mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,555
- 6,972
Tunakumbuka kuwa kulikuwa kuna fununu za jitihada za kutaka Mama asishike usukani baada ya Mzee kufariki, na hali hiyo ilichangia kuchelewa kutangawaza kifo cha Mzee mpaka pale Mkubwa wa Mapiganaji wetu alivyoingilia kati
Tunakumbuka wakati wa mazishi ya Mzee kule kijijini Mkubwa wa Mapiganaji alimwambia Mama Wapiganaji wetu wanaahidi utii kwake kama Mkubwa wetu na akamwambia ana dokezo la siri atampa wakiwa wawili tu
Ni wazi lile kundi au Genge halikuishia hapo, tulianza kusikia fununu za kutaka kutenganisha kofia ya Ukuu wa Chama na Nchi katika jitihada za kumkwamisha Mama kutawala.
Kundi/Genge hilo linaongozwa na wabunge wakiwemo Gwajima, walianzia Bungeni katika kile kilichoonekana kulinda utendaji wa Mzee, mpaka pale Mama alipotamka kuwa wanapoteza muda kubishana kwa mambo yasiyo ya msingi.
Matukio ya mifumo ya umeme kama lile la luku, moto soko kariakoo ambalo linahudumia sehemu kubwa wananchi na yanayofanana na hayo ni moja tu viashiria vya hujuma
Baada ya majaribio ya kihaini kushindwa kwa sasa, wanachofanya sasa ni kumkwamisha katika kuongoza kwa kumtanguliza mtu mwenye ujasiri na uzoefu wa kuropoka lakini pia mwenye platform ya kuongea kila mara, mtu anayezua utata ambaye akiongea atasikika na wengi, naye ni Gwajima ambaye ana nafasi kuongea kila Jumapili
Ndio kama Raia ana haki ya kutoa maoni,mawazo, dukuduku au ushauri kama Raia anayewajibika lakini ukiangalia namna ya uwasilishaji wake unagundua hana nia hiyo kama Raia anayewajibika bali ni 'vita binafsi' na Mkubwa wa nchi
Maneno kama " utaona kesho au kesho kutwa wanachanja, hizo ni feki MWAMBIENI ACHANJE ZOTE MILIONI MOJA ALIZOAGIZA"
" Hizo chanjo wanawataka mchanje kwa sababu WAMESHAKULA HELA ZA JUU wapewa pesa"
Hizo ni tuhuma, kejeli na kashfa za moja kwa moja, ni wazi wamemtanguliza front na watakuja wengine
Ukiangalia ni kwamba anamshambulia Mama sio Serikali, na hili suala chanjo ni moja tu uwanja wa MAPAMBAMO YA LILE KUNDI/GENGE DHIDI YA MAMA, haitoshia kwenye chanjo tu watakuja na kwengine lengo ni kumkwamisha na kuhakilisha 2025 wanaweka mtu wa lile kundi kama walivyotaka wao kipindi kile kabla ya kufeli.
Gwajima ni kifaranga tu, atafutwe Mama aliyempandisha kwenye chungu
Tumevuka salama kama Taifa kipindi kigumu lakini bado watu wanataka kuliingiza taifa katika mtanziko, HUU NI UHANI
MAMA umezungukwa na wengi wa hilo genge, chukulia mfano baada ya ile kaichanganya jamii na kuleta sintofahamu tulitarajia Waziri wa Afya, Katibu Mkuu wake kuongea chochote badala yake wanaongea watu wa mtaani wakina Kambakamba na Vigwangala, wasaidizi wako wamekususia hawako na wewe
Nije kwenye chanjo, serikali ilishasema sio lazima ni hiari, zimekuja chanjo tofauti mtu achague, Kama tunawasiwasi na Wazungu na Wamarekani kuna chanjo za jamaa zetu URUSI, CHINA, CUBA na hata INDIA
Haikutakiwa kuwa mjadala na kushutumu viongozi, unaweza ukawaambia watu wako wasichome ukawapa sababu, lakini kuna makundi kama vile wanafunzi wanaosoma nje, wafanyabiashara, wanaokwenda kufanya kazi nje, na hata wanaokwenda kweye ibada kuhiji Israel, Makkah hata Vatican huko ni lazima chanjo. Sasa utawanyima vipi haki yao hawa? Mwaka huu ndugu zetu Waislam wengi wamekosa ibada ya hija kwa kutokuwa na chanjo
USHAURI KWA CHAMA TWAWALA, Msimfukuze uanachama na muacheni na ubunge wake, hilo ndilo analitaka litokee yeye na waliomtuma kwa namna anavyotenda, ni makusudi kabisa ni calculated movement