Gwajima: Baada ya siku kumi ukirudi, muumini wako naye katuahidi kurudi!

Mwasisi wa kuitumia TAHLISO kupenya kwa viongozi ni Paul Makonda. Wenyeviti wa TAHLISO waliofuata nao wanatamani kupita njia zile zile za Makonda.
Hizo nafasi za rais wa serikali ya wanafunzi kwenye vyuo vya serikali hushikwa mara nyingi na 'vipepeo'
 
HIVI Makonda aliwezaje kuwa kiongozi wa TAHLISO ?

KUNA MAMBO YA AJABU SANA
Alikuwa waziri mkuu wa chuo cha Ushirika, 2011/2012. Ilizoeleka wenyekiti wa TAHLISO kuchaguliwa kutoka miongoni mwa maraisi wa serikali za wanafunzi, mara nyingi wakitokea UDSM, lakini makonda nadhani alikuwa waziri mkuu wa kwanza kushinda uwenyekiti wa TAHLISO. Kipindi kile kulikuwa na siasa moto sana nchini, maana Lowassa alikuwa kesha anza safari ya matumaini, kwahiyo kambi za wawania uraisi zilikuwa zinaweka watu wao kwenye kila kanafasi kalikokuwa kakijitokeza.
 
Hawa vijana wajinga wajinga huwa wanawatoa wapi ?

Ningekuwa na mamlaka wahuni kama hawa ningewatafutia shughuli ya kufanya.
Wala hamna anayewatafuta, huwa wanajipeleka, kutafuta fursa za kuonekana na wakubwa!
 
Makonda mwenyewe mwisho wake u Karibu na mbali naivyo ashukuru anakoenda kuroga Roga watu Hadi wanamuona very decent ila Kitengoni kamwe Hawezi kuingia. Uyo dogo anatafta kick sana huku hana watu nyuma WA kumbeba tofauti na Heri James na Paul M.
Makonda anakubalika sana na system. Pia anakipaji cha kutengeneza ushawishi, kwa watu anaowaongoza na maboss wake. Mm namtabiria kuwa atafika mbali. Usishangae akiwa waziri mashuhuri baada ya uchaguzi mkuu October
 
Huyo nyau ni nani na anajishughulisha na nini?
 
Makonda anakubalika sana na system. Pia anakipaji cha kutengeneza ushawishi, kwa watu anaowaongoza na maboss wake. Mm namtabiria kuwa atafika mbali. Usishangae akiwa waziri mashuhuri baada ya uchaguzi mkuu October
Makonda anapendwa na watu wajinga Makonda ilitakiwa hawe jela ndo maana waziri mpango aliuza fanicha zake pale bandari hizo fanicha contena kibao zilikua unajua zinaenda wapi? Tokea hapo Magu alianza kukaa mbali na Makonda au hujui Magu anafariki makonda alikua tayari ameshatupwa nje ya system Magu alikuja kugundua anakumbatia moto
 
Ngoja tuone mbwai mbwai zao
 
Siasa chuoni zilitungiwa sheria kuzuiwa lakini kwa kuwa ni ccm ndio maana anajitutumua kwa kuwa ametumwa na hajui baada ya chuo ataajiliwa wapi na wakampokea
 
Mwambieni dogo anachofaya ni PROCRASTINATION kumbuka zimebaki siku tano askofu amwage mchele.
 
Makofi ya mchongo... Anayesemewa ni yule aliyekosa pumzi
 
"Kiongozi wa wasomi"
TAHLISO haina cheo kinaitwa Rais. Huo ni uongo unaoenezwa na waliowahi kupata nafasi hiyo kujipa umuhimu. Kiongozi mkuu wa TAHLISO ni mwenyekiti ambaye anamakamu wake na katibu.
TAHLISO haina jurisdiction yoyote kwenye internal affairs za wanafunzi wa chuo cha mahali pamoja na haina mamlaka yoyote ya kudai uwajibikaji kutoka katika serikali za wanafunzi.
Shabaha yake ilikuwa iwe jukwaa la pamoja la wanafunzi kuunganisha nguvu katika kudai maslahi yao mathalani mambo ya mikopo na welfare zingine. Hatahivyo Tangu wakati wa Kipala alipokuwa mwenyekiti, TAHLISO imekuwa kama idara ya serikali. Kila anayepata uenyekiti, anaitumia nafasi hiyo kujipendekeza barabara.
 
Sasa mtu anamapepo anasema pepo likimshinda NGUVU ataongea. Sasa ataongea yeye au hilo pepo.

Wote tunajua wachungaji wa kilokole wote ni wasanii akiwemo Gwajima. Kikubwa kama anahoja ajibiwe kama anaropoka apuuzwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…