Hyrax
JF-Expert Member
- May 20, 2023
- 1,458
- 4,409
Anajiita Bishop ila matendo yake kama mhuni wa kinondoni, hapendi shwari anapenda shari, mdomo usio na kiasi, ubishi, ujuaji kiburi mbele ya mamlaka ambayo ina nguvu kuliko yeye na ukoo wake wote.
Tamaa yake ya kutaka kiti cha uraisi ni njema ila nia yake moyoni juu ya kutaka kiti hicho cha urais si njema.
Kwa wale wakristo naomba tusome maandiko hapa ya Neno la Mungu kuhusu sifa za Askofu anayepaswa kuwa:
1 Timotheo 3:2-7 (NEN)
[2] Basi, imempasa mwangalizi awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha, [3] asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha. [4] Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia. [5] (Kwa maana kama mtu hajui jinsi ya kusimamia nyumba yake mwenyewe, atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu?) [6] Asiwe mtu aliyeokoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya ibilisi. [7] Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.
Sasa ukimpima huyu anayejiita huyu Askofu hizo sifa zote hana ila wengi mmejificha kwenye kivuli cha kumtazama kama mpigania haki jambo ambalo si kweli.
Ukifanya screening ya kiroho huyu mtu hana nia njema kwa kile anachokizungumza au kukipigania ana mambo yake binafsi anayoyapigania ndio maana imekuwa rahisi kulikimbia kanisa lake na kuwaacha mamia ya waumini kupata changamoto mahali pa kuabudia hilo kwake unafikiri hakuwaza kabla ?
Alishaona ataingia kwenye misukosuko lakini kwa kuwa anapigania jambo lake hakujali kabisa kuhusu maslahi ya watu wake (waumini)
Hajali kabisa kuhusu hasara anazoziingiza kwenye kanisa lake baada ya haya yote kutokea.. narudia tena mtu mbinafsi huwa hajali lolote wala mtu yeyote zaidi ya yeye binafsi na mambo yake binafsi.
Watu wote waliopotezwa na polisi wengi wao ni kwasababu ya mdomo usio na kiasi, kiburi, ujuaji na kuikosea heshima mamlaka kama wewe unabisha anza kutukana sasa hivi mitandaoni uone kama wiki utamaliza na tulivyowapumbavu tunataka kumtetea mtu aliyeinajisi mmamlaka kwa kuikosoa serikali bila heshima na matusi juu kwa Rais aliyeoko mamlakani mbaya zaidi hata huyo Lissu mnayemshabikia akifanikiwa kuingia madarakani kuna makosa atafanya na bado mtamtukana kana kwamba aliingia ikulu kwa kujipigia kura mwenyewe.
Ni kweli Serikali yetu kwenye baadhi ya mambo haipo sawa sio Tanzania tu hili ni tatizo la dunia nzima tunapishana tu uzito ila njia gani sahihi za kuondoa hayo yote bila kubishana na mamlaka.? La sivyo tuendelee kubondwa tu hivi hivi mpaka masikio yapate kusikia vizuri.
Njooni mnitukane!