Baada ya mahakama kuamua tusiendelee kuuona "ingia kati tuyaone malingo yako, bingiribingiri mpaka mpaka chini" anazochezeshwa Lissu, sinema nyingine ya Gwajima vs Muumini wa Gwajima itaanza rasmi baada ya siku kumi.
Kiliba kesharudisha mpira kwa Bishop, tuendelee kusubiri kama Bishop atatekeleza ahadi yake ya kuja kulipua bomu litakaloamua kama October tutatiki.
==================
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa elimu ya Juu nchini TAHLISO na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama asemewe Bw. Geofrey Kiliba amesema vijana wa Jumuiya hiyo watakabiliana vilivyo na Aliyekuwa mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima ikiwa ataendelea kwenda kinyume na taratibu na Miongozo yenye kuwaongoza Viongozi wa dini nchini.
Kiliba amebainisha hayo Jumatatu Agosti 18, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam, akikiri kuwa aliwahi kuwa muumini wa Askofu Gwajima na sasa anashangazwa na kauli za vitisho zinazotolewa na Kiongozi huyo wa kidini kwa Viongozi wa serikali.
"Kiongozi wa dini anakuambia baada ya siku kadhaa atazungumza jambo ambalo litamstaajabisha kila mtu? Mnatufundisha nini? kama Kiongozi wa dini uko hivyo sisi Vijana tutajifunzia wapi upole na ukarimu? Hapana, tunachukua hatua kubwa sana ya maneno yetu lakini tusilazimishane kutojali ama kutochukua hatua za tahadhari tunapowazungumzia Viongozi wa dini." Amekaririwa Bw. Kiliba.
View attachment 3445405