanaisi nawatenga af worse part hataki wala kiwakubali my friends
 
Mungu anataka kukurudisha kundini kondoo wake Ila inaonekana wewe mbishi Shetani keshakutawala.
 
Swali. 1. mnakulana?
Kama ndio, huyo dini iko hati hati.
2. Unampenda kweli?
Kama mbili ndio na moja ndio unaweza kukomaa mkaishi naye.
Hawa huishia kwenda kumuombea uache pombe tu na mnaendelea kuishi.

Kama moja ni hapana. Huyo atakuacha usipokubali dini yake.

Yaani haya mambo mi niliyasolve day one, raha sana kuwa mkweli.
 
Duuuh kazi ninayo
 
Back
Top Bottom