Uchaguzi 2020 Gwajima, dharau hizi hutafika popote

Uchaguzi 2020 Gwajima, dharau hizi hutafika popote

Kusema mahakama ya kadhi ni kitu kisichomhusu Gwajima ni Uongo au ujinga wa kutojua!

Mahakama ya kadhi itawaadhiri wote wa-islam , wakristo, wabudha, mpaka wasiomini how?! Ukitafakari utajua.

Mahakama ya kadhi itaondoa umoja wa kitaifa, how?!, Ukishiba utajua

Imagine leo nyumbani kwenu kila mmoja aamue kuishi anavyotaka ndani ya familia eti kisa anayofanya ni yake binafsi?! Itakuwa ni familia(taifa)?

Unaweza kuwa uko sahihi kwa mengine ila kwa hili hapana

Nimeona nichangie tu hapo ulipoingiza udini kama vile wewe ambavyo umeona tu mabaya ya Gwajima ukaacha mazuri yake!

Hakuna aliyemkamilifu, kila mmoja na mapungufu yake!
Una haki ya kuwa na mtazamo lakini ujue tumezungukwa na nchi zenye mahakama hhizo na athari uzisemazo hatuzioni
 
Sisi wana Kawe tutampa Gwajima tumemchoka huyo Mdee anawaibisha wanakawe.....!! Wewe endelea na Mdee!!
 
Ina maana ninyi mnaotutaadharisha mnafikiri sisi wana Kawe hatuna akili? Maana kuhofia kuwa tunaweza tukampa Gwajima kura ni kututukana kabisa. Iko wazi gwajima hawezi kuchaguliwa na watu wanaojielewa.
Naunga mkono hoja mimi ni mwanakawe pia na sidhani kama kuna mwana kawe atampa kura sio Gwajima tu hata mtu yeyote
 
Kosa lipo wapi kama halima kapewa sifa za bi Kidude? Unajua bi kidude ni nick name? Maana ya bi kidude unaijua? Punguzeni mihemko na chuki zenu za kishenzi. Mdee kapewa sifa za mtu maarufu kabisa ukanda wa maziwa makuu.mtu mwenye award nyingi za kimataifa kwanye sanaa.bado mnamuona Gwajima mtu mmbaguzi..vp yule alimuita mrembo fulan ...uliandika post ya kukemea kauli ile ya Ki Khanithi...au ulicheka tu na ushuzi ukakutoka mambo yakaenda kama yalivyo.Nikuache kwa swali Wewe ni nani yake mdee mpaka mishipa ikutoke kumtetea ? Au dada yk anakwanguliwa na a k a bi kidude?
Ulivyoandika naona kama unajua kiswahili lakini maantiki mbona haiji? Bi Kidude kadhalilishwa huko aliko lakini ni mrembo gani kadhalilishwa kwa kufananishwa na Gwajiboy? Kwa namna ulivyoandika unaonekana ni msomi kwahiyo utakuwa unajua kuwa neno mshenzi au kishenzi kama ulivyoitumia sio tusi kabisaa
 
Unamzungumzia gwajima Mzee wa porn movies,anawadhalilisha wanawake,anawafanya huku akichukua video,yule ni shetani wa ngono hata usihangaike naye.
 
Asiyekujua uongo wako humu ni Nani? Jana nilikwambia tuwekee details za utafiti kuhusu huyo anayejiita KICHAA kushinda kwa 89% utafiti ulifanyiki lini na wapi na ukubwa wa sample ulikuwa upi? Bado unang’aa macho kwa kuwa hakuna hizo details.

Tulete picha?
 
GWAJIMA AZIDI KUHARIBU, DHARAU KWA BIBI KIDUDE NANI ATAZIVUMILIA?

Na, Robert Heriel

Mwanzo nilisema Gwajima ni Mbaguzi na mdini, sikuwahi kudhani anaudhaifu mwingine wa kudharau watu ambao hata hawahusiani na yeye kwa lolote Lile.

Nilimhusisha Gwajima na Ukabila kutokana na tuhuma zake za kutaka kuanzisha kikundi cha kikabila kutoka kabila lake chenye lengo la kumtetea Mhe. Rais ambaye anatoka Kabila lake. Nashukuru Jeshi la Polisi lilimuonya.

Pia nilimhusisha Gwajima na Udini pale alipopinga waziwazi mahakama isiyomuhusu hata kidogo, Mahakama ya Kadhi ya ndugu zetu Waislamu. Hiyo Mahakama ya Kadhi haimuhusu yeye wala sisi Wakristo, inawahusu Waislamu wenyewe na mambo yao. Sasa kilichomuwasha Gwajima ni nini atoke hadharani kupinga kitu kisichomuhusu. Hilo pia nilimuonya miaka ile.

Mwisho ni kauli yake inayohusu ndoto yake ya kugeuza misikiti kuwa Sunday school, na mashehe na maimamu kupigwa maji na kusilimishwa mbele ya msalaba. Alisema muota ndoto hafi mpaka ndoto yake itimie, kumaanisha yeye kabla hajafa atahakikisha misikiti itakuwa Sunday School. Hiyo watu wengi walimpiga, hasa mashehe, na wadau mbalimbali, mimi nami nikiwepo.

Sababu hizo ndizo zilizonifanya nishawishike kuikubalia akili yangu kuwa Gwajima hafai kupewa ubunge kwa jamii iliyostaraabika, watu wenye akili, na wenye muono wa mbali. Nilisema Gwajima anyimwe kura na wana Kawe, na mpaka sasa kundi kubwa la watu kutoka KAWE limenihakikishia kuwa halitampa kura huyo aitwaye Gwajima.

Sasa juzi juzi Gwajima katoa tena boko bila ya yeye kujielewa. Kitendo cha kumhusisha Marehemu Bibi Kidude katika siasa zake za vijembe ni dharau kubwa kwa Bibi Yetu huyo.

Kumdharau Bibi Kidude ni kudharau sanaa ya muziki hapa Tanzania na Zanzibar.
Kumdharau Bibi Kidude ni kuwadharau wanawake wanamuziki.
Kumdharau Bibi Kidude ni kuwadharau wazee wa kike waliojenga nchi hii.
Kumdharau Bibi Kidude ni kudharau harakati za haki za wanawake zilizopiganiwa na Marehemu Bibi Kidude.

Gwajima, atamuhusisha vipi Mzee anayeweza kumzaa Baba yake, na kumzaa yeye?
Gwajima wakati unatoa kauli ya kumshambulia mpinzani wako(bila shaka Halima Mdee) Ulikusudia kuwaambia nini wanaokusikiliza?

Hivi Gwajima unamchukuliaje Marehemu Bibi Kidude?

Fatuma Binti Baraka ndiye huyo Bidi Kidude anayoheshima kubwa sana katika nchi yetu kuliko hata wewe unavyodhani. Ni mwanamke aliyeweza kukomboa fikra za wanawake wengi, akaondoa dhana potofu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni ambapo akiwa na miaka 13 alitoroka kwao kwa kuepa kuolewa akiwa na umri mdogo. Bibi Kidude pia aliweza kufungua njia kwa wanawake wengi ambao walitamani kuwa wanamuziki, ukizingatia kwa zama za zamani mwanamke kujiingiza kwenye masuala ya muziki ilikuwa ni nongwa.

Bibi Kidude pia ni moja ya wanamuziki walioupaisha muziki wa Taarabu kimataifa kwa nyimbo zake za mikogo ya kipekee. Bibi Kidude pia mwalimu, kungwi wa unyago kwa mabinti wa zama zile ambao aliwafunda na mpaka anakufa hakuna ndoa iliyovunjika ambayo yeye alimfunda mwali.

Bibi Kidude anatuzo nyingi za kimataifa, siajabu wewe huna hata tuzo moja lakini unamshushia heshima Bibi yetu kwa mambo yenu ya siasa.

Bibi Kidude kaitangaza sana Zanzibar na Tanzania bara kimataifa, watalii wengi walikuja na kuburudika kwa nyimbo zake. Alafu wewe unaleta dharau za Rejareja.

Bibi Kidude anafahamika na vyombo vya habari vya ndani na kimataifa. Pengine wewe sio msikilizaji wa Redio, ungekuwa msikilizaji wa Redio huenda ungemsikia Bibi Kidude kwenye Idhaa ya Kiswahili ya DW, wimbo wake wa Mhogo wa jang'ombe. Wewe Unaleta dharau zako.

Bibi Kidude ni ICON ya kimataifa wakati wewe ni Icon ya kanda ya mashariki hapa nchini.

Bibi Kidude alitunza na kuhamasisha utamaduni wa kiafrika kwa kutumia muziki wa Taarabu, Unyago, kuuza hina, kucheza ngoma na kuzipiga, wewe unahamasisha utamaduni wa kigeni kupitia dini yako hiyo.

Dharau zako zinakunyima mambo mazuri, Gwajima unamambo yako mazuri mengi lakini kinachokuharibia ni Udini, ukabila, na dharau.

Hayo mambo matatu yatakusumbua sana wewe mwenyewe.

Lakini yanaweza kuja kutusumbua sisi watu wengine endapo utapata nafasi za juu katika maamuzi na mamlaka.

Je Kawe watakuchagua ili uwadharau?
Je Kawe watakuchagua ili ulete mambo yako ya ajabu?

Pengine hujui siasa vyema, au unajua lakini hujui namna ya kuzungumza.
Mwenzako alikuita mrembo, yaani alikushambulia wewe binafsi kwa kutumia nomino ya jumla kwa kutaja neno "Mrembo" Wewe umetumia Nomino ya Kipekee kwa kutaja jina la Bibi Kidude. Hilo ndilo kosa lako.

Ulidhamiria kumdhalilisha au kumkejeli mtu mmoja lakini umetumia mtu mwingine yaani asiyehusika(Bibi KIdude) Matokeo yake umewadhalilisha wote wawili au kuwakejeli wote wawili. Yaani Hasimu wako na Marehemu Bibi Kidude.

Ushauri wangu;
Siku nyingine ukiamua kumtukana au kumtupia mtu kijiwe/kijembe basi tumia nomino au kitu kisicho na majina ya watu waliopo nchi hii. Kwa kufanya hivyo hutaleta mgogoro kama ulivyofanya wakati huu.

Mwisho: ACHA DHARAU KWA WATU WAZIMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Mimi ndio sijaelewa au mtoa post ndio hajaelewa? Kwa sifa zote hizi ulizozitaja za Bi. Kidude, huyo aliyefananishwa naye si ndio kapewa sifa hizo? Sasa hapo ni kudhalilishwa au kukwezwa?
 
Kama anaakili nyingi afuate nilichomuambia.

Kijembe kikikutwa kwa mtu kisipige mtu asiyehusika
Hivi mnamuongelea yule "MREMBO" tuliyeambiwa kapelekwa na CCM kwa "JIKEDUME" wa Kawe? 😂😂 Mkuki kwa nguruwe....
 
Hivi Gwajima na "mtukufu" Kibwetere aliyewaua waamini wake pale Uganda kwa kuwapika unawatofautishaje? He is barbaric and a pure fula pygmy!He has to go to hell as well! Down with these fake pastors! 😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Mimi ndio sijaelewa au mtoa post ndio hajaelewa? Kwa sifa zote hizi ulizozitaja za Bi. Kidude, huyo aliyefananishwa naye si ndio kapewa sifa hizo? Sasa hapo ni kudhalilishwa au kukwezwa?


Huwezi ukaelewa Mkuu kama hufuatilii haya mambo.

Aliyetuma kijembe kaelewa na ndio maana kaomba msamaha, kwa wafuasi wa bibi Kidude.

Kasome maana ya Kijembe, Kebehi na Kejeli, utaelewa.
 
Kosa lipo wapi kama halima kapewa sifa za bi Kidude? Unajua bi kidude ni nick name? Maana ya bi kidude unaijua? Punguzeni mihemko na chuki zenu za kishenzi. Mdee kapewa sifa za mtu maarufu kabisa ukanda wa maziwa makuu.mtu mwenye award nyingi za kimataifa kwanye sanaa.bado mnamuona Gwajima mtu mmbaguzi..vp yule alimuita mrembo fulan ...uliandika post ya kukemea kauli ile ya Ki Khanithi...au ulicheka tu na ushuzi ukakutoka mambo yakaenda kama yalivyo.Nikuache kwa swali Wewe ni nani yake mdee mpaka mishipa ikutoke kumtetea ? Au dada yk anakwanguliwa na a k a bi kidude?

Huna ujuacho kwa habari ya vijembe kwenye siasa, naomba nisikuelimishe.

Gwajima mwenyewe kaomba radhi wewe unakalia chuki hapo.

Sijakataa Gwajima kumkejeli au kumkebehi, au kumpa kijembe Halima Mdee, ila amemkejeli hasimu wake kwakutumia udhaifu wa mtu mwingine, na hilo ndilo kosa alilofanya, wewe huelewi wapi. Gwajima angesema "Yule Bibi Kizee" Au "ajuza" au Nomino yoyote ya Jumla wala isingezua mgogoro. Sasa yeye kazua mgogoro kwa kuingiza nomino ya pekee yaani mtu mahususi "Bibi Kidude" ambaye watu wanamfahamu, anandugu, na anawafuasi licha ya kuwa ni marehemu. Bado hujaelewa mantiki ya uzi wangu.

Ni sawa mtu akuambie kuwa yule anasura mbaya kama "Remmy ongala" Hapo utakuwa umepiga watu wawili kwa wakati mmoja, yaani huyo unayemtania au kumkebehi na Remmy mwenyewe. Hujaelewa tuu?

Kuhusu "Nickname"
Hujui Nickname pia ni utambulisho wa Mtu,
Mtu akisema Diamond Platnum, Nay wa Mitego, Sugu, Profesa Jay hao ni watu mkuu,

Wewe bila Bibi Kidude, unafikiri neno hilo ungelisikia wapi?

Hakuna mwenye chuki na huyo Gwajima, ila mambo yake ya hovyo ndio tutayapinga. Mimi sina chama, wala sina mpango wa kuwa na chama. Napinga na kuunga mkono yeyote anayekosea na anayefanya vyema
 
Usuhamishe goli wewe unajua na kila mmoja anajua anafahamu mashambulizi yalikuwa yakiekezwa wapi.


Siwezi hamisha Goli Mkuu.

Ipo hivi, unapotuma kijembe, kejeli au kebehi kwa mtu unapaswa uwe mwerevu.

Ngoja nikupe mfano ufuatao;
Wahusika, Taikon, Geradi, Rashidi na wasikilizaji wengine.

Mazungumzo yalikuwa hivi;

Taikon: Huna Lolote Gerald
Gerald: Wewe lako lipo wapi, au hicho kipara chako ndio jipyaa(Unacheka)
Wasikilizaji na Rashidi: (wote wanamshangilia Gerald)
Taikon: Basi unadhani umeshinda siyo, kipara cha pesa hiki. Wewe vizinga tuu!
Gerald: Pesa madafu kumbe ni pesa.
Taikon: Muone ndio maana kafupi kama Rashidi! (Ninacheka)
Wasikilizaji: (Wote wananishangilia)
Gerald: (Kimya)
Rashidi: (Kimya akiwa kakunja uso)

Kupitia mazungumzo hayo nafikiri umeelewa nilichokuwa nazungumzia.
Kama hujaelewa, nikusaidie kuelewa kwa maswali haya;

1. Unafikiri kwa nini wasikilizaji walikuwa wanashangilia pande zote mbili yaani upande wa Gerald na Taikon kila mmoja alipotupa kijembe kwa mwenzake?

2. Unafikiri kwa nini Rashidi mara ya kwanza alicheka Pale Taikon alipotupiwa kijembe?
3. Unafikiri kwa nini Rashidi alikaa kimya bila kucheka uso wake akiwa ameukunja pale Taikon alipomtupia kijembe Gerald?

Bado hujaelewa?
 
Gwajima ana akili nyingi usije ukamfananisha na huyo mwanamke anayeishi kihuni

Bi kidude anayezungumziwa hapa ni marehemu na alikuwa na heshima kuwa baracna visiwani, hata nje ya nchi. Si sahihi jina lake kutumika atumiavyo Gwaj!
 
Kusema mahakama ya kadhi ni kitu kisichomhusu Gwajima ni Uongo au ujinga wa kutojua!

Mahakama ya kadhi itawaadhiri wote wa-islam , wakristo, wabudha, mpaka wasiomini how?! Ukitafakari utajua.

Mahakama ya kadhi itaondoa umoja wa kitaifa, how?!, Ukishiba utajua

Imagine leo nyumbani kwenu kila mmoja aamue kuishi anavyotaka ndani ya familia eti kisa anayofanya ni yake binafsi?! Itakuwa ni familia(taifa)?

Unaweza kuwa uko sahihi kwa mengine ila kwa hili hapana

Nimeona nichangie tu hapo ulipoingiza udini kama vile wewe ambavyo umeona tu mabaya ya Gwajima ukaacha mazuri yake!

Hakuna aliyemkamilifu, kila mmoja na mapungufu yake!
Acha ungosha ngosha, mimi ni mkristo nimeifuatilia mahakama ya kadhi katika nchi zetu Zanzibar na Kenya hayo usemayo wala hamna, labda aujui kuwa Kenya na Zanzibar Kuna kadhi hiyo mahakama inawahusu waislam tu,usipotoshe.
 
Acha ungosha ngosha, mimi ni mkristo nimeifuatilia mahakama ya kadhi katika nchi zetu Zanzibar na Kenya hayo usemayo wala hamna, labda aujui kuwa Kenya na Zanzibar Kuna kadhi hiyo mahakama inawahusu waislam tu,usipotoshe.
Kinyume cha ungosha ni u-kike

Acha ukike kike,
Hakuna japo linaloihusu jamii flani tu ndani ya jamii!

Usi-judge jina la mtu ndio maana unajiita Akili lakini ulivyojibu inaonesha kabisa bichwa ni empty set.
 
Back
Top Bottom