Gwajima aendelea kukiona cha mtema kuni: Kesi ya Gwajima kupinga kanisa lake kufutwa yatupiliwa mbali na Mahalama Kuu

Gwajima aendelea kukiona cha mtema kuni: Kesi ya Gwajima kupinga kanisa lake kufutwa yatupiliwa mbali na Mahalama Kuu

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
20,711
Reaction score
31,331
erikali inasema haijafuta* Kanisa la Gwajima - hakuna maamuzi ya kufuta Kanisa la Gwajima linaloenda kwa jina la Glory of Christ TANZANIA Church. Na wala Barua ya kufuta haijawahi kupelekwa kwenye Kanisa hilo. Kwamba, kinachoonekana kufutwa kwenye ile Barua ya Msajili wa Jumuiya, ni Kanisa linaloitwa Glory of Christ Church (hakuna neno TANZANIA).

👆🏿 Kwahiyo, kwasababu aliyeleta Maombi ya Zuio na kutaka hali irudi kama ilivyokuwa (status quo ante) ni Glory of Christ TANZANIA Church ambaye hakuna maamuzi ya kumfuta, Serikali imeweka pingamizi kwamba Mahakama haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo.

Kama ni hivyo👆🏿, kwanini sasa Polisi walienda kwenye kanisa la Glory of Christ TANZANIA Church kuzuia shughuli zisiendelee na kuwakamata Waumini wakidai wanatekeleza Amri ya Msajili kulifunga kanisa hilo? Ni hoja ya upande wa pili wakipinga pingamizi na kusema hiyo imewafanya wakate Rufaa kwa Waziri na kuleta maombi haya Mahakamani.

Soma Pia: Serikali yalifutia usajili Kanisa la Askofu Gwajima kwa kuingilia masuala ya siasa kwa nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi

Mahakama Kuu imesema *haioni ni kwa namna gani Mamlaka yake yameporwa. Imetupilia mbali pingamizi.
 
Back
Top Bottom